COP28:Maandishi yaliyoidhinishwa yana njia ngumu kuelekea siku sijazo bila mafuta
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Maandishi yaliyoidhinishwa katika COP28 yanafuatilia njia gumu kuelekea siku zijazo bila vmafuta, ndivyo Teresa Anderson, mkuu wa kimataifa wa ActionAid kwa haki ya hali ya Tabianchi alitoa maoni juu ya maandishi yaliyopigiwa kura katika COP28 katika kikao cha mwisho cha mazungumzo yao ambayo Cop28 ilihitimishwa tarehe 12 Desemba 2023. “Wakati maandishi yanatoa ishara kwamba siku za sekta ya mafuta zinahesabika, nchi tajiri zimekataa waziwazi kutoa ufadhili mpya ili kusaidia nchi zinazoendelea kufanya malengo haya kuwa ukweli unaoweza kufikiwa. Nchi tajiri zinataka kuwa na keki yao na kuila pia.” alisema Anderson. Kwa kuongezea alisema “Lakini wanapaswa kukumbuka kuwa hakuna malengo ya tabianchi ya bure.
Maandishi haya yanamaanisha kuwa nchi za kipato cha chini, ambazo tayari zina madeni kutokana na gharama za majanga ya tabianchi, zinaweza kulazimika kufanya uchaguzi usiowezekana kati ya usalama wa kiuchumi na hatua za tabianchi. Kwa kuongezea, Bi Andreson alisema: "Maandishi yanatoa mianya mingi na yanatoa zawadi kadhaa kwa wanaoitwa 'waoshaji wa kijani', ambao huficha njia halisi ya kutoka katika nishati ya mafuta na teknolojia ya 'kijani', ikijumuisha kukamata na kuhifadhi makaa, kinachojulikana kama nishati ya mpito, nishati ya nyuklia na makaa. Kwa jumla, inaelekeza njia gumu kuelekea mustakabali usio na mafuta,” alihitimisha Anderson.
Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antony Guterres kuhusiana na COP28 alithibitisha ni kipindi cha mpito wa kuondoka nishati ya mafuta na kuharakisha mpito wa nishati wa haki na wenye utaratibu kwa wote. “Tuko kwenye mbio dhidi ya wakati. Kama nilivyosema kwenye ufunguzi wa Cop28, sayari yetu iko umbali wa dakika chache kutoka usiku wa manane kwa sababu ya kikomo cha nyuzi 1.5. Na wakati unaendelea kupita. Cop28 itaisha kesho, lakini bado kuna mapungufu makubwa ya kujaza. Sasa ni wakati wa matamanio ya hali ya juu na kubadilika kwa hali ya juu.” Alisisitiza tarehe 11 Desemba 2023 wakati Kikao kinakaribia kuhitimishwa tarehe 12 Desemba 2023.
Kwa hivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ambaye kulingana naye alisema mawaziri na wapatanishi lazima wapite zaidi ya mistari nyekundu ya kiholela, misimamo iliyoimarishwa na mbinu za kuzuia. Ni wakati wa kutoa nguvu zetu zote kujadili kwa nia njema na kuchukua changamoto iliyozinduliwa na rais wa COP, Sultan Ahmed Al Jaber." “Ni wakati wa kutafuta maelewano na kutafuta suluhisho, bila kuathiri sayansi au hitaji la kufikia matarajio ya hali ya juu,” aliendelea Guterres, akitoa wito wa matamanio ya juu katika nyanja mbili. Kwanza, kabisa nia ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi. Pili, nia ya kuhakikisha haki ya tabianchi. Global Stocktake (yaani kuangalia kila kitu kinachohusiana na mahali ulimwengu unasimama juu ya hatua na usaidizi wa Tabianchi kutambua mapungufu, na kufanya kazi), lazima itoe mpango wazi wa nishati mbadala mara tatu, ufanisi maradufu wa nishati na kulenga kushughulikia chanzo kikuu cha mzozo wa tabianchi kuhusu uzalishaji na matumizi ya mafuta.
Alisisitiza katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa “Bila shaka mabadiliko hayatatokea mara moja. Mpango wa mchakato wa kupunguza kiwango cha kaboni (Decarbonisation) hasa hewa chafuzi (CO2), inayotumwa kwenye angahewa. Madhumuni yake ni kufikia uchumi wa kimataifa wenye uzalishaji mdogo ili kufikia kutoegemea katika hali ya hewa kupitia mpito wa nishati itaunda mamilioni ya nafasi mpya za kazi, lakini lazima serikali pia zihakikishe msaada, mafunzo na ulinzi wa kijamii kwa wale ambao wanaweza kukumbwa na athari mbaya. Wakati huo huo, mahitaji ya nchi zinazoendelea zinazotegemea sana uzalishaji wa mafuta lazima pia yashughulikiwe.” Onyo la mwisho kutoka kwa Katibu wa Umoja wa Mataifa alisema “ Lakini ni muhimu cha nyuzi 1.5 - na kuharakisha mabadiliko ya nishati ya haki, ya usawa na ya utaratibu kwa wote.”