Tafuta

2024.01.24: Tukio kubwa la mchezo  wa Kitesurf usio wa kibiashara tarehe 27 Januari 2024 huko Zanzibar 2024.01.24: Tukio kubwa la mchezo wa Kitesurf usio wa kibiashara tarehe 27 Januari 2024 huko Zanzibar 

Tanzania,Zanzibar:Shindano la Kitesurf 2024

Huko Zanzibar,Tanzania itawaona wachezaji 20 wa nchi 9 wa Kitesurf,Januari 27.Ni katika muktadha wa mshikamano kama asemavyo Papa kuwa:“kwa kucheza tu kama timu na kuwa pamoja inawezekana kufikia malengo ya kauli mbiu ya Olimpiki:juu zaidi,haraka zaidi na ngumu zaidi.Mchezo ni jenereta ya jamii hasa kwa vijana kwani huunda umoja,urafiki,kushirikiana na kuhusika."

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Mnamo Jumamosi tarehe 27 Januari 2024, litafanyika shindano la mchezo wa Kitesurf katika Fukwe za Kiwengwa huko Zanzibar, lililoandaliwa na Shirika lisilo la kibishara, Baraza la Michezo la Taifa Zanzibar(ZNSC)na Kamati ya Kiwengwa Kitesurf (KKC),ambayo inawakilishwa na shule mbili za zanzibar za kitesurf: Onelove Kite na Jambo Kite. Mashindano haya ya kimataifa yameidhinishwa na Serikali ya Zanzibar na Wizara ya Utalii, Jumuiya ya Hoteli Zanzibar, Ubalozi wa Tanzania nchini Italia na Ubalozi wa Italia nchini Tanzania. Shindano hili litawaona watu 20 kutoka mataifa mbali mbali 9 kwa lengo la kuwa pamoja na kusheherekea msimu wa kwanza wa mchezo huo wa Kitesurf 2024.

Bango la maelezo ya mchezo wa Kitesuf
Bango la maelezo ya mchezo wa Kitesuf

Kwa mujibu wa muandaaji mkuu Daktari Stefano Conte, na ambaye ni Daktari wa Watoto, kama mpenda mchezo huo, amefanya juhudi kubwa ya maadalizi kutokana na uzoefu wake ili kuunganisha watu wa mataifa mbali mbali kufanya uzoefu huo wa pamoja, kwa mara ya kwanza katika eneo hilo la Zanzibar. Hii ni kama kutaka kufafanua kile ambacho Baba Mtakatifu Francisko amekuwa akikazia kuhusu thamani ya mchezo kwa watu. Papa Francisko alisema kuwa: “Kukuza mchezo ambao ni kwa ajili ya kila mtu, mshikamano unaoweza kufikiwa na kulengwa kwa kila mwanamume  na mwanamke ni dhamira kubwa na changamoto ambayo hakuna mtu anayeweza kuifanya peke yake. Kiukweli, kwa kucheza tu kama timu na kuwa pamoja inawezekana kufikia malengo ya kauli mbiu ya Olimpiki: altius, citius, fortius, yaani: juu zaidi, haraka zaidi na ngumu zaidi. Baba Mtakatifu alisisitiza hayo wakati wa kutoa hotuba yake  kwa Washiriki wa Kongamo la Kimataifa la Michezo mnamo tarehe 30 Septemba 2022, lililokuwa limeandaliwa na Baraza la Walei, Familia na Maisha.

Shiriki mchezo wa Kitesurf
Shiriki mchezo wa Kitesurf

Baba Mtakatifu alikazia kusema kuwa "Mchezo ni jenereta ya jamii, hasa kwa vijana kwa sababu huunda ujamaa, huunda urafiki, huunda kushirikiana, ushiriki na hali ya kuhusika. Mchezo una mwelekeo wa elimu, mchezo, ambao hauwezi kutenganishwa na mwelekeo wa burudani na ukomavu hata katika viwango vya juu vya taaluma. Kama vile washiriki wanavyounda kundi, vivyo hivyo wachezaji huunda timu na watu huunda jumuiya. Kwa maana hiyo, michezo unaweza kuwa ishara ya umoja kwa jamii, uzoefu wa utangamano, kielelezo cha mshikamano na ujumbe wa maelewano na amani.”

Papa Francisko akiendelea alisitiza kuwa: “Leo  hii tuna hitaji kubwa la ufundishaji wa amani, kukuza utamaduni wa amani, kuanzia uhusiano wa kila siku kati ya watu na kumalizia na ule wa kati ya watu na mataifa. Ikiwa ulimwengu wa michezo utasambaza umoja na mshikamano unaweza kuwa mshirika mkubwa katika kujenga amani. Nje ya mantiki hii, tuna hatari ya kuanguka katika mashine ya biashara, ya faida, ya kuvutia ya watumiaji, ambayo hutoa wahusika ambao picha yao inaweza kutumiwa. Lakini huo sio mchezo tena. Mchezo ni jambo jema la kielimu na la kijamii na lazima ubaki hivyo!"

Mchezo usio wa kibiashara huko Zanzibara 27 Januari 2024
Mchezo usio wa kibiashara huko Zanzibara 27 Januari 2024

Baba Mtakatifu alisema kwa "Kwa sababu hiyo, kwanza kabisa, ufikiaji ni muhimu unaotuwezesha kuondoa vikwazo hivyo vya kimwili, kijamii na kiutamaduni vinavyozuia au kuzuia upatikanaji wa michezo. Kujitolea ni kwamba kila mtu ana nafasi ya kufanya mazoezi ya michezo, kama kulima ambapo mtu anaweza kusema kufundisha maadili ya mchezo na kuyabadilisha kuwa fadhila. Pamoja na upatikanaji pia kuna haja ya ukarimu, kwa mtu anayeweka mlango wa moyo wazi, na kwa hiyo, husaidia kuondokana na ubaguzi, hofu, wakati mwingine tu ujinga. Ni kwa njia hiyo tu tunaweza kukuza mchezo unaolenga kila mtu, ambapo kila mtu anaweza kukuza talanta zao, hata kuanzia hali ya udhaifu au ulemavu. Tukio hili lina harufu ya kujinyima raha, ya utafutaji wa kile kinachotukamilisha na kutufanya twende mbali zaidi. Kiini cha utafutaji huu kuna, hatimaye, mvutano kuelekea uzuri na utimilifu wa maisha ambao Mungu anaota kwa kila kiumbe chake.” Alisisitiza Papa Francisko kwa wanamichezo hao.

Ni katika muktadha huo wa michezo, ambapo Mchezo wa shindano la Kitesurf huko Zanzibar  tarehe 27 Januari 2024 unasisitizitwa kuwa sio wa kibiashara, kama alivyosema mwandaaji mkuu Dk. Stefano Conte: “Habari marafiki na ndugu waswahili. Mimi ni Daktari Stefano Conte, lakini mnaweza kuniita, Stefy. Ujumbe huu ni wa kukufahamisha kuwa Jumamosi ijayo saa tano kamili, Mechi ya I ya Kimaifa ya “Zanzibar Cup ya Kitesurfing” itafanyika Kiwengwa Zanzibar, Tanzania. Wengi wenu njooni ili kuona, au ninatumaini kwamba mnaweza kufuatilia kwenye Runinga. Hili litakuwa tukio kubwa lisilo la faida, yaani (lisilo la kibiashara). Na ninasaidia Baraza la Michezo, Zanzibar kuliandaa, na kutakuwa na washiriki 20 wa mataifa 9 tofauti. Tukutane Zanzibar."

Walioko Zanzibar wanaweza kwenda kuona, hata kufuatilia kwenye Runinga na walio mbali wanaweza kufuatilia kwenye Runga na majukwaa mbali mbali kama vileFacebook.

Wasiliana na waandaaji

Kombe la Zanzibar linadhaminiwa pia na Hoteli ya Amelia Zanzibar. Kwa maelezo zaidi kwa niaba ya ZNSC na KKC, wasiliana kwa Tanzania: WHATSAPP (+255) 762 478 528, na Kimataifa: EMAIL stefconte@yahoo.it

Shiriki Shindano la Kitesurf huko Zanzibar 27 Januari 2024
25 January 2024, 12:25