Jeshi la Polisi nchini Haiti linajaribu kuongeza nguvu ya usalama wa katika Ikulu ya Port-au-Prince.                                                                                         5565666 Jeshi la Polisi nchini Haiti linajaribu kuongeza nguvu ya usalama wa katika Ikulu ya Port-au-Prince. 5565666  (ANSA)

Haiti:Jeshi la polisi la kimataifa litatumwa nchini Haiti si zaidi ya wiki tatu

Mnamo Oktoba 2023,Kenya ilijitolea kuongoza ujumbe wa usalama nchini Haiti na kuahidi kutuma hadi maafisa 1,000 kusaidia polisi wa Haiti katika kudumisha usalama.Maafisa wengine 1,500 wameahidiwa kutoka nchi nyingine zikiwemo Jamaica,Barbados,Bangladesh,Benin na Chad.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ujumbe wa kimataifa unaoongozwa na Kenya nchini Haiti hautatumwa kabla ya wiki tatu zijazo. Alisema hayo Rais wa Kenya Bwana William Ruto katika mahojiano na Shirika la Habari la Uingereza (BBC). Utumaji wa awali wa maafisa 200 wa polisi wa Kenya ulipaswa kutua Haiti mnamo Mei 23, lakini kuwasili kwao kuliahirishwa dakika za mwisho.  Rais Ruto nchini Kenya alieleza kuwa kuchelewa kuwasili kwa kikosi hiki cha kwanza cha polisi kumetokana na ugumu wa kuandaa miundo ambayo italazimika kukidhi kikosi cha kimataifa na ukosefu wa silaha na vyombo vya usafiri. Mnamo Oktoba, Kenya ilijitolea kuongoza ujumbe wa usalama nchini Haiti na kuahidi kutuma hadi maafisa 1,000 kusaidia polisi wa Haiti katika kudumisha usalama. Maafisa wengine 1,500 wameahidiwa kutoka nchi nyingine zikiwemo Jamaica, Barbados, Bangladesh, Benin na Chad.

Maisha ya watu wa Haiti wanaishi bila usalama
Maisha ya watu wa Haiti wanaishi bila usalama

Jeshi la polisi la kimataifa litakuwa na jukumu la kusaidia vikosi vya usalama vya ndani kudhibiti ghasia za magenge ambayo yamelipuka nchini Haiti katika miezi ya hivi karibuni. Mwezi Machi 2024, magenge ya wahalifu yalishambulia magereza makubwa mawili ya nchi hiyo, na kuwaachia huru zaidi ya wafungwa 4,000, kuuzingira uwanja wa ndege na kumlazimisha Ariel Henry, waziri mkuu wa nchi hiyo kwenda uhamishoni. Henry amejiuzulu tangu wakati huo. Ujumbe huo wa kimataifa pia unakabiliwa na upinzani kutoka katika magenge ya wahalifu. Kundi la G9 na G-Pèp, miungano kati ya magenge yaliyokuwa waasi nchini Haiti, yameungana kupinga ujumbe wa usalama, na kuunda kikundi kiitwacho Vivre Ensemble.

Megenge ya kihalifu yenye silaha nchini Haiti yanaleta ghasia kubwa
Megenge ya kihalifu yenye silaha nchini Haiti yanaleta ghasia kubwa

Hata hivyo silaha zinaendelea kumiminika nchini, baadhi ya hizo huenda zikatokana na wizi katika kambi katika nchi za Amerika Kusini kama vile Colombia. Jambo la hakika ni kwamba magenge ya Kihaiti yanaonesha silaha za hali ya juu zaidi, kama alivyoeleza Sr  Marcella Catozza wa Jumuiya ya Wamisionari ya Kifransisko wa Busto Arsizio, ambaye amekuwa katika utume huko  Haiti kwa miaka 20, akizungumza na Shirika la Habari za kimisionari Fides. Silaha ambazo labda pia zilinunuliwa kwa ushirikiano wa wajasiriamali watatu wa Haiti ambao waliwekewa vikwazo na Serikali ya Canada mnamo Desemba 2022 kwa madai ya “kunyonya hadhi yao kama wanachama mashuhuri wa wasomi wa uchumi wa Haiti kulinda na kuwezesha shughuli haramu za magenge ya uhalifu, ikiwa ni pamoja na uchakachaji fedha na vitendo vingine vya rushwa.” Watatu hao ni Gilbert Bigio, rais wa Kikundi cha GB cha viwanda cha Haiti pamoja na wafanyabiashara Reynold Deeb na Sherif Abdallah. Wakati huo huo, hali ya kibinadamu ni ya kustaajabisha kwani hali ya vurugu hazioneshi dalili zozote za kupungua. Mnamo tarehe 23 Mei 2024, wamisionari wawili vijana Waprotestanti Waamerika, Natalie na Davy Lloyd, pamoja na msindikizaji wao wa Haiti, Jude Montis, waliuawa katika ukanda wa Cul ya Sac.

Kikosi cha Polisi kutoka Kenya kitawasili hivi karibuni nchini Haiti
29 May 2024, 10:34