Moto wateketeza kambi ya wakimbizi wa Rohingya:watoto 3,500 hawana makazi
Vatican News
Moto uliteketeza kambi ya wakimbizi wa Rohingya tarehe 7 Januari 2024, na kuwaacha watoto 3,500 bila kuwa na makazi na 1,500 bila kuwa na elimu. Habari hizo zimetolewa na Shirika la Kimataifa la Watoto UNICEF ambalo kwa kifupi linaeleza “rambirambi zake kuu kwa wakimbizi 5,000 waliopoteza makazi yao katika Kambi ya 5 ya kambi za Cox's Bazar. Wakati tunashukuru kwamba hakuna majeruhi walioripotiwa, lakini karibu watoto 1,500 walipoteza fursa ya kupata elimu wakati vifaa vya shule 20 viliharibiwa na moto,” alisema Mwakilishi wa Unicef nchini Bangladesh, Sheldon Yett. Kwa kuongezea alisema: “Tunapotathmini kiwango kamili cha uharibifu, UNICEF na washirika watajenga mahema ya muda ili kuruhusu watoto kujifunza wakati madarasa yanajengwa upya.”
Shirika la Umoja wa Mataifa na washirika wake waliripoti kwamba: “wamefanya kazi usiku kucha kulinda na kusaidia watoto waliopatwa na kiwewe na familia zao: “Tunakumbuka kwamba watoto hawa tayari wameepuka ukatili na kiwewe. Kwa hiyo ni muhimu kufanya kazi kwa karibu na mamlaka za mitaa, na kwamba watoto hawa wamekimbia kiwewe.” Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wabia wanataka kuwapatia walio hatarini zaidi makazi na kushughulikia mahitaji yao ya kimsingi, ili watoto wote walioathirika wawe salama, wenye afya na kulindwa.”