Tafuta

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limebainisha kuwa “Bei za vyakula duniani zimepanda kwa miezi mitatu mfululizo, mwezi Mei,asilimia kubwa ikiwa katika ongezeko la gharama ya nafaka. Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limebainisha kuwa “Bei za vyakula duniani zimepanda kwa miezi mitatu mfululizo, mwezi Mei,asilimia kubwa ikiwa katika ongezeko la gharama ya nafaka. 

FAO:Bei ya chakula duniani imepanda kwa mwezi wa tatu mfululizo!

Tathimini ya bei ya chakula ya FAO,ambayo hufuatilia mabadiliko ya kila mwezi ya gharama ya bidhaa kuu za chakula duniani kote,ilikuwa pointi 120.4 mwezi Mei,ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.9 kutoka mwezi Aprili,lakini asilimia 3.4 chini ya kiwango cha 2023 na asilimia 24.9 chini ya kile kilichorekodiwa mwezi Machi 2022.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 7 Juni 2024 na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limebainisha kuwa “Bei za vyakula duniani zimepanda kwa mwezi wa tatu mfululizo kwa mwezi Mei, asilimia kubwa ikiwa katika ongezeko la gharama ya nafaka na bidhaa za maziwa, lilizidi kupungua na bei ya sukari na mafuta ya mboga. Tathimini ya bei ya chakula ya FAO, ambayo hufuatilia mabadiliko ya kila mwezi ya gharama ya bidhaa kuu za chakula duniani kote, ilikuwa pointi 120.4 mnamo mwezi Mei, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.9 kutoka mwezi Aprili, lakini asilimia 3.4 chini ya kiwango cha mwaka 2023 uliopita na asilimia 24.9 chini ya kilele kilichorekodiwa mwezi Machi 2022.

Bei ya nafaka

Tathimini hiyo ilibainisha kuwa bei ya nafaka iliongezeka kwa asilimia 6.3 ikilinganishwa na mwezi Aprili. Hii iliungwa mkono na kupanda kwa bei ya ngano duniani kote, ikionesha wasiwasi unaoongezeka kuhusu hali mbaya ya mazao katika kanda muhimu zinazozalisha nafaka hiyo. Bei za mauzo ya mahindi pia zimeelezewa kupanda, zikisukumwa na matatizo ya uzalishaji nchini Argentina kutokana na ugonjwa wa Spiroplasma na nchini Brazili kutokana na hali mbaya ya hewa, pamoja na shughuli chache za mauzo nchini Ukraine. Na kwa upande wa tathimini ya bei ya mchele iliongezeka kwa asilimia 1.3 mwezi Mei. Tathimini ya bei ya maziwa ilionesha kupanda kwa asilimia 1.8 kutoka mwezi Aprili, huku ikiongezeka kwa mahitaji kabla ya likizo ya majira ya joto na matarajio ya soko kwamba uzalishaji wa maziwa katika eneo la Ulaya Magharibi unaweza kushuka chini ya viwango vya kihistoria.

Kwa upande wa Afrika

Mahitaji mapya ya uagizaji bidhaa kutoka katika baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini pia yalichangia kupanda kwa bei ya bidhaa za maziwa. Na bei ya sukari ilishuka kwa asilimia 7.5 kuanzia Aprili, hasa kutokana na mwanzo mzuri wa msimu nchini Brazili.  Bei ya chini ya mafuta ghafi duniani pia imeweka shinikizo kwa bei ya sukari, na hivyo kupunguza mahitaji. Kwa upande wa bei ya mafuta ya mboga, ilipungua kwa asilimia 2.4 ikilinganishwa na Aprili. Kwa upande wa bei ya nyama FAO ilisema kuwa ilishuka kwa asilimia 0.2, na bei za kimataifa za kuku na ng'ombe zikianguka huku mayai na nyama ya nguruwe zikipanda.

Mazao ya Nafaka kwa wakulima
Mazao ya Nafaka kwa wakulima

Katika taarifa hiyo aidha  FAO ilitoa utabiri wake wa kwanza wa msimu wa mwaka 2024-25, huku ikitoa wito kwa uzalishaji wa nafaka duniani kufikia tani milioni 2,846, kulingana na rekodi ya uzalishaji ya 2023-24. Uzalishaji wa kimataifa wa mahindi na ngano unakadiriwa kupungua, huku uzalishaji wa shayiri, mpunga na mtama ukitarajiwa kuongezeka. Hali mbaya ya hewa ya hivi karibuni katika eneo la Bahari Nyeusi huenda ikapunguza uzalishaji wa ngano duniani.

Ukulima wa mazao ya nafaka
Ukulima wa mazao ya nafaka

Jumla ya matumizi ya nafaka duniani yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 0.5 mwaka 2024-25 hadi rekodi mpya ya juu ya tani milioni 2,851, ikisukumwa na kuongezeka kwa matumizi ya chakula, hasa mchele. Hifadhi ya nafaka ya kimataifa huenda ikaongezeka pia kwa asilimia 1.5 kutoka viwango vyake vya mwanzoni mwa mwaka, na kufikia rekodi ya tani milioni 897. Hesabu za mahindi, shayiri, mtama na mchele zinatarajiwa kuongezeka, huku akiba ya ngano ikapungua. FAO inakadiria kuwa biashara ya nafaka duniani itashuka kwa asilimia 1.3 mwaka baada ya mwaka hadi kufikia tani milioni 481, ikichochewa na matarajio duni ya biashara ya mahindi.  Biashara ya kimataifa ya mchele nayo inakadiriwa kukua kwa kasi.

Uwekeaji wa mbolea katika mahindi
Uwekeaji wa mbolea katika mahindi
12 June 2024, 11:15