Tafuta

Mpango Mkakati wa Mattei wa Maendeleo kwa Bara la Afrika “Piano Mattei” unajikita katika mambo makuu matano. Mpango Mkakati wa Mattei wa Maendeleo kwa Bara la Afrika “Piano Mattei” unajikita katika mambo makuu matano.  (ANSA)

Mpango Mkakati wa Mattei wa Maendeleo Barani Afrika: Utekelezaji: Vitendo

Ni mpango unogusia pia: Usalama na matumizi ya nishati mbadala, maendeleo ya miundombinu, usalama wa chakula, elimu na mafunzo ya ufundi pamoja na kupambana na wahamiaji haramu. Serikali ya Italia inatarajia kushiriki kwa kiasi kikubwa kukuza maendeleo Barani Afrika kwa kupitia Mpango Mkakati wa Mattei, unaokazia: Kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na Bara la Afrika, kuunda njia mpya za usambazaji wa nishati, kudhibiti wimbi kubwa la wakimbikizi!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Mpango Mkakati wa Mattei wa Maendeleo kwa Bara la Afrika “Piano Mattei” unajikita katika mambo makuu matano: Elimu, Majiundo, Afya, Kilimo, Maji na Nishati, utakaogharimu kiasi cha Euro bilioni 5.5, sawa na shilingi bilioni 969. Ni mpango unogusia pia: Usalama wa nishati na matumizi ya nishati mbadala, maendeleo ya miundombinu, usalama wa chakula, elimu na mafunzo ya ufundi pamoja na kupambana na wahamiaji haramu. Serikali ya Italia inatarajia kushiriki kwa kiasi kikubwa kukuza maendeleo Barani Afrika kwa kupitia Mpango Mkakati wa Mattei. Mpango huu pamoja na mambo mengine unakazia: Kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na Bara la Afrika, kuunda njia mpya za usambazaji wa nishati, kudhibiti wimbi kubwa la wakimbikizi na wahamiaji.

Mkutano wa Nne kati ya Italia na Bara la Afrika, 2024
Mkutano wa Nne kati ya Italia na Bara la Afrika, 2024

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat ameiomba Serikali ya Italia, ili Afrika ipewe muda wa kuchanganua Mpango Mkakati wa Mattei wa Maendeleo kwa Bara la Afrika “Piano Mattei” kabla ya kuanza utekelezaji wake. Huu ni wakati wa kubadilisha maneno kwenda kwenye vitendo; kwa kuona njia gani zinaweza kutumika kutekeleza mpango huu. Vinginevyo, Mpango Mkakati wa Mattei wa Maendeleo kwa Bara la Afrika “Piano Mattei” utabakia kuwajengea Waafrika matumaini, lakini bila ya kutekelezwa.

Mpango Mkakati wa Mattei: Utekelezaji kwa vitendo
Mpango Mkakati wa Mattei: Utekelezaji kwa vitendo

Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, EU, imekazia umuhimu wa Bara la Afrika kujizatiti zaidi katika mapambano dhidi ya athari za mabadiliko la tabianchi; kudhibiti maafa makubwa yanayotokana na uhamiaji haramu; Bara la Afrika linapaswa kujielekeza zaidi katika kulinda na kudumisha haki, amani, usalama, ustawi na maendeleo endelevu. Viongozi wakuu wa baadhi ya nchi za Afrika, mawaziri, maafisa waandamizi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa, wawakilishi kutoka taasisi na mashirika ya Kimataifa, wafanyabiashara pamoja na mashirika ya kifedha wameshiriki mkutano huo wa nne wa ushirikiano kati ya Bara la Afrika na Serikali ya Italia.

Mkakati wa Mattei

 

03 February 2024, 13:57