Mashariki ya Kati,kamanda wa Hezbollah auawa Lebanon
Vatican News
Lengo jipya lililofikiwa katika vita vya Israel dhidi ya Hamas na washirika wake wa Kishia,tarehe 7 Januari 2024, kamanda wa Hezbollah Wissam Hassan Tawil aliuawa akiwa ndani ya gari katika kijiji cha Majdal Selm, karibu kilomita 6 kutoka mpaka na Israel. Uvamizi huo ulianza baada ya shambulio la Hezbollah dhidi ya kituo cha ulinzi wa anga cha Israel kwenye Mlima Meron.
Lebanon yasema ndiyo katika azimio la UN
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Lebanon Abdallah Bou Habib alitangaza kuwa nchi hiyo iko tayari kutekeleza azimio namba 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo linatoa udhibiti kamili wa jeshi hadi mpakani na kupokonywa silaha kwa Hezbollah ambayo haitaweza kupelekwa kusini mwa nchi hiyo kwenye Mto Litani. Kwa upande wake, Tel Aviv ni thabiti katika lengo la kurudisha angalau watu elfu 80 nyumbani kwa usalama huko Galilaya".
Blinken aliwasili Israel
Hatari ya kuongezeka kwa mzozo katika eneo hilo ndio msingi wa safari mpya ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ambayo ni ya nne tangu kuanza kwa mapigano hayo tarehe 7 Oktoba 2023 na ambaye baada ya Saudi Arabia alitua Israel usiku wa tarehe 7 Januari 2024. Kwa mujibu wa Waziri huyo alisema: “ Vita havina maslahi ya mtu yeyote,” huku akisisitiza haja ya kujenga mustakabali salama pia kupitia kuundwa kwa taifa la Palestina huko Gaza. Blinken pia kuna lile la kupunguza kasi ya mapigano huko Gaza, ili kuruhusu Wapalestina kurudi polepole kaskazini mwa Ukanda huo, dhana kwamba Israel ingeruhusu tu kwa kubadilishana na kuachiliwa kwa mateka zaidi kutoka sehemu ya Hamas.
Hali katika Ukanda wa Gaza
Wakati huo huo, vita vya upande wa kusini vimeingia katika awamu mpya yenye sifa ya operesheni maalum na mashambulizi machache, ya angani na ya ardhini, kwa ajili ya ulinzi zaidi wa raia. Wakati huo huo, malori 202 ya misaada ya kibinadamu yamewasili katika Ukanda huo, hasa yakisafirisha chakula, maji safi na dawa. Hali, hata hivyo, bado ni ngumu sana kwani kulingana na makadirio, idadi ya vifo imefikia watu 23,0000.