Familia mjini Tel Aviv zimeadhimisha siku 100 tangu walipotekwa katika shambulio la kigaidi la Hamas. Familia mjini Tel Aviv zimeadhimisha siku 100 tangu walipotekwa katika shambulio la kigaidi la Hamas.  (ANSA)

UNICEF kuhusu hali ya watoto katika Serikali ya Palestina

Mwakilishi Maalum wa UNICEF kwa Palestina akizungumza waandishi wa habari 13 Januari 2024 katika Jumba la UN huko Geneva alisema kuwa:Hakuna sehemu iliyo salama katika Ukanda wa Gaza.Mashambulizi ya mabomu na migogoro yanaendelea katika maeneo ya wakazi wengi inatishia maisha ya raia na wafanyakazi wa kibinadamu.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Mwakilishi wa Maalumu wa UNICEF katika Serikali ya Palestina, Lucia Elmi ametoa tamko lake wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 13 Januari 2024  kwenye ukumbi wa Jumba la Umoja wa Mataifa mjini Geneva. Kwa mujibu wake alisema “Baada ya takriban siku 100 za ghasia, mauaji, mabomu na kufungwa kwa watoto huko Gaza, mateso yamekuwa mengi sana. Kila kukicha, watoto na familia katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na hatari inayoongezeka ya vifo kutokana na mashambulizi ya anga, magonjwa kutokana na ukosefu wa maji salama, na kunyimwa chakula.” Na kwa watoto wawili wa Israel ambao bado wanashikiliwa mateka huko Gaza, katika jinamizi hilo lililoanza mnamo tarehe 7  Oktoba 2023 linaendelea. “Na hali inaendelea kuzorota kwa kasi. Juma lililopita UNICEF ilizungumza kuhusu “tishio mara tatu” linalowaandama watoto katika Ukanda wa Gaza ambapo ni migogoro, magonjwa na utapiamlo. Tunafanya kila tuwezalo, lakini tunakabiliwa na changamoto kubwa katika kushughulikia masuala haya.” Watoto wa Gaza wanaishiwa na wakati, wakati sehemu kubwa ya misaada ya kibinadamu ya kuokoa maisha wanayohitaji sana inabakia kukwama kati ya mikondo isiyotosheleza na viwango vya muda mrefu vya ukaguzi. Mahitaji yanayoongezeka na mwitikio mdogo  na ndio mtindo wa  maafa ya idadi kubwa. Maelfu ya watoto tayari wamekufa, na maelfu zaidi watakufa haraka ikiwa hatutatua vizuizi vitatu vya haraka ambavyo ni:

KWANZA - USALAMA: Hakuna sehemu iliyo salama katika Ukanda wa Gaza. Mashambulizi makali ya mabomu na migogoro inayoendelea katika maeneo ya mijini yenye wakazi wengi inatishia maisha ya raia na wafanyakazi wa kibinadamu. Mabomu hayo pia yanazuia uwasilishaji wa misaada inayohitajika sana. Nilipokuwa Gaza Juma lililopita, tulijaribu kwa siku 6 kupata mafuta na vifaa vya matibabu kaskazini na kwa siku 6 vikwazo vya harakati vilituzuia kusafiri. Wenzangu katika Gaza walikabili changamoto hiyo kwa majuma kadhaa kabla ya kuwasili kwangu. Familia za kaskazini zinahitaji sana mafuta haya kuendesha miundombinu ya maji na usafi wa mazingira. Bado wanasubiri.

PILI – KUFIKISHA MISAADA: Msaada bado haujatosha - jana ni lori 139 tu zilizoingia (73 kutoka Rafah na 66 kutoka KS). Mchakato wa ukaguzi unabakia kuwa wa  polepole na hautabiriki. Na baadhi ya nyenzo tunazohitaji sana zinaendelea kuwa mdogo, bila uhalali wazi. Hizi ni pamoja na jenereta za kusambaza maji kwenye vituo vya maji na hospitali, na mabomba ya plastiki kukarabati miundombinu ya maji iliyoharibiwa vibaya. Zaidi ya hayo, mara tu msaada unapowasili, kuna matatizo makubwa katika kuisambaza katika Ukanda wa Gaza, hasa kaskazini na hivi karibuni pia katika eneo la kati. Kukatika kwa mawasiliano mara kwa mara hufanya iwe vigumu sana kuratibu usambazaji wa misaada na kuwafahamisha watu jinsi ya kuipata na kwa wakati gani. Msongamano upande wa kusini, kutokana na kuhama kwa watu wengi na hitaji kubwa, inamaanisha matukio ya mara kwa mara ya watu waliokata tamaa kusimamisha lori na kujaribu kunyakua chochote wanachoweza. Upungufu wa mafuta na malori ndani ya Ukanda na uharibifu mkubwa wa barabara hufanya usafiri kuwa wa polepole na wa kawaida.

TATU – BIASHARA: “misaada ya kibinadamu pekee haitoshi. Kiasi cha bidhaa za kibiashara zinazouzwa katika Ukanda wa Gaza lazima kiongezeke, na kwa haraka. Angalau lori 300 za kibinafsi za mizigo zinahitajika kwenda kila siku. Hii itasaidia watu kununua mahitaji ya kimsingi, kupunguza mivutano ya jamii na kuongeza programu za usaidizi wa pesa zinazotolewa na UNICEF na wengine. Lakini tunaona mabadiliko kidogo sana na, kusema ukweli, matokeo yanapimwa kila siku katika kupoteza maisha ya watoto. Usitishaji vita wa mara moja na wa kudumu ndiyo njia pekee ya kukomesha mauaji na kujeruhi watoto na familia zao na kuwezesha utoaji wa haraka wa misaada inayohitajika sana. Lakini tunapoendelea kuuliza na kushinikiza hili lifanyike, tunahitaji haraka: Vivuko vyote vya mpaka kwenye Ukanda wa Gaza vimefunguliwe; Uidhinishaji wa misaada na michakato ya ukaguzi iwe haraka, yenye ufanisi zaidi na inayotabirika;  Shughuli za sekta ya kibiashara/binafsi zianze  tena; Kiasi kikubwa cha mafuta kiingie mara moja na kinaweza kuvuka Ukanda wa Gaza; Njia za mawasiliano ziwe za kuaminika na zisizokatizwa; Kuwe na uwezo mkubwa wa usafiri ndani ya Ukanda wa Gaza; Miundombinu ya kiraia, kama vile shule na hospitali, lazima ilindwe; Uwepo ufikiaji wa Ukanda wa kaskazini wa Gaza, ili kuturuhusu kufikia watoto na familia zilizo hatarini ambazo zinahitaji sana msaada wa kibinadamu. Hatimaye, watoto wawili wa Israeli waliotekwa nyara lazima waachiliwe bila masharti na kwa usalama. Vurugu hizi lazima zikome sasa.

13 January 2024, 13:18