Uwanja wa Mpira jijini  Roma utakaribisha Siku ya I ya Watoto Duniani Jumamosi tarehe 25 Mei 2024 . Uwanja wa Mpira jijini Roma utakaribisha Siku ya I ya Watoto Duniani Jumamosi tarehe 25 Mei 2024 . 

Mkurugenzi wa UNICEF na Siku ya I ya Watoto Duniani mjini Vatican!

Katika fursa ya Siku ya I ya Watoto duniani(GMB)inayofanyika mjini Vatican 25 na 26 Mei 2024,Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF amesisitiza kuwa Maelfu ya watoto watashiriki ili kuhamasisha amani na haki za watoto wa Ulimwengu mzima.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maelfu  ya watoto na watu wa kujitolea wa UNICEF wanashiriki na wengine ili kuadhimisha miaka 50 ya UNICEF nchini Italia. Katika muktadha huo tarehe 25 Mei 2024, Bi Catherine Russell Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF naye anashiriki na maelfu ya watoto katika Uwanja wa Olimpiki jijini Roma ili kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Kwanza ya Vatican kwa ajili ya Watoto iliyohamasishwa na Baba Mtakatifu Francisko na kuandaliwa na Baraza la Kipapa Utamaduni na Elimu kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Cooperativa Auxulium.

Tuwe mawala wa mabadiliko chanya kwa ulimwengu

Bi Russell, ambaye pia alisafiri kuja Roma Juma hili  kukutana na wawakilishi wa taasisi, anashiriki katika Mkutano wa alasili ili kusisitiza  hali ya watoto walio hatarini zaidi, hasa wale walioathiriwa na migogoro, umaskini na shida ya tabianchi. Bi Russell atawahimiza makumi ya maelfu ya watoto katika uwanja wa michezo - na wengi zaidi wanaotazama duniani kote kupitia viunga mbali mbali na majukwa ya mitandao – “kuendelea kuwa mawakala wa mabadiliko chanya kwa ulimwengu wenye amani zaidi, usawa na kuishi. pamoja” “Kuna mamia ya mamilioni ya watoto duniani kote ambao maisha yao yanaendelea kusambaratishwa na vita na ghasia, umaskini na ukosefu wa usawa, na athari za mabadiliko ya tabianchi. “Mkurugenzi Mkuu wa  UNICEF Bi  Catherine Russell alisema  hayo kabla ya tukio hili muhimu . Aidha alibainisha kuwa “Huu ni wakati muhimu wa kuja pamoja katika ari ya kukuza amani na haki za watoto wote, kila mahali, ni lazima tusikilize sauti za watoto na kutambua ulimwengu unaofaa kwa kila mtoto wa leo na vizazi vijavyo.”

Zaidi ya watoto 3,700 wa Italia watashiriki na wenzao 

Zaidi ya watoto 3,700 kutoka nchini  Italia watakuwepo kwenye Uwanja wa Olimpiki kwa msaada wa UNICEF Italia na mamia ya watu waliojitolea. Mwaka huu  2024 ni mwaka wa 50 wa UNICEF  nchini Italia katika  shughuli za utetezi na uchangishaji fedha na watu wa Italia wa msaada wa muda mrefu kwa watoto duniani kote.” “ Leo, watoto milioni 400 – au takriban mtoto 1 kati ya 5 – wanaishi au wanakimbia maeneo yenye migogoro, katika maeneo kama vile Gaza, Haiti, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC), Sudan, Ukraine na Yemen. Wengi huuawa, kujeruhiwa au kuteseka kwa aina kali za vurugu. Wanapoteza familia na marafiki na kupata huduma muhimu, ikiwa ni pamoja na elimu. Umoja wa Mataifa ulithibitisha zaidi ya ukiukwaji mkubwa 315,000 wa haki za watoto katika maeneo yenye migogoro kati ya 2005 na 2022. Na hizi ni kesi zilizothibitishwa, ambayo ina maana kwamba idadi halisi ya ukiukaji hakika ni kubwa zaidi.” Vile vile “Ulimwenguni, zaidi ya watoto bilioni 1 kwa sasa wanaishi katika nchi ambazo ziko katika “hatari kubwa sana” kutokana na athari za mabadiliko ya Tabianchi.”

UNICEF NA WATOTO KATIKA SIKU YA KWANZA YA WATOTO DUNIANI
25 May 2024, 13:00