Zanzibar:Shiriki shindano la Kwanza la Kimataifa la Kitesurf,27Januari 2024
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baraza la Michezo la Taifa Zanzibar (ZNSC) na Kamati ya Kiwengwa Kitesurf(KKC) inayowakilishwa na shule mbili za zanzibar za kitesurf za Onelove Kite na Jambo Kite wanatoa mwaliko wa kushiriki mashindano nchini Zanzibar kwamba: “Mwaka huu 2024, chini ya Mti wa Noeli, tunawaalika ninyi nyote kushiriki katika mashindano ya kwanza ya kitesurfing kwenye kisiwa cha ajabu cha Zanzibar (Tanzania) moja kwa moja katika kipindi bora cha upepo mwanana wa kitropiki! Jiunge nasi kwa mbio hizi nzuri za kusherehekea kuanza kwa msimu wa kitesurf 2024, visiwani Zanzibar na kuona ni nani mkimbiaji mwenye kasi zaidi katika Bahari ya Hindi!”
Wadhamini wa shindano hilo
Kwa njia hiyo ni tukio lililoandaliwa na Shirika lisilo la kibishara, Baraza la Michezo la Taifa Zanzibar(ZNSC) na Kamati ya Kiwengwa Kitesurf (KKC), ambayo inawakilishwa na shule mbili za zanzibar za kitesurf za: Onelove Kite na Jambo Kite. Mashindano haya ya kimataifa yameidhinishwa na Serikali ya Zanzibar na Wizara ya Utalii, Jumuiya ya Hoteli Zanzibar, Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Ubalozi wa Italia nchini Tanzania.
Tarehe 27 Januari 2024 katika mwambao wa Kiwengwa
Tukio hilo litafanyika Jumamosi tarehe 27 Januari 2024 tu, ambalo litaanza kwa taarifa saa 5.00 kamili asubuhi na kuendelea na mbio saa 9.00 alasiri ndani ya mwambao wa Kiwengwa na kumalizia kwa utoaji wa tuzo saa 11.00 kamili jioni katika ngazi ya Hoteli ya Melia, huko huko Zanzibar.
Dk. Conte anawaalika washiriki na watazamaji kupitia runinga
Katika maelezo kuhusu shindano hilo Daktari Stefano Conte anawaalika wote kwa kusema kuwa: “Habari marafiki na ndugu waswahili. Mimi ni Daktari Stefano Conte, lakini mnaweza kuniita, Stefy. Ujumbe huu ni wa kukufahamisha kuwa Jumamosi ijayo saa tano kamili, Mechi ya I ya Kimaifa ya “Zanzibar Cup ya Kitesurfing” itafanyika Kiwengwa Zanzibar, Tanzania. Wengi wenu njooni ili kuona, au ninatumaini kwamba mnaweza kufuatilia kwenye Runinga. Hili litakuwa tukio kubwa lisilo la faida, yaani (lisilo la kibiashara). Na ninasaidia Baraza la Michezo,Zanzibar kuliandaa, na kutakuwa na washiriki 20 wa mataifa 9 tofauti. Tukutane Zanzibar.”
Wasiliana na waandaaji
Kombe la Zanzibar linadhaminiwa pia na Hoteli ya Amelia Zanzibar. Kwa maelezo zaidi kwa niaba ya ZNSC na KKC, wasiliana kwa Tanzania: WHATSAPP (+255) 762 478 528, na Kimataifa: EMAIL stefconte@yahoo.it