Tafuta

Wawakilishi wa Kitaifa wa Jumuiya za Kiorthodoksi,Kikatoliki na Kiprotestanti,kwa kushirikiana na Mtandao wa Amani na Upatanisho wa Muungano wa Kiinjili wa Ulimwenguni, Ushirika wa Kiinjili wa Canada  wabaomba kuimbea Ukraine Wawakilishi wa Kitaifa wa Jumuiya za Kiorthodoksi,Kikatoliki na Kiprotestanti,kwa kushirikiana na Mtandao wa Amani na Upatanisho wa Muungano wa Kiinjili wa Ulimwenguni, Ushirika wa Kiinjili wa Canada wabaomba kuimbea Ukraine  

Februari 24 ni mwaka wa 2 wa vita Ukraine na wito wa amani kutoka viongozi wa Canada!

Jumatano tarehe 21 Februari 2024,Makanisa na viongozi wa Kikristo nchini Canada wametoa wito wa amani wakati vita nchini Ukraine vikiingia mwaka wa tatu,vilivyoanza 24 februari 2024

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tarehe 24 Februari 2024 ni kumbukumbu ya mwaka wa pili tangu  uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ambapo Wawakilishi wa Kitaifa wa Jumuiya za Kiorthodoksi, Kikatoliki na Kiprotestanti, kwa kushirikiana na Mtandao wa Amani na Upatanisho wa Muungano wa Kiinjili wa Ulimwenguni, Ushirika wa Kiinjili wa Canada na Baraza la Makanisa la Canada, walitia saini  katika Waraka wa Kichungaji kuhusu ‘Ukraine, Canada na Kanisa’ ili kuwaalika kila mtu kujumuika katika maombi kwa ajili ya amani. Kwa mujibu wa wito wao wanabainisha kuwa: “Bila kwa njia yoyote kupunguza mateso na huzuni zinazosababishwa na vita na vurugu katika sehemu nyingine za dunia, tunasimama pamoja kuwaalika Wakristo na watu wote wenye mapenzi mema kutafakari kwa sala jinsi sisi sote tumeitwa, na tunaweza kuchangia, ili kufikia mafanikio ya amani ndani na kwa Ukraine.”

Viongozi wa kidini 45 wametia saini waraka wa kuomba amani nchini Ukraine

Barua ya kichungaji imeidhinishwa na wakuu viongozi 45, ambapo barua hiyo inabainisha njia sita muhimu za kuimarisha amani:Sala, Kusaidia wakimbizi wa Kiukreni, Kuhimiza mipango ya kidiplomasia kwa ajili ya amani ya haki na ya kudumu nchini Ukraine, Kutafuta uhusiano wa ushirikiano wa usaidizi wa kibinadamu, Kukumbuka tarehe 24  Februari siku hiyo na hatimaye  Matumaini ya upatanisho. Na  Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Canada, Askofu William T. McGrattan, Askofu wa Jimbo Katoliki la Calgary, akiungwa mkono na Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Maaskofu(CCCB),ni mmoja wa watia saini waliotajwa katika Waraka huo, ambao sasa unapatikana katika lugha ya Kifaransa, Kiingereza na Kiukraine. Kwa njia hiyo katika waraka huo wanatoa mwaliko wa kushiriki viungo hivyo ili kuomba na kufanya kazi pamoja kwa ajili ya amani.

Viongozi wa kidini 45 wa Canada wanaomba amani kwa ajili ya Ukraine
22 February 2024, 13:55