Jumuiya ya Wakristo na mabango pamoja na misalaba wakipaza sauti ya kutaka haki kutokana na vurugu dhini yao huko Karanwala,Karachi nchini Pakistan. Jumuiya ya Wakristo na mabango pamoja na misalaba wakipaza sauti ya kutaka haki kutokana na vurugu dhini yao huko Karanwala,Karachi nchini Pakistan.  (AFP or licensors)

UN:kila Agosti 22 ni Siku ya Kimataifa ya waathiriwa wa vurugu kuhusiana na dini

Katika taarifa iliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali Open Doors limebainisha kuwa haiwezekani kutotaja ongezeko la ghasia dhidi ya Wakristo.India (Manipur),Pakistan (Punjab),Nigeria,Cameroon,Bangladesh na nchi nyingine nyingi ni nchi ambazo ongezeko la vitendo vya ukatili vinavyoegemezwa kwenye dini dhidi ya Wakristo walio wachache ni wazi.

Na Agella Rwezaula, - Vatican.

Waathiriwa wa vitendo vya unyanyasaji kwa misingi ya dini au imani: Milango iliyofunguliwa,  na unyanyasaji dhidi ya Wakristo huongezeka. Hayo yamesikika tena terehe 22 Agosti  ambayo  ni Siku ya kuwakumbuka waathiriwa  wa vitendo vya unyanyasaji vinavyohusiana na dini au imani. Katika maeneo mengi ya migogoro duniani kote, watu ni waaathirwa wa ghasia zilizokithiri. Miongoni mwao madhehebu ya  walio wachache ndio hasa walio hatarini na mara nyingi wanalengwa. Mkristo ndiye anayelengwa zaidi ulimwenguni kulingana na ripoti ya Kituo cha Utafiti cha Pew, kilichotajwa na shirika lisilo la kiserikali laOpen Doors ambalo  kwa zaidi ya miaka 60 liimekuwa ikijitolea kusaidia Wakristo wanaoteseka kwa sababu ya imani yao. Katika dokezo lililotolewa tarehe 22 Agosti 2023, shirika hilo lisilo la kiserikali linasema kuwa: “haiwezekani kutotaja ongezeko la ghasia dhidi ya Wakristo. India (Manipur), Pakistani (Punjab), Nigeria, Cameroon, Bangladesh na nchi nyingine nyingi ni nchi ambazo ongezeko la vitendo vya ukatili vinavyoegemezwa kwenye dini dhidi ya Wakristo walio wachache ni dhahiri sana”.

Katika hafla ya siku ya kumbukumbu ya waathiria wa vurugu kwa misingi ya dini au imani, hata Papa Francisko katika ujumbe wa Twitterì, Agosti  22, 2023 aliizindua ombi la kukomesha unyonyaji wa dini kuchochea chuki, vurugu, itikadi kali na uonevu. Papa aliandika kuwa: “Narudia tena wito wangu wa kuacha kutumia dini kwa ajili ya kuchochea chuki, vurugu, misimamo mikali na ushabiki na kuacha kutumia jina la Mungu kuhalalisha vitendo vya mauaji, uhamisho, ugaidi au uonevu.” Ujumbe waka Baba Mtakatifu unachukua baadhi ya maneno kutoka katika Hati kuhusu Udugu wa binadamu, na kuishi Pamoja.

Taarifa hiyo inaripoti ushuhuda wa Wakristo waliofanyiwa unyanyasaji, kama vile huko Dhaka, Bangladesh, ambapo mtoto wa miaka minane alichomwa moto na majirani kwa sababu wazazi wake walikuwa wamegeukia Ukristo. Malalamiko ya baba huyo hayakuwa na matokeo yoyote yoyote yaani kusikilizwa. Nchini Uganda, tarehe 16 Juni 2023, kundi la wanamgambo wa Kiislamu kutoka Allied Democratic Forces (ADF) walivamia mabweni ya shule ya Lhubiriha, huko Mpondwe, magharibi mwa nchi hiyo, na kuwaua kikatili wanafunzi 37 na wanakijiji wanne. Huko Colombia, Wakristo walinaswa kati ya vikundi na vitendo vya uhasama kwa miongo kadhaa. Viongozi wa Kikristo wanaopinga makundi ya wahalifu wanatishwa, kushambuliwa au kuuawa. Katika jimbo la Manipur, kaskazini-mashariki mwa India, kwenye mpaka na Myanmar, mapigano makali yamekuwa yakishuhudiwa kwa karibu miezi mitatu kutokana na mvutano kati ya kabila lenye asili ya Hindu Meitei na wale walio wachache sana Wakristo wa Kuki-Zomi.

Idadi ya Wakristo na makanisa yalilengwa hasa. Baada ya mwezi mmoja, Wakristo 60 walikuwa wameuawa, 35,000 walikimbia, na makanisa 397 na majengo 6 ya Kikristo yalikuwa yameharibiwa. Nigeria inakusanya idadi kubwa zaidi ya Wakristo waliouawa kwa ajili ya imani yao (mwaka 2023, kesi 5,014 zilizorekodiwa. Cameroon, yenye Wakristo wengi (zaidi ya 60%), pia imekabiliwa na mashambulizi ya kikatili na wapiganaji wa Boko Haram kwa miaka kadhaa dhidi ya vijiji vya Kikristo kaskazini mwa mbali. Kwa mujibu wa Shirika la Open Doors linabainisha kuwa vurugu hujidhihirisha kwa namna nyingi: mashambulizi ya kikatili hayajidhihirishi pekee kwa mashambulizi ya moja kwa moja kwa maisha ya mwathiriwa, lakini yanaweza kuchukua aina mbalimbali za vurugu za kimwili au vifaa.

Hata hivyo, daima husababisha uharibifu unaoonekana wazi au unaoweza kupimika. Utekaji nyara, unyanyasaji wa kingono, ndoa za kulazimishwa, unyanyasaji wa kimwili na kisaikolojia, kuhamishwa, nyumba au biashara zilizoharibiwa au kuporwa ni matukio mengine ya vurugu dhidi ya Wakristo. Mnamo Julai, mwaka huu  limekumbusha shirika la  Open Doors, Bunge la Ulaya (Brussels) liliidhinisha azimio la dharura juu ya matukio ya Manipur, India. Bunge la Ulaya limeitaka serikali ya India kuchukua hatua zote zinazohitajika ili kukomesha mara moja vurugu zinazoendelea za kikabila na kidini. Miriam Lexmann, MEP kutoka Slovakia, alisema: “Umoja wa Ulaya hauwezi kufumbia macho uhalifu huu. Ujumbe wetu lazima uwe wazi: hatutageuka kutoka kwa ghasia na hatutawapa kisogo Wakristo wanaoteswa, aliongeza Ladislav Ilcic, MEP kutoka Croatia.

Vurugu dhidi ya wakristo zinazidi kuongezeka katika mataifa mengi
23 August 2023, 18:12