Tafuta

2024.02.15 Tanzania: Zanzibar CUP2024- Washidni wa mchezowa Kitesurf  huko Kiwengwa - Zanzibar. 2024.02.15 Tanzania: Zanzibar CUP2024- Washidni wa mchezowa Kitesurf huko Kiwengwa - Zanzibar. 

Tanzania,Zanzibar Cup 2024:mshindi ni Lukman Mohammed miaka 15

Mara baada ya mashindano ya mchezo wa Kitesurf huko Zanzibar 10 Februari 2024,Radio Vatican,Vatican News ilimfikia muhusika wa maandalizi,Dk Stefano Conte ambaye ametoa ushuhuda kuhusu siku hiyo:“Mashindano yalikuwa ya kiwango cha juu zaidi cha kiufundi na yalipangwa kama chombo chenye nguvu cha Amani na Udugu kati ya watu wote.”

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Tarehe 10 Februari 2024, yalifanyika mashindano ya mchezo wa Kitesurf huko Zanzibar CUP 2024 ambayo yaliwaona wachezaji 20 kutoka mataifa mbali mbali na hatimaye washindi wa mchezo huo kutoka Tanzania kwa kijana mwenye umri wa miaka 15. Mara baada ya mchezo huo Radio Vatican, -Vatican News ilimfikia muhusika mkuu wa maandalizi hayo, Dk. Stefano Conte ambaye ametoa ushuhuda kwa yote yaliyotokea katika siku ya mashindano. Tunachapisha ushuhuda wa Dk. Conte akizungumza na Radio Vatican.

Wapendwa Marafiki, siku chache zilizopita, Jumamosi tarehe 10 Februari 2024, yalifanyika mashindano ya ZANZIBAR CUP 2024, mashindano ya kwanza ya kimataifa ya mchezo wa kitesurfing kuwahi kufanyika huko Zanzibar, na ambayo yalifanyika kwa mafanikio katika maji ya Kiwengwa (Zanzibar - Tanzania). Washiriki 20, wenye umri kati ya kumi na tano na sabini na saba, walikuwa ni kutoka nchi tano tofauti na pia walijumuisha mwanamke mmoja. Mataifa yaliyowakilishwa katika MAJIRA haya ya “ZANZIBAR CUP 2024 WINTER” yalikuwa ni Tanzania, Italia, Ufaransa, Czech na Lithuania. Tunatumaini kuwa na mengi zaidi kwenye kikao cha majira ya joto. Mashindano yetu yalikuwa ya kiwango cha juu zaidi cha kiufundi na yalipangwa kama chombo chenye nguvu cha Amani na Udugu kati ya watu wote.

Ushindi wa Kitesurf Zanzibar
Ushindi wa Kitesurf Zanzibar

Washindi wa Zanzibar Cup 2024

Kwa upande wa mshindi alikuwa ni kijana Lukman Mohammed mwenye umri wa miaka 15 kutoka Zanzibar, ambaye ndiye amekuwa mkimbiaji mwenye kasi zaidi katika Bahari ya Hindi na kujinyakulia dola  za kimarekani 500, akifuatiwa na bingwa wa mtindo huru (freestyle) Seif Shabani Ngingo na Suleiman Abdalla Hassan.

Wakiwa katika mbio
Wakiwa katika mbio

Mbio za kitesurfing zilianza saa kumi na nusu jioni, na kuvuka  pwani ya Kiwengwa karibu na ‘Olympic Triangle’ kati ya vijiji vya Kairo na Kumba Orembo na kumalizia mbele ya shule ya ‘Jambokite kitesurfing’ saa 11:15 jioni. Mashindano yetu ya kimataifa ya kitesurfing yalifana sana na hafla ya utoaji tuzo ilifanyika mara baada ya mashindano hayo katika hoteli ya Melia Zanzibar.

Wakiwa katika mashindano
Wakiwa katika mashindano

Dk. Stefano Conte, anatoa shukrani

“Ninapenda kuwashukuru wale wote waliofanikisha michuano ya ZANZIBAR CUP 2024 na waliochangia kuiandaa. Awali ya yote, ninafuraha kuwashukuru waandaaji rasmi, Bwana Said Marine, Katibu Mtendaji, kwa niaba ya Baraza la Michezo Zanzibar, na Abdul Haji Hassan, kiongozi wa skuli ya Jambokite, kwa niaba ya Kamati ya Kiwengwa Kitesurfing. Kisha, ninamshukuru Bwana Nicolas Koenig, meneja mkuu, kwa niaba ya Hoteli ya Melia Zanzibar ambao walifadhili hafla yetu. Kisha ninapenda kumshukuru Rais Hussein Mwinyi kwa niaba ya Serikali ya Zanzibar, Mkurugenzi wa Masoko Rahma Sanya kwa niaba ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Mabalozi Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo, kwa niaba ya Ubalozi wa Tanzania nchini Italia na Mheshimiwa Marco Lombardi, Ubalozi wa Italia nchini Tanzania, na Mheshimiwa Wilfred Shirima kwa niaba ya Chama cha Hoteli Zanzibar waliopitisha Kombe la Zanzibar 2024.

Baadhi ya washiriki wa Shindano la Kitesurf huko Kiwengwa Zanzibar - Tanzania
Baadhi ya washiriki wa Shindano la Kitesurf huko Kiwengwa Zanzibar - Tanzania

Dk. Conte akiendela na shukrani anaendelea kusema kuwa  "Aidha, nina furaha kuwashukuru wasaidizi wetu wote: Mheshimiwa Josef Stary, Mheshimiwa Federico Re, Mheshimiwa Buruhani, Issa Abdalla, Bwana Aldo Trazza, Bwana Hassan Ali Hassan, Bwana Hamad Abdullah Khamis, Bwana Zidini Tano, Bwana Amour Suleiman, Bwana Zafania Mahonda, Bwana Ali Khams,  Bwana Abdallah Karega, Bwana Ussy Amir Omar na Bwana Yusel Rodriguez.  Hataimaye namshukuru Rais Samia Suluhu Hassan aliyetukaribisha katika nchi yake nzuri ya Tanzania. Tukutane hivi karibuni  kwenye ZANZIBAR CUP ijayo. Ninawakumbatia kwa mkubatio mkubwa kwenu nyote kutoka kwa Stefano Conte.

Dk Conte akimkumbatia mshindi wa kwanza wa mchezo huo kwa mara ya kwanza kufanyika Zanzibar
Dk Conte akimkumbatia mshindi wa kwanza wa mchezo huo kwa mara ya kwanza kufanyika Zanzibar

Matumaini ya mchezo ujao

Dk. Conte kwa shukrani hiyo akizungumza na Vatican News,  huku akiwa na furaha kubwa ya matokeo hayo ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika mchezo  kama huo, katika Bahari ya Hidni huko Zanzibar -Tanzania na anayo matarajio makubwa ya ushiriki wa wengi kwa kipindi kijacho. Ikumbukwe mchezo huo uliandaliwa na Shirika lilisilo la Kiserikali kwa hiyo lisilo la kibiashara kwa kuwashirikishisha wote hayo mliowasoma kushiriki katika kufanikisha mchezo huo.

Dk Conte akionesha zawadi ya mshindi wa kwanza wa mchezo huo wa Kitesurf huko Zanzibar
Dk Conte akionesha zawadi ya mshindi wa kwanza wa mchezo huo wa Kitesurf huko Zanzibar
Wakati wa mashindano
Wakati wa mashindano
15 February 2024, 16:38