Tafuta

Wapalestina wakitembea katika magofu ya nyumba zilizoharibiwa sana. Wapalestina wakitembea katika magofu ya nyumba zilizoharibiwa sana. 

Israel yafungua vivuko vya mpakani kwa ajili ya usaidizi kuelekea Gaza

Ikulu ya Marekani yaridhishwa na tangazo la serikali ya Israel kujitolea kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Ukanda wa Gaza.Masharti ya kusitisha mapigano ni kuachiliwa kwa mateka wa Israel.

Vatican News

Baada ya shambulio baya dhidi ya msafara wa World Central Kitchen na kufuatia simu kati ya Netanyahu na Rais wa Marekani Joe Biden, Israel iko 'wazi' kwa msaada zaidi kwa Ukanda wa Gaza, unaozingirwa na kutishiwa na njaa. Ujumbe kutoka kwa waziri mkuu wa Israel ulithibitisha kuwa Baraza la mawaziri la usalama la Israel liliidhinisha “hatua za mara moja za kuongeza misaada ya kibinadamu kwa raia katika Ukanda huo” kupitia bandari ya Ashdod na kivuko cha Erez. Tangazo ambalo linakuja wakati wa shinikizo kubwa zaidi la kimataifa kwa serikali ya Israeli. “Ongezeko hili la misaada litatumika kuepusha mzozo wa kibinadamu na ni muhimu kuhakikisha kuendelea kwa mapigano na kufikia malengo ya vita, ndivyo yanasomeka maelezo kutoka kwa Waziri mkuu wa Israel.

Ukosoaji wa kimataifa

Kifo cha wafanyakazi saba Jumatatu tareh Mosi Aprili  2024 kutoka shirika lisilo la kiserikali la World Central Kitchen (WCK) wakati wa uvamizi wa Israel kimeongeza kutoridhika kimataifa. Jeshi la Israel lilikiri “kosa kubwa,” lakini shutuma za kimataifa zilikuwa zikishinikiza Tel Aviv. “Shambulio la kutisha la Juma hili dhidi ya  World Central Kitchen (WCK) halikuwa la kwanza la aina yake. Ni lazima liwe la mwisho,” alisisitiza Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bwana Antony Blinken wakati wa sherehe za Nato mjini Brussels tarehe 4 Aprili 2024 kwa ajili ya kuadhimisha miaka 75 tangu kuzaliwa kwa Muungano huo. Na wakati tarehe 5 Aprili 2024 Ikulu ya Marekani imeeleza kuridhishwa na maamuzi ya Israel:“Tutafanya kazi kwa uratibu kamili na Serikali ya Israel, Serikali ya Jordan na Misri, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kibinadamu, ili kuhakikisha kwamba hatua hizi zinachukuliwa na kusababisha ongezeko kubwa la utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa raia ambao wamehitaji sana kote Gaza katika siku na wiki zijazo,” msemaji wa Ikulu ya alisema.

Shida ya Gaza

Hivi sasa kumekuwa na zaidi ya wahanga elfu 33 tangu kuanza kwa vita dhidi ya Hamas. Hili lilifahamishwa na mamlaka ndani ya Ukanda wa Gaza, lakini mgogoro wa kibinadamu unathibitishwa na mashirika mengi huru ya kimataifa. Oxfam inaripoti kuwa idadi ya raia sasa wanaishi na 12% tu ya mahitaji ya chakula muhimu kwa ajili ya kuishi na Shirika la Msalaba Mwekundu la Palestina limefahamisha vifo vya watoto 31 kutokana na njaa na upungufu wa maji mwilini.

Sehemu zingine za vita

Mpalestina mmoja aliuawa katika makabiliano na jeshi la Israel katika kambi ya wakimbizi ya Nour Shams, mashariki mwa Tulkarem katika Ukingo wa Magharibi. Gazeti la Times of Israel, likinukuu polisi, akiripoti kuwa maafisa walivamia mji wa Tulkarem Ukingo wa Magharibi ili kuwakamata Wapalestina watatu waliokuwa wakisakwa wanaoshukiwa kuhusika na shughuli za kigaidi. Polisi walisema maafisa waliwazuilia watu waliokuwa wanatafutwa na walipokuwa wakiondoka mjini, ghasia kali zilizuka, ambapo "gaidi aliondolewa na vikosi vya siri baada ya kurusha kifaa cha vilipuzi upande wao." Tahadhari bado iko juu ndani ya Israeli kutokana na tishio la kulipiza kisasi kutoka kwa Iran, baada ya uharibifu huko Damasco wa jengo linalotumiwa na uwakilishi wa kidiplomasia wa Tehran.

 

05 April 2024, 14:52