Mkutano wa Italia na Afrika mjini Roma:makumi ya viongozi wa kisiasa wanahudhuria
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Kuna takriban nchi arobaini za Kiafrika zilizopo mjini Roma, Italia kwa ajili ya Mkutano wa Italia na Afrika, uliofunguliwa Dominika jioni, tarehe 28 Januari 2024, katika ukumbi wa Taifa na unaendelea katika Seneti na majopo mbalimbali. Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Bi Ursula von der Leyen, pia aliwasili katika Ikulu ya Italia kwa ajili ya mkutano huo.
Kabla yake, rais wa Bunge la Umoja wa Ulaya EU, Bi Roberta Metsola, na rais wa Baraza la Ulaya, Bwana Charles Michel, walikuwa tayari wameingia. Lengo lao ni kutoa fedha kwa nchi za Afrika ili kukuza maendeleo ya kiuchumi. Nchi nyingi zinawakilishwa katika ngazi ya wakuu wa nchi na serikali, na wengine na wakuu wa diplomasia au mawaziri wa ngazi ya juu, walioitwa jijini Roma kwa Mkutano huu ambao tayari ni mpango unaobeba kauli mbiu: "Italia-Afrika, daraja la ukuaji wa pamoja." Wazo ni kuwasilisha Italia kama daraja kati ya Ulaya na Afrika, ili kuipatia bara la zamani mabonde mapya ya usambazaji wa nishati na uwekezaji mkubwa kwa Afrika.
Serikali ya Italia inakusudia kuwasilisha Mpango wa Mattei kwa kila mtu kwa undani, mpango ulioongozwa na Enrico Mattei, mwanzilishi wa Eni,(shirika la mafuta)ambaye, tayari katika miaka ya 1950, alifanya kazi katika uhusiano wa ushirikiano na nchi za Afrika, akiwasaidia kuendeleza rasilimali zao za asili. Kwa Waziri Mkuu wa Italia, Bi Giorgia Meloni, Mpango wa Mattei anabainisha kuwa: "unaweza kutegemea euro bilioni 5.5 kati ya mikopo, shughuli za zawadi na dhamana: takriban bilioni 3 kutoka katika mfuko wa tabianchi ya Italia na bilioni 2.5 na nusu kutoka mfuko wa ushirikiano wa maendeleo." Waziri Mkuu Meloni aliongeza kuwa Italia inafanya "chaguo sahihi la sera ya kigeni, ambayo italeta kuhifadhi nafasi ya heshima kwa Afrika katika ajenda ya yetu ya Urais wa G7."
Italia, ambayo inaongoza G7 katika nusu ya kwanza ya mwaka, kwa hakika imejitolea kufanya maendeleo ya Afrika kuwa mada kuu ya mamlaka yake. Ni mara ya kwanza katika Mkutano wa Italia na Afrika, ambao hadi sasa umekuwa ukifanyika mara kwa mara katika ngazi ya mawaziri, umepandishwa hadhi ya kuwa kilele cha Wakuu wa Nchi na Serikali; na ni tukio la kwanza la kimataifa kufanyika nchini Italia tangu kuanza kwa Urais wa G7, ambapo ni muhimu na kusisitiza umuhimu ambao Italia inatoa kwa ajili ya ushirikiano na mataifa ya bara la Afrika.