Ufaransa kuelekea Katiba inayopinga maisha
Massimiliano Menichetti
Ni miezi mitano tu iliyopita ambayo Baba Mtakatifu akiwatazama machoni zaidi ya waamini 50,000 katika Uwanja wa Vélodrome wa Marsiglia, aliwaeleza : “Njia mpya ya imani, upendo na matumaini” na ilikuwa ni hatua ya mwisho wa ziara yake ya kitume ya 44 ya kimataifa, huku akihutubia hivyo Kanisa, Ufaransa na Ulaya nzima, na akihimiza maisha, na kukubalika kwa udugu. Katika tukio hilo hasa alitumia maneno mawili yenye nguvu: “ujinga na kujiuzulu,” mapigo mawili ambayo mara nyingi yaliumiza ukweli wetu, na yalisababisha kila mtu kutazama mbinguni, huku akimtumaini Bwana ambaye “hutenda katika historia, akifanya maajabu na yuko huko pia akitenda kazi katika jumuiya zetu zilizo na alama za kidunia na kutojali kwa kidini.”
Baba Mtakatifu katika kutazama janga la upotevu wa maisha ya mwanadamu ambayo huchukua sura tofauti, alisisitiza kuanzia kwa wahamiaji waliokataliwa, hadi kwa watoto ambao hawajazaliwa, au wazee waliotelekezwa, huku akiomba kutogeuza kisogo, kupenda, kumtambua mwingine, iwe ndani ya mtumbwi katikati ya bahari, au katika hali isiyo na ulinzi zaidi tumboni mwa mama. Ujumbe mzito wa matumaini, mwanga na kujitolea ulisisitizwa huko na Papa Francisko nchini Ufaransa.
Hata hivyo mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu Mkutano wa Kitaifa huko Paris uliidhinisha kujumuishwa kwa haki ya kutoa mimba katika Katiba. Hatua ya mageuzi iliyoletwa mbele na serikali sasa inachunguzwa na Seneti. Katika Ulaya iliyojeruhiwa na vita, iliyodhoofishwa na watawala, watu wengi, shinikizo la watumiaji, na mikakati ya kiuchumi ambayo inajaribu kuweka mbali maono ya waanzilishi kama vile: Alcide De Gasperi, Robert Schuman, Konrad Adenauer ya msukumo huo wa ukweli, uliokumbukwa na Mrithi ni uamuzi wa Petro, ambaye anamulika uso wa mwanadamu.
“Kutoa mimba ni mauaji,” Papa Francisko aliwaambia waandishi wa habari waziwazi kwenye ndege ya kurudi kutoka Slovakia mnamo Septemba miaka mitatu iliyopita. Kwa hivyo inawezekanaje kuchanganya katika hati ya kimsingi ya serikali haki inayomlinda mtu na yule anayeidhinisha kifo chake? Tunaishi katika jamii iliyoendelea kiteknolojia, iliyotumia kompyuta na iliyounganishwa. Ukuaji wa mwanadamu tangu kutungwa mimba haukuwa na siri tena kwa miongo kadhaa.
Tunatumia maneno kama vile kabla ya kiinitete, umbu, mtoto mchanga, mtoto, kijana, mtu mzima, wazee kuonesha hatua za ukuaji ambao idadi ya seli hubadilika, ambayo kipengele cha utambuzi hubadilika, hitaji la usaidizi, lakini kila wakati ni mtu. “Je, ni sawa kuua maisha ya binadamu ili kutatua tatizo? Je, ni sawa kuajiri mshambuliaji ili kuchukua maisha ya binadamu?” aliuliza Papa, akihutubia waandishi wa habari tena kwenye ndege ya kurudi kutoka Bratislava hadi Roma.
Jamii haipimwi kwa makatazo yake, bali kwa uwezo wake wa kupenda na “uhuru hukua kwa upendo,” Papa Francisko alieleza katika katekesi ya tarehe 20 Oktoba 2021, lakini “kwa upendo tunaouona katika Kristo, mapendo; hakika huu ni upendo wa bure na ukombozi.” Mwanzoni mwa mchakato wa Bunge, Maaskofu wa Ufaransa walionesha wasiwasi wao juu ya marekebisho haya ya Katiba, na kusisitiza tena kwamba kila maisha ni zawadi, zawadi dhaifu na ya thamani, inayostahili kukaribishwa na kuhudumiwa tangu mwanzo hadi mwisho wake, muda wa asili. Ubinadamu daima umelaani kila nadharia ya eugenic, lakini viinitete vinaendelea kudanganywa na kuchaguliwa kana kwamba ni nyenzo na sio watu. Utoaji mimba katika muktadha huu ni msingi na matokeo. Ajabu ni kana kwamba hatuwezi tena kuona, kuwa huru, kuchangia na kusaidia.
Katika dunia iliyojeruhiwa na vurugu nyingi inaonekana vigumu kujenga uzuri, mkakati wa kimataifa wa kukaribisha na msaada, kuweza kutenga fedha, tahadhari, upendo kwa wanawake wanaopata ujauzito mgumu, kwa watoto waliobebwa tumboni. Hata hivyo, maisha mengi yangeokolewa, kama inavyooneshwa na shughuli za vituo vya kusaidia maisha, ikiwa wanawake wangeungwa mkono katika nyanja za kiuchumi, kisheria, kisaikolojia, kidini na kijamii, katika wakati mgumu ambao utoaji mimba unaonekana kuwa suluhisho pekee. Mara nyingi tunajifungia katika mizozo ya kisiasa au ya kiitikadi isiyo na matunda, lakini changamoto ni kupitisha sheria na kurekebisha katiba na mapendekezo ya maisha, sio kifo. Uwekezaji na hatua za kuimarisha miundo na hali halisi inayoweza kuchukua mateso, hofu, hali mbaya na kali. Msaada huo ni upendo, ni kuwa huru kuchagua. Na upeo huu wa kidugu, unaomjali mwingine, wa mtu, hujenga jamii zisizokata tamaa, bali zielekee kwenye utamaduni halisi wa kukaribishwa, kushirikiana na amani.