Tafuta

Watu wasiopungua 160 wameuawa huko Plateau katikati mwa Nigeria. Watu wasiopungua 160 wameuawa huko Plateau katikati mwa Nigeria.  (AFP or licensors)

Mashambulizi ya silaha katika maeneo 20 nchini Nigeria na kuua watu 160

Serikali ya Plateau katikati mwa Nigeria,imetangaza kuwa raia wasiopungua 160 waliuawa katika mashambulizi kadhaa yaliyotokea katika maeneo mengi ya eneo hilo ambalo ni takriban kilomita 200 kutoka mji mkuu Abuja.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Taarifa ya kwanza iliyowasili Dominika tarehe 24 Desemba na ilizungumza kuhusu waathirika 16 katika Wilaya ya Plateau, katikati mwa Nigeria. Lakini siiku ya Jumatatu tarehe 25 Disemba 2023 idadi ya watu iliongezeka mara kumi ambapo ilithibitishwa kuwa vifo 160 vilisababishwa na mashambulizi mengi ambayo yalitokea karibu na maeneo 20 katika eneo hilo. Hayo yalibainishwa na Makao ya Wilaya, ambapo ilizungumza kuhusu majambazi walioshambulia takriban vituo 20 vya watu kati ya Jumamosi 23 Desemba jioni na Jumatatu asubuhi 25 Desemba 2023.

Katika serikali ya Plateau kwa hiyo, migogoro kati ya jamii mbalimbali zinazoishi humo ni ya mara kwa mara na zikiambatana na vurugu na mara nyingi huhusisha wachungaji na wakulima ambao hushambuliana hasa kutokana na migogoro. Wachungaji kwa kiasi kikubwa ni Waislamu, huku wakulima wengi wao wakiwa Wakristo, jambo ambalo kwa miaka mingi limechangia kuibua vurugu hizi kwa kuchochewa na sababu za kikabila. Vurugu ambazo athari za mabadiliko ya tabia nchi kwenye kilimo pia huchangia.

Paul Dakete, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Makabila ya Plateau, alisisitiza kuwa mauaji hayo yamegeuza kile kilichopaswa kuwa sikukuu ya Noeli na kuwa kipindi cha maombolezo na kuzitaka mamlaka hizo kukomesha mashambulizi hayo kwa sababu “ukichaa lazima ukomeshwe.” Kwa hiyo uhasama ulioanza Jumamosi 23 Desemba uliendelea Jumatatu tarehe  25 Desemba asubuhi. Kassah, Mwenyekiti wa Wilaya ya Bokkos  alisema  na  “zaidi ya watu 300 walijeruhiwa na kuhamishiwa katika hospitali za Bokkos, Jos na Barkin Ladi.”

Habari zaidi kutoka kwa ofisi ya Amnesty International  huko Nigeria ambayo iliambia Ofisi ya Habari ya Associated kwamba hadi sasa imethibitisha vifo 140 katika maeneo yenyeWakristo wengi wa Bokkos na Barkin-Ladi, kulingana na takwimu zilizokusanywa na wafanyakazi wake wa uwanjani na maafisa wa eneo hilo. Inahofiwa kuwa idadi hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi kwani baadhi ya watu hawajulikani waliko na kuhusiana na mashambulizi  bado hayajadaiwa sababu zake.

28 December 2023, 14:43