Tafuta

Wanawake kwa huzuni wa wapendwa wao na uharibifu mkubwa huko Gaza unaondelea. Wanawake kwa huzuni wa wapendwa wao na uharibifu mkubwa huko Gaza unaondelea.  (AFP or licensors)

Vita vinaendelea katika Mashariki ya Kati,WFP:raia wanakufa kwa njaa

Vifo 241 zaidi huko Gaza kulingana na Hamas,wakati Israel inasema kwamba vita bado vitadumu miezi kadhaa kwa wakati muhimu wa ushindi.Umoja wa Mataifa unalaani hali ngumu ya kibinadamu inayoendelea katika maeneo hayo.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Ilikuwa Noeli ya umwagaji damu ambayo Nchi Takatifu ilipitia. Kwa mujibu wa vyanzo vya Wapalestina, walisema kulikuwa na  mamia ya wahanga wa shambulio la bomu la Israel, wakiwemo 106 usiku wa kati ya mkesha wa tarehe  24 na 25 Disemba 2023. Mkuu wa Wafanyakazi wa Israel Halevi alisema kuwa Israel itawasiliana na uongozi wa Hamas, “iwe ni kuchukua juma moja au iwe kuchukua miezi, na itaongeza shinikizo kwa njia mbalimbali ili kuwezesha kutekelezwa kwa malengo ya vita, uharibifu wa Hamas na kurudi kwa mateka.” Halevi aidha alizungumzia kukithiri kwa ghasia katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, huku akisema kuwa “vikosi vya Israel vinaendelea kufanya kazi usiku na mchana kukabiliana na kutokomeza ugaidi katika maeneo ya Yudea na Samaria, na kufanya hivyo kwa mafanikio makubwa.”

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, shirika kubwa zaidi la kibinadamu duniani, linaripoti kwamba raia katika Ukanda huo wanakufa kwa njaa. Mwezi mmoja uliopita shirika la Umoja wa Mataifa lilionya juu ya hatari hii. Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za wakimbizi wa ndani pia alisema: "Israel inafanya kazi ya kuwafukuza raia kutoka Ukanda wa Gaza.” “Israel inatafuta kubadilisha kabisa muundo wa wakazi wa Gaza kwa amri zinazoongezeka kila mara za kuondoka na mashambulizi makubwa na ya kimfumo dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia,” Paula Gaviria Betancur alisema katika taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu. Tangu kuanza kwa vita, asilimia 85 ya wakazi wa Gaza wamekuwa wakimbizi wa ndani, tunasoma katika taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa.

Ufaransa inasikitishwa sana na tangazo la mamlaka ya Israel kwamba mapigano huko Gaza yatazidi na kurefushwa, wakati ambapo mashambulizi ya kimfumo yamesababisha idadi kubwa ya vifo vya raia katika siku za hivi karibuni.” Haya ndiyo tuliyosoma katika barua iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa. Na Rais wa Marekani Joe Biden alimpigia simu Emir Tamim bin Hamad Al Thani wa Qatar kujadili vita kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa taarifa iliyobebwa na shirika rasmi la habari la Qatar. Taarifa ilisema watu hao wawili walizungumza, miongoni mwa mada nyingine ni kuhusu “juhudi za upatanisho wa pamoja ili kutuliza hali na kufikia usitishaji wa kudumu wa mapigano." 

Operesheni kubwa ya kijeshi ya Israel iliripotiwa katika kambi ya wakimbizi ya Nur Shams katika Ukanda wa Magharibi kwa usiku wa tatu mfululizo. Hayo yaliripotiwa na shirika la habari la  Al Jazeera, kulingana na shambulio la ndege isiyo na rubani na Wapalestina sita waliuawa. Wafanyakazi wa hospitali hiyo walisema, tena kulingana na chanzo, wafanyakazi wa matibabu na gari la wagonjwa walizuiwa kuwafikia waliojeruhiwa. Washambuliaji wa Israel wanasemekana kuwa wamekaa juu ya paa za majengo kadhaa huko Nur Shams. Jeshi la Israel limetangaza hata hivyo kuhusu  kifo cha wanajeshi wengine watatu katika mapigano ya Jumanne tarehe 26 Desemba 2023  kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, na kufanya idadi ya waliouawa katika operesheni ya ardhini dhidi ya Hamas kufikia 164. Katika taarifa iliyonukuliwa na vyombo vya habari vya ndani, Jeshi la Ulinzi la Israel lilitaja kwamba wathiriwa ni wanajeshi wawili wenye umri wa miaka 20 na 21 na naibu kamanda mwenye umri wa miaka 23.

Habari za ulimwengu wa vita na ghasia
28 December 2023, 12:05