Rais wa COMECE anakaribisha uamuzi wa kihistoria wa Baraza la Ulaya
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ulaya inatoa nuru kwa mazungumzo Ukraine na Moldovia kujiunga na Umoja wa Nchi za Ulaya(EU). Huu ni uamuzi wa kihistoria. Alikuwa amesema hayo Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel, katika Tweet yake kwamba kulikuwa na nuru ya mazungumzo ya kujiunga, na kueleza jinsi ambavyo kulikuwa na ugumu hasa kati ya Wakuu wa Nchi na Serikali katika mkutano wa Brussels. Kiti kilichoachwa tupu na Viktor Orban, wakati viongozi wengine 26 wa Baraza la Umoja wa Ulaya walipiga kura ya ndiyo kwa Ukraine na Moldovia ni picha ya siku hiyo ya kwanza ya kilele cha mkutanowa Brussels na kilikuwa ni kipengele muhimu kilichopendelea azimio la haraka la mazungumzo.
COMECE kupongeza Ukraine na Moldavia
Kufuatia na tukio hilo akizungumzia juu ya uamuzi wa Baraza la Umoja wa Nchi za Ulaya kuhusu upanuzi wake, Askofu Mariano Crociata, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Nchi za Umoja wa Ulaya (COMECE,) alitoa taarifa Ijumaa 15 Desemba 2023 akiipongeza Ukraine na Moldavia kwa maana ya uamuzi wa kujiunga na Nchi za Umoja wa Ulaya na pia Nchi ya Georgia kupewa hadhi ya Nchi Mgombea. Rais alisema: “Kwa niaba ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya, napenda kuwapongeza Ukraine na Moldovia kwa maamuzi ya kihistoria yaliyochukuliwa jana na Baraza la Ulaya juu ya ufunguzi wa mazungumzo ya kujiunga na Umoja wa Ulaya, pamoja na Georgia kwa kupewa hadhi ya nchi mgombea. Vile vile ninaelezea matumaini yangu kwamba mazungumzo ya kujiunga yanaweza kuanza hivi karibuni na Bosnia na Herzegovina, mara tu vigezo muhimu vitakapopatikana.”
Maamuzi ni ujumbe madhubuti ya matumaini
Maamuzi ni ujumbe madhubuti wa matumaini kwa wananchi wa nchi zinazotaka uanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) wa baadaye, ambao wamesubiri kwa muda mrefu wakati huu kwa imani, kuvumilia magumu na sadaka. Kwa mtazamo wa kukamilisha Umoja wa Ulaya, ushirikiano wenye mafanikio wa Umoja wa Ulaya wa Balkan Magharibi pamoja na nchi za Ulaya Mashariki una umuhimu wa kimkakati kwa utulivu, ustawi na amani katika bara la Ulaya. Mchakato unaoaminika wa upanuzi wa Umoja wa Ulaya (EU), hata hivyo, hauhitaji tu nchi zinazogombea kuendelea kufanya mageuzi yanayohitajika, lakini pia unamaanisha kuwa Umoja wenyewe unahitaji kuwa tayari kukaribisha wanachama wapya hivi karibuni. Umoja wa Ulaya (EU ) kubwa na tofauti zaidi hautalazimika kufikiria tena masuala fulani ya kisiasa, kiutawala na ya bajeti, lakini pia utahitaji kugundua tena msingi wetu wa kawaida wa dhamana na vifungo maalum ambavyo vinatuunganisha kama familia ya Ulaya.”https://www.comece.eu/eu-enlargement-comece-president-welcomes-yesterdays-historic-decision/
Ukraine na Moldovia zilikuwa zimetuma maombi ya kujiunga na Umoja wa Ulaya kufuatia uvamizi wa Urussi nchini Ukraine mnamo Februari 2022, na Umoja huo ukawapa hadhi rasmi ya kuwa mgombea mnamo Juni mwaka huo huo. Mwezi mmoja uliopita Tume ilikuwa na matumaini ya kuanza kwa mazungumzo. Sasa Baraza la Ulaya limeamua kwamba utaratibu unaweza kuanza. Uamuzi huo ulichukuliwa kwa kauli moja na nchi 26 wanachama huku Waziri Mkuu wa Hungaria, Viktor Orban, ambaye mara zote alisema anapinga, huku akikataa haki yake ya kura ya turufu, akatoka nje ya chumba wakati wa majadiliano. Hata hivyo, njia ambayo nchi hizo mbili zitalazimika kupitia ili kuingia kwenye Muungano bado ni ndefu.
Mchakato wa Moldavia na Ukraine
Moldovia na Ukraine kiukweli zitalazimika kujibu vyema baadhi ya vigezo kama vile kuheshimu demokrasia na haki za binadamu, uhuru wa kimsingi na utawala wa sheria, pamoja na uwepo wa uchumi huria na wa ushindani wa soko. Katika awamu ya mwisho, uanachama lazima uidhinishwe kwa kauli moja na Nchi zote 27 Wanachama. Kuhusu mchakato wa kujiunga, muda ambao unaweza hata kuzidi miaka kumi, Rais wa Baraza la Ulaya, Bwana Charles Michel, alisema kwamba ripoti ya kwanza itachapishwa mapema mnamo Machi 2024.
Upinzani wa Hungaria dhidi ya Ukraine
Nchi pekee iliyopinga waziwazi kufunguliwa kwa mazungumzo ilikuwa Hungaria. Waziri Mkuu wa Hungaria Bwana Viktor Orban baada ya kuondoka kwenye chumba hicho ili asizuie uamuzi huo, hata hivyo alionesha upinzani wake kwenye Facebook: “Kujiunga kwa Ukraine kwa EU ni uamuzi usio sahihi. Hungaria haitaki kuwa sehemu ya uamuzi huu mbaya.” Kwa upande mwingine nchi zingine 26 zilisisitiza kwamba uamuzi huu uchukuliwe. Hii ndiyo sababu Hungari imeamua kwamba "ikiwa Nchi 26 wataamua kufanya hivyo, itabidi waende zao," aliandika Orban. Wakati huo huo Rais Volodymi Zelensky wa Ukraine alifurahi na kutoa maoni yake kuwa: “Ushindi kwa Ukraine ni wa Ulaya yote. Wakati utakuja ambapo tutaweza kusherehekea kujiunga kwa Ukraine katika Umoja wa Ulaya (EU)."
Amani ya Ukraine itakuwapo baada ya ufikiaji malengo ya Urussi
Urussi haikukosa kutoa neno kupitia taarifa ya Rais wa Urussi Vladimir Putin, ambaye wakati wa mkutano wa kawaida wa waandishi wa habari mwishoni mwa mwaka alisema: “Amani nchini Ukraine itakuwepo wakati Urussi itafikia malengo yake.”