Ukraine,mabomu ya Urussi huko Kharkiv.Zelensky:Msituache peke yetu
Vatican News.
Makombora mawili ya Urussi yaligonga hoteli moja huko Kharkiv, kaskazini-mashariki mwa Ukraine na kuwajeruhi watu kumi na moja, wakiwemo waandishi watatu wa habari wa Uturuki. Mamlaka ya manispaa ya jiji ilitangaza. Mmoja wa waliojeruhiwa alisemekana kuwa katika hali mbaya sana. Jeshi la Urussi pia lilishambulia kampuni moja ya uchimbaji madini ya makaa ya mawe katika mji wa Mirnograd, eneo la mashariki la Donetsk, na kumuua mtu mmoja. Kwa sasa inaonekana wazi kwamba mzozo huo unakabiliwa na hatua ya mabadiliko, kwenye kizingiti cha mwanzo wa mwaka wa tatu wa vita na huku Urussi ikifanya mashambulizi ya patchy katika eneo lote la Ukraine.
Msaada kwa Ukraine
Ukraine, kupitia sauti ya Rais Volodymyr Zelensky, ilionesha kwamba kusita kwa nchi za Magharibi juu ya kutoa misaada kwa nchi yao kunamtia moyo Rais wa Urussi Vladimir Putin, ambaye lengo lake halisi ni kuikalia kwa mabavu Ukraine nzima. Kwa hakika, nchini Marekani na nchi kadhaa za Ulaya, mjadala unaendelea kuhusu fursa ya kuendelea kusambaza silaha kwa nchi iliyoshambuliwa.
Kuanzisha tena mazungumzo ya kidiplomasia
Kulingana na waangalizi wengi, kinachokosekana katika awamu hii ya mzozo wa Urussi na Ukraine ni shinikizo la kimataifa la kutoa nafasi kwa mazungumzo katika mgogoro huo. Kuhusiana na hilo, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Boris Johnson, katika mahojiano na gazeti la Times, alikanusha tuhuma za Urussi kulingana na ambayo yeye ndiye aliyezuia mazungumzo ya amani kati ya Urussi na Ukraine katika msimu wa kiangazi cha 2022.