Italia,Save the Children:dharura kwa watoto waathirika wa vurugu za nyumbani!
Na Angella Rwezaula –Vatican.
Mnamo 2023, kulikuwa na zaidi ya watoto 5,000 waliokuwa wakiishi pamoja waliohusika moja kwa moja au isivyo moja kwa moja katika vipindi vya ukatili wa nyumbani au kijinsia dhidi ya wanawake. Maombi 2,100 ya kuomba msaada yalipokelewa na Jeshi la Polisi kwa madai ya vurugu zilizofanywa moja kwa moja na watoto wadogo. Na katika hali nyingi tunazungumza juu ya watoto wenye umri wa miaka kumi au chini. Ufafanuzi ambao haujawahi kushuhudiwa wa jambo hili zito na Shirika la Saidia Watoto (Save the Children,) kwa ushirikiano wa majaribio na Huduma ya Uchambuzi wa Uhalifu, unaonyesha idadi ya wasiwasi, ambayo, pamoja na mambo mengine, inaonesha maombi 13,793 ya usaidizi na uingiliaji kati wa vipindi vya unyanyasaji wa nyumbani au jinsia inayoteseka na wanawake. nchini Italia.
Takwimu zinazotolewa na Huduma ya Uchambuzi wa Uhalifu, kwa mujibu wa Bi Raffaela Milano, Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo wa Save the Children nchini Italia alisema kuwa ni muhimu sana kwa kuchunguza jambo, lile la unyanyasaji unaofanywa na watoto nyumbani.” Zaidi ya yote, mhusika huyo alisisitiza uzito wa aina hii ya unyanyasaji, kwamba sio tu kwa wale watoto wa kike na kiume ambao ni waathiriwa wa moja kwa moja, lakini pia kwa wale wanaoshuhudia zaidi tabia ya ukatili zinayofanywa dhidi ya mama zao.
“Kiukweli, hata kushuhudia vurugu huacha majeraha makubwa ambayo ni vigumu kushinda. Alisema ma kwamba “Watoto mara nyingi ni mashahidi wa unyanyasaji wa nyumbani, na mara nyingi hii ina madhara makubwa juu ya maendeleo yao ya kisaikolojia na kimwili, ambayo yanaweza pia kuendelea hadi kufikia kuwa watu wazima. Hofu ya mara kwa mara, hali ya kutokuwa na msaada na kutokuwa na uwezo wa kuguswa ni alama ya ukuaji wa maisha haya ya vijana. Athari za kisaikolojia ni mbaya sana unapoona mama zako wakiuawa na baba zao.”
Katika utafiti uliofanywa, tunasoma kuwa “Katika muktadha wa uingiliaji kati ulioainishwa kwa madai ya unyanyasaji wa kinyumbani/kijinsia ambapo mwathiriwa anayedaiwa ni mwanamke, ni katika 1.5% tu ya kesi ambayo ni mwathiriwa asiyejulikana kwa mwathirika. Katika 61.5% ya kesi, mhalifu anahusishwa na mwathirika na uhusiano wa kimapenzi. Katika asilimia 42 ya matukio haya ya ukatili unaofanywa na wanandoa/wapenzi/wake wenza kwa madhara ya wanawake, inaonekana kuna watoto wanaoishi pamoja. Kwa kuzingatia takwimu hizi, inaonekana “ni muhimu kukuza uwezo wa kugundua mara moja ishara yoyote ya dhiki", alielezea Stefano Delfini, Mkurugenzi wa Huduma ya Uchambuzi wa Uhalifu wa Kurugenzi Kuu ya Polisi ya Jinai ya Idara ya Usalama wa Umma.
Unyanyasaji unaoshuhudiwa na unyanyasaji wa watoto hasa ni katika maeneo ya siri na magumu kufahamu hivyo basi kuna haja ya kufanya kazi kama timu”,alisisitiza mhusika huyo. Shirika la Save the Children Italia, daima imekuwa ikijitolea kwa mipango ya kuzuia na kulinda wanawake waathriwa wa unyanyasaji, watoto wao waathiriwa wa dhuluma inayoshuhudiwa na watoto mayatima kutokana na mauaji ya wanawake.