Tafuta

Mgogoro wa Palestina na Israel. Vyombo kwa ajili ya mgawo wa chakula. Mgogoro wa Palestina na Israel. Vyombo kwa ajili ya mgawo wa chakula.  (AFP or licensors)

UNICEF/Gaza:watoto wenye utapiamlo wanakufa pole pole machoni pa dunia!

Kwa mujibu wa taarifa za UNICEF"karibu watoto 10 wamekufa kwa ukosefu wa chakula na hivyo utapiamlo katika Hospitali ya Kamal Adwan,Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kwa siku kumi za mwisho.Janga hili la vifo na vya kutisha vimesababishwa na mwanadamu aliyeviandaa na ambavyo vinaweza kuzuiliwa."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika tamko la Adele Khodr, Mkurugenzi wa Kikanda wa UNICEF kwa ajili ya Nchi za Mashariki na Afrika Kaskazini amebainisha kuwa: “Vifo vya watoto ambayo tulikuwa tunaogopa vimefika, wakati kuna utapiamlo wa kutisha katika ukanda wa Gaza.” Kwa mujibu wa taarifa, “karibu watoto 10 wamekufa kwa ukosefu wa maji na chakula na hivyo kwa utapiamlo katika Hospitali ya Kamal Adwan, Kaskazini mwa Ukanda wa Gazwa kwa siku kumi za mwisho.” Hii “Inawezekana kwamba watoto wengine wapo wanapambana kwa ajili ya maisha na sehemu nyingine moja ya nyingi katika hospitali zilizobaki huko Gaza na ambazo idadi kubwa bado ni watoto katika Kaskazini ambao hawawezi kupata hata matibabu. Janga hili la vifo na vya kutisha vimesababishwa na mwanadamu aliyeviadaana na ambavyo vinaweza kuzuiwa.”

Watu wengi wana njaa

Katika taarifa hiyo bado inabaiisha kuwa “Ukosefu mkubwa wa chakula chenye lishe bora, maji salama na huduma za matibabu, matokeo ya moja kwa moja ya vikwazo vya upatikanaji na hatari nyingi ambazo operesheni za kibinadamu za Umoja wa Mataifa zinakabiliana nazo, huathiri watoto na mama, na kuzuia uwezo wao wa kunyonyesha watoto wao, hasa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. Watu wana njaa, wamechoka na wana kiwewe. Wengi hung’ang’ania maisha. Tofauti kati ya Kaskazini na Kusini ni ushahidi wa wazi kwamba vikwazo vya misaada Kaskazini vinagharimu maisha. Uchunguzi wa utapiamlo uliofanywa na UNICEF na WFP kaskazini mwa nchi mnamo Januari uligundua kuwa karibu 16% - au 1 kati ya watoto 6 walio chini ya miaka 2 - wana utapiamlo mbaya. Majaribio sawa na hayo yalifanyika kusini, huko Rafah, ambako misaada ilipatikana zaidi, na kugundua kuwa asilimia 5 ya watoto chini ya miaka 2 walikuwa na utapiamlo mkali.

Dhamana ya usalama  kwa kusambaza misaada

Mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu kama UNICEF, lazima yapewe uwezo wa kubadili mzozo wa kibinadamu, kuzuia njaa na kuokoa maisha ya watoto. Kwa hili tunahitaji viingilio vingi vya kuaminika ambavyo huturuhusu kuleta misaada kutoka kwa njia zote zinazowezekana, pamoja na ile ya kaskazini huko Gaza; na dhamana ya usalama na kifungu kisichozuiliwa kusambaza misaada, kwa kiwango kikubwa, kote Gaza, bila kupigwa marufuku, ucheleweshaji na vikwazo vya kupata. UNICEF imeonya tangu Oktoba kwamba idadi ya vifo huko Gaza itaongezeka kwa kasi ikiwa shida ya kibinadamu itaibuka na kuruhusiwa kuongezeka. Hali imezidi kuwa mbaya na kwa sababu hiyo, wiki iliyopita, tulionya kwamba mlipuko wa vifo vya watoto unakaribia ikiwa shida ya lishe inayoendelea haitatatuliwa.

Dunia inatazama watoto tu  wakifa pole pole

 

Sasa, vifo vya watoto tulivyohofia viko hapa na huenda vitaongezeka kwa kasi isipokuwa vita vitakapoisha na vikwazo vya misaada ya kibinadamu vitatatuliwa mara moja.” Hisia ya kutokuwa na msaada na kukata tamaa ya wazazi na madaktari katika kutambua kwamba msaada wa kuokoa maisha, kilomita chache tu kutoka kwao, lazima usiwe na uwezo wa kustahimili, lakini mbaya zaidi ni vilio vya uchungu vya watoto hao ambao wanakufa polepole chini ya mtazamo wa macho ya dunia. Maisha maelfu ya watoto wachanga na watoto yanategemea hatua zinazochukuliwa haraka.”

04 March 2024, 12:35