Tafuta

Biashara haramu ya binadamu ni chanzo cha tatu baada ya silaha na dawa za kulevya Biashara haramu ya binadamu ni chanzo cha tatu baada ya silaha na dawa za kulevya 

Italia.Usafirishaji haramu wa binadamu ni uhalifu wa III baada ya silaha na dawa za kulevya

Waathiriwa wa usafirishaji haramu wa binadamu katika EU ni wanawake na wasichana wanaosafirishwa kwa madhumuni ya unyonyaji wa kijinsia.Takriban 1 kati ya 4 ni mtoto mdogo.Shirika la Save the Children na mashirika mengine 6 wamezindua mpango wa E.V.A.ili kupambana kwenye mipaka ya Ufaransa,Italia na Hispania.

Vatican News

Takwimu imetolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ikionesha kwamba nchini Italia biashara haramu ya binadamu inawakilisha chanzo cha tatu cha mapato ya uhalifu uliopangwa, baada ya biashara ya silaha na dawa za kulevya. Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2023, watu waliosaidiwa na mfumo wa kupambana na biashara haramu unaosimamiwa na Idara ya Fursa Sawa, walikuwa 1,477, ambapo 64.2% walikuwa wanawake na 2.4% watoto, hasa wakitoka Nigeria(51, 5%), Pakistan(6.4%), Moroco (5.5%), Brazili (4.5%), na Ivory Coast (3.9%).

Mashirika saba ya mpango wa E.V.A

Ili kukabiliana na hali hiyo na kuhakikisha wanakomesha kuibuka kwa unyonyaji wa wavulana na wasichana kutoka nchi  tatu chini ya umri wa miaka 18 na kwa wasichana wenye umri wa hadi miaka 30, wanakuwa waathiriwa wanaowezekana kwa usafirishaji na unyonyaji au hatari ya kurejea kwenye mtandao wa wanyonyaji, ushirikiano wa asasi saba za kiraia zinazofanya kazi nchini Italia, Hispania na Ufaransa, zikiongozwa na (Save the Children Italia,) Shirika la Saidia Watoto zilizindua mpango uitwao: “Utambulisho wa Mapema na Ulinzi wa Waathiriwa wa Usafirishaji Haramu katika Maeneo ya Mipaka (E.V.A)” ndani ya nchi hizo tatu. Usafirishaji haramu wa binadamu una sifa zinazofanana duniani kote, kama vile kuajiriwa katika nchi zao za asili kwa ahadi ya hali bora ya maisha katika Umoja wa Ulaya, wahamiaji mara nyingi huwa waathiriwa wa aina mbalimbali za unyonyaji katika usafiri na katika nchi wanakokwenda 

Kwa waathirika, ulinzi na njia za kuwaunganisha tena

Kama ilivyofahamisha,taarifa ya Shirika la Save the Children Italia mpango huo unalenga kutoa ulinzi na njia za kuwaunganisha na jamii waathiriwa, zilizotolewa na serikali, kupitia hatua mbalimbali zikiwemo za kupata makazi, mahali ambapo wanawake wahanga wa biashara haramu ya binadamu na watoto wao wanaowezekana kuepuka shuruti na udhibiti wa mitandao ya usafirishaji haramu wa binadamu. Raffaela Milano, mkurugenzi wa Programu za Kitaifa na Utetezi wa Shirika la Save the Children Italia alisema: “Kwa miaka mingi tumeona kwamba usafirishaji haramu wa binadamu ni jambo lililofichwa na kwamba waathiriwa waliotambuliwa mara nyingi ni ncha ya barafu, yaani hawasemi. Miongoni mwa watu walio hatarini huko kuna watoto wengi wanaotoroka mtandao wa ulinzi wa serikali kwa sababu wako chini ya wasafirishaji wasio waaminifu. Kwa kuingiliwa na UVIKO basi, mtandao wa biashara ya wahalifu ulijipanga upya kutumia huduma za kidijitali.”

Aina nyingi za unyonyaji

Kwa mujibu wake Raffaella Milano: Watu wazima na watoto wananyonywa kwa njia nyingi, na aina tofauti za usafirishaji: unyonyaji wa kingono na kazi umeenea sana, lakini pia kuna wahasiriwa wa kuomba kwa lazima, utumwa wa nyumbani, ndoa za kulazimishwa, uchumi wa uhalifu unaolazimishwa, na hivyo mpango unalenga kutambua waathiriwa wa usafirishaji haramu wa binadamu wanaohusishwa na harakati la  pili huko Ulaya na unalenga kuwa sehemu ya uingiliaji kati ambao lazima ulenge, kwa kiwango kikubwa, kutafiti jambo hilo na kuhamaisha hatua madhubuti za kuzuia, utambuzi na utofautishaji.” Kati ya 2023 na 2024, mikakati madhubuti na endelevu ya kitaifa na kimataifa itaandaliwa kwa ajili ya utambuzi wa mapema na upatikanaji wa ulinzi wa watoto na wanawake, sio tu katika vivuko vya mpaka wa Italia-Ufaransa na Hispania na Ufaransa, bali pia katika mapokezi ya Jiji la Paris na karibu na  mpaka wa Ufaransa na Italia.

Hali nchini Italia

Italia inachukuliwa na wahamiaji wengi kuwa nchi ya kupitisha. Mojawapo ya njia zinazotumiwa kutoroka nchi ni Mkoa wa Liguria. Wahamiaji kwa ujumla huvuka mji wa mpaka wa Ventimiglia na kisha kuendelea hadi Ufaransa au Hispania. Mwishoni mwa mwaka 2021, timu ya Save the Children Italia ya kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu ilifanya kazi, moja kwa moja huko Ventimiglia, na kupata tathmini ya hatari za usafirishaji na unyonyaji kati ya watoto na wanawake walio na watoto wanaovuka mpaka na Ufaransa, huku ikionesha harakati za wasichana na vijana wa Ivory Coast, wanawake wanaosafiri peke yao au na watoto, waathiriwa au walio katika hatari ya kusafirishwa. Zaidi ya hayo, safari ya wanawake vijana  wa Nigeria wanaorejea Italia baada ya kukimbilia Ufaransa ili kuepuka unyonyaji, wakiwa katika hatari ya kuuzwa tena, ilibainishwa. Kuanzia Januari hadi Novemba 2023 inakadiriwa karibu watoto 3,627 walivuka mipaka ya Ventimiglia. Sheria ya Italia dhidi ya bianshara haramu na unyonyaji inaambatana na kukuza kanuni elekezi zinazotambulika kimataifa. Sheria inatoa ujumuishaji wa waathiriwa katika utambulisho kamili, usaidizi na mpango wa ushirikiano wa kijamii. Zaidi ya hayo, inaruhusu utoaji wa kibali maalum cha makazi, kinachojumuisha kielelezo cha hali ya juu katika mapambano dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu na unyonyaji.

Usafirishaji haramu wa binadamu unaongezeka nchini Hispania

Ingawa kuna uangalizi mdogo kuliko mpaka wa Italia na Ufaransa, mpaka wa Hispania na Ufaransa pia umekuwa kitovu cha ongezeko la biashara ya wahamiaji na usafirishaji haramu, hasa wa Wanigeria, Ivory Coast na Guinea wanaoingia Ulaya kupitia mpaka wa kusini wa Hispania. Shirika la Save the Children yaani Saidi Watoto, Hispania limekusanya ushahidi madhubuti wa watu walioweza kunusurika katika ununuzi wa watoto, vijana na familia zao wanaopitia Hispania. Wasifu mwingi unaotambulika kuwa hatarishi au unaoonesha dalili za unyonyaji na unyanyasaji katika vituo vya mapokezi vya kwanza na katika maeneo muhimu kwenye mpaka wa kusini mwa Ulaya nchini Hispania huwa na harakati hatari za pili ili kufikia nchi zingine, kwa kawaida Ufaransa. Uundaji wa hatua salama za utambuzi na ulinzi katika Kaskazini unaweza kusaidia kukamilisha shughuli za sasa, kuhakikisha uingiliaji wa kina zaidi na utambuzi bora zaidi wa hali za usafirishaji haramu wa binadamu.

Vita dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu nchini Ufaransa bado hautoshi

Kati ya Italia na Hispania, hata hivyo imebainishwa kuwa Ufaransa ni kivutio na nchi ya kupitisha wahamiaji wengi waliosafirishwa kutoka Italia na Hispania. Kama ilivyoakisiwa katika ripoti ya hivi karibuni kuhusu Ufaransa(2022) na Baraza la Wataalamu wa Baraza la Ulaya la Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu,(GRETA), idadi kubwa ya walionusurika hawaripoti vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu kwa mamlaka husika, hasa kwa sababu wanaogopa kulipizwa kisasi na wafanyabiashara wenyewe kufukuzwa kutoka Ufaransa.” GRETA aidha inaakisi kwamba juhudi za kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu nchini Ufaransa bado hazitoshi na kwamba kuna haja ya haraka ya kuboresha utambuzi, ulinzi na usaidizi wa waathirika. Kuhusu utambuzi na ulinzi, mapungufu muhimu zaidi ni ukosefu wa utaalamu mahususi wa usafirishaji haramu wa binadamu miongoni mwa wafanyakazi wanaofanya kazi katika vituo vya mapokezi na ukosefu wa malazi salama kwa watu wanaosafirishwa.

29 December 2023, 11:58