Tafuta

Muonekano wa Bunge la Ulaya. Muonekano wa Bunge la Ulaya. 

UIP:Kwa 2023 idadi ya wanawake wabunge duniani imeongezeka kidogo!

Tarehe 8 Machi 2024 ni siku ya Wanawake duniani ambapo mwaka 2024 inaongozwa na kauli mbiu:“Wekeza kwa wanawake.Harakisha maendeleo.”Kulingana na ripoti ya hivi karibuni zaidi ya Muungano wa mabunge duniani(UIP)kuhusu idadi ya wanawake bungeni kwa 2023,imeongezeka hadi asilimia 26.9, duniani kote kutokana na uchaguzi na uteuzi uliofanyika mwaka 2023.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Majukumu tofauti ya wanaume na wanawake katika familia, kazini na katika jamii huamua mahitaji tofauti ambayo mwitikio sawa lazima utolewe kupitia sio tu marudio ya matumizi ya umma, lakini pia zana zinazotolewa na sekta binafsi. Ustawi wa kampuni kiukweli unaweza kuwa chombo halisi cha usawa, pia katika kuongeza uwepo wa wanawake katika ulimwengu wa kazi, na sehemu mbambali za majukumu ya ngazi za juu. Hata hivyo katika ulimwengu wa kazi bado kuna safari ndefu na bado kuna tofauti kubwa kati ya asilimia ya ajira za wanaume na wanawake.

Inaonekana haiwezekani kufikiri kwamba kufikia hata mwaka 2024 wanawake bado wanakuwa waathirika wa pengo la mshahara: kwa kazi iliyo sawa, wafanyakazi wa kike wanapata mshara mdogo chini ya wanaume. Lakini si hivyo tu: upatikanaji wa kazi ulimwenguni  kwa wanawake unaelekezwa zaidi kwenye nafasi za chini ya  kifahari na za kulipwa kuliko wanaume. Zaidi ya hayo, ni mwanamke mmoja tu kati ya wanne anayeweza kushikilia nafasi ya usimamizi. Sababu zinaweza kuhusishwa na dhana potofu za kijinsia, ambazo bado zinahusu elimu. Mara nyingi tunasikia maneno kama haya: Wanawake wanafaa zaidi kwa masomo ya kibinadamu(Humanistic, kwa sababu ya unyeti wao, na chini ya yale ya kisayansi.

Bi Tulia Ackson ni Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa UIP tangu 2023
Bi Tulia Ackson ni Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa UIP tangu 2023

Mfano mwingine wa chuki ni juu ya jukumu la wanawake ndani ya makao ya nyumbani. Takwimu zinaonesha kuwa katika familia ambazo wazazi wote wawili wanafanya kazi, ni mwanamke  tu ambaye hutumia wakati wake mwingi kutunza nyumba na watoto, wakati baba kwa ujumla hayupo ndaniya familia.  Hata matukio ya ukatili, kimwili, kisaikolojia na maneno bado yameenea. Takriban 32% ya wanawake wanadai kuwa waathiriwa, ikizingatiwa kuwa vipindi vingi vya unyanyasaji wa nyumbani  haviripotiwi!

Tunahitaji msaada wa pande mbili kwa usawa, hasa katika maeneo ya kazi, familia na unyanyasaji wa kijinsia: kwa upande mmoja, marekebisho ya kimuundo na kanuni ni muhimu; kwa upande mwingine ni muhimu kukuza mabadiliko ya mawazo. Dhana ya usawa lazima itolewe katika maeneo ya elimu kutoka utoto wa mapema, kusambaza utajiri unaotokana na utofauti wa kila mtu, ambao lazima uheshimiwe na kuthaminiwa. Ili kuwaruhusu wanawake kukuza taaluma zao kama vile wanaume, tunahitaji huduma zaidi zinazotolewa kwa watoto na familia kwa bei nafuu, pamoja na mchango mkubwa kutoka kwa akina baba, ambao wanapaswa kuchukua fursa ya likizo ya uzazi sawa na ile ya mama. Kuhusu vurugu, wanapaswa kulaaniwa kwa vyovyote vile kwa adhabu kali zaidi wote wanaofanya vitendo hivyo kinyume na haki ya mwanamke.

Bunge la Ufaransa
Bunge la Ufaransa

Ndugu msomaji, katika muktadha wa siku ya wanawake na hata katika nafasi, tunaona tafiti nyingine zilizofanywa kwa mfano  Muungano wa Wabunge duniani (UIP) unasema wanawake wameongozeka katika bungu kwa mwaka 2023 ambapo wanawakilisha ongezeko la asilimia 0.4 mwaka baada ya mwaka, kiwango sawa cha ukuaji kwa mwaka 2022. Hata hivyo, ukuaji huo ni wa polepole kuliko miaka iliyopita kwani chaguzi za 2021 na 2020 zilishuhudia ongezeko la asilimia 0.6 ya wabunge. Ripoti ya UIP  inasema masuala ya kijinsia yalitawala chaguzi nyingi huku kukiwa na upinzani dhidi ya haki za wanawake katika baadhi ya nchi.  Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa wanawake kadhaa mashuhuri wameacha siasa hivi karibuni, wakilaumu uchovu na vitisho. Ripoti hiyo ya IPU inatokana na marekebisho yaliyofanywa na bunge katika mabunge 66 kwenye nchi 52 mwaka 2023. Wanawake walikuwa asilimia 27.6 ya wabunge katika mabunge hayo mapya yaliyochaguliwa au kuteuliwa, ikiwa ni ongezeko la jumla la asilimia 1.4 ikilinganishwa na kura za awali katika nchi hizo hizo.

Nyanja zilizopiga hatua

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya UIP kulikuwa na maendeleo makubwa katika baadhi ya maeneo, kwa mfano: Katika bara la Amerika, wanawake walichangia asilimia 42.5 ya wabunge wote waliochaguliwa au kuteuliwa katika mabunge ambayo yalichaguliwa upya mwaka wa 2023, asilimia kubwa zaidi ya kikanda. Kwa hivyo kanda hiyo inashikilia nafasi yake ya muda mrefu kama eneo lenye uwakilishi wa juu zaidi wa wanawake duniani, kwa asilimia 35.1. Ulimwenguni kote, sehemu ya Maspika wanawake wa mabunge iliongezeka hadi asilimia 23.8 ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.1. Cambodia na Ivory Cost zilichagua Maspika wanawake kwa mara ya kwanza. Viwango vilivyoundwa vyema na kutekelezwa vinaendelea kuwa jambo muhimu katika kuongeza uwakilishi wa wanawake. Mabunge 43 ambayo yalikuwa na aina fulani ya viti maalum yalichagua wabunge wanawake asilimia 28.8 kwa wastani, dhidi ya asilimia 23.2 katika nchi ambazo hazina.

Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara

Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa mujibu wa Muungano Mabunge duninai(UIP) unasema ulirekodi uboreshaji wa juu zaidi kati ya kanda zote na ongezeko la asilimia 3.9 katika chaguzi za mwaka 2023 ikilinganishwa na kura za awali katika nchi hizo hizo. Mafanikio makubwa zaidi yalikuwa nchini Benin, Eswatini na Sierra Leone, yakiwezeshwa na nafasi za upendeleo. Rwanda inaendelea kuongoza katika orodha ya kimataifa ya IPU huku wanawake wakichukua asilimia 61.3 ya viti katika Baraza la Manaibu, ikifuatiwa na Cuba na Nicaragua zenye asilimia 55.7 na 53.9 mtawalia, huku Andorra, Mexico na Umoja wa Falme za Kiarabu zikiwa na usawa.

Masuala ya jinsia yanatawala katika baadhi ya chaguzi

Ripoti ya IPU inabainisha kuwa masuala ya kijinsia mara kwa mara yaliibuka kama mazungumzo muhimu wakati wa uchaguzi mwaka 2023, hasa haki za uzazi za wanawake katika nchi ambapo utoaji mimba unasalia kuwa suala la kutatanisha. Katika uchaguzi wa Poland, suala hilo lilikuwa kuu baada ya uamuzi wa mahakama wa 2020, ulioungwa mkono na serikali wakati huo, ambao ulizuia vikali fursa za utoaji mimba. Uamuzi huo ulifuatiwa na maandamano makubwa kote nchini, yakiongozwa na wanawake na vijana. Ripoti hiyo inadokeza kuwa hii ni sababu mojawapo iliyopelekea chama tawala kupoteza madaraka. Kwa upande mwingine, Javier Milei, ambaye aliahidi kura ya maoni kufuta sheria zinazoendelea zaidi za utoaji mimba ambazo ziliwekwa mwaka wa 2020, alichaguliwa kuwa Rais wa Argentina. Lakini hata hivyo kwa sasa kuna habari nyingine mpya yenye mashaka ambayo Bunge la Ufaransa limepitisha sheria yautoaji mimba.

Nafasi za kazi kwa wanawake
07 March 2024, 14:58