Chiara Amirante, Mwanzilishi wa Chama cha Nuovi Orrizonti. Chiara Amirante, Mwanzilishi wa Chama cha Nuovi Orrizonti. 

Rais wa Chama cha Nuovi Orizzonti,Chiara Amirante amejiuzulu uongozi

Rais wa chama kinachotambuliwa na Vatican na kushiriki katika maeneo mbalimbali ya huduma kupitia vituo,jumuiya za mapokezi na mipango ya kijamii,ametoa taarifa ya kujiuzulu kwake kwa Papa,kutokana na afya ambayo haimwezeshi tena kuendelea na majuku magumu ya kuzidi uwezo wake.Shughuli hizo zinahitaji mtu ambaye aweze kusimamia kazi hizi kubwa na ngumu.

Vatican News

Chiara Amirante amechagua kushiriki uamuzi wake, kuchukuliwa kwa maumivu makubwa, kuacha urais wa Jumuiya ya Nuovi Orizzonti – Jumuiya ambayo  inahusika katika vitendo vya mshikamano katika maeneo yote ya shida za kijamii, kwa makini hasa kwa matatizo ya watoto wa mitaani na ulimwengu wa vijana, ambapo hayo yameonekana katika  ujumbe uliochapishwa  tarehe 20 Februari 2024, kwenye tovuti ya ukweli aliyoanzisha, mwenyewe huku akiomba maombi kwa ajili yake na familia ya Chama hicho.

Baada ya ushauri kuhusu afya ametoa uamuzi

“Baada ya kusikia maoni niliyopewa na madaktari wanaonifuatilia ilibidi nikiri kwamba hali yangu ya kiafya haiendani tena na ahadi zinazozidi kuwa ngumu na nyingi zinazohusiana na jukumu la urais, katika uongozi huu mkubwa na tata.” Chiara alikuwa amethibitishwa tena kuwa mkuu wa  Jumuiya hii ya Nuovi Orizzonti, shirika linalotambuliwa na Vatican mnamo tarehe 6 Januari 2024 na uchaguzi wa nyadhifa mpya kwa miaka mitano ijayo, lakini baada ya “kudorora zaidi kwa afya na kuzorota kwa dalili nyingi za kutisha” alieleza kwamba ilimbidi “kufungua upya utambuzi juu ya utangamano wa hali yake ya afya na ahadi nyingi zinazohusiana na jukumu la urais.

Amekabidhi barua ya kujiuzulu kwa Papa Francisko

“Katika picha ya jumla inayooneshwa na hali halisi nyingi na dalili nne katika hatua ya juu sana ambayo hufanya usimamizi wa matibabu kuwa ngumu sana wataalam kadhaa wa matibabu walionesha wasiwasi wao mkubwa kwa afya ya Amirante, kwa hiyo alithibitisha kudhoofika kwa afya yake  na viwango vya juu sana vya dhiki kutokana na mtindo wake wa maisha. Katika “miaka hii thelathini ya  Chama cha Nuova Orizonte, kwa sababu ya ukuaji wa haraka wa Jumuiya na matokeo yake kuongezeka kwa majukumu mazito, maamuzi muhimu na misalaba mizito iliyounganishwa na uongozi wa Familia hii kuu, ilinibidi kuendelea kudumisha kasi isiyowezekana” aliongeza kuandika  Chiara, huku  akibainisha kuwa haya yote yamemdhoofisha zaidi, lakini kwamba katika wakati huu wa dhiki kuu na dhaifu sana kwa ulimwengu wote hangetaka kuacha jukumu lake. Hata hivyo, kuporomoka zaidi kwa afya yake kulimsukuma kuwasilisha rasmi kujiuzulu kwake kwa kupeleka barua  kwa Papa Francisko na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha tarehe 11 Februari 2024.

Uongozi wa Chama hicho kwa muda wa kazi

Uongozi wa kazi hiyo “sasa utakabidhiwa kwa nafasi mpya zilizochaguliwa mwezi Januari, iliyopita huku tukisubiri kuelewana, na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, jinsi ya kuendelea, kwa sababu kwa mujibu wa Sheria Kuu zinazotumika, kwa kujiuzulu kwa rais”, alisema Chiara na uchaguzi mpya wa viongozi unahitajika. “Siku zote nipo, lakini kwa njia tofauti - alihitimisha Amirante. Kwa upande mwingine, alisema “hatuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya chochote, kwa sababu Kazi hii inatoka kwa Mungu na itaendelea kuiongoza katika maji yenye dhoruba ya wakati huu.” Alisisitiza

 

22 February 2024, 15:42