2024 Kongamano la Biashara kati ya Korea Kusini na Afrika. 2024 Kongamano la Biashara kati ya Korea Kusini na Afrika. 

Korea Kusini na malengo kwa Nchi za Afrika katika mkakati wa madini

Rais Yoon Suk Yeol alisema tarehe 5 Juni 2024 kwamba Korea Kusini itaanzisha ushirikiano muhimu wa madini na mataifa makubwa ya Afrika ili kuendeleza rasilimali katika bara hilo kwa njia ya kunufaishana na msaada wa Umoja wa Mataifa.Ni katika kilele cha Mkutano wa Kibiashara kati ya Korea Kusini na bara la Afrika.

Na Angella Rwezaula  - Vatican.

Ukuaji wa pamoja, uendelevu na mshikamano, hizo ndizo nguzo tatu za ushirikiano kati ya nchi za Afrika na Korea Kusini, kulingana na taarifa ya pamoja iliyotolewa mwishoni mwa Kongamano la Wakuu wa Afrika na Korea Kusini, uliomalizika huko jijini Seoul mnamo tarehe 5 Juni 2024.  Kwa upande wa Rais Yoon Suk Yeol wa Korea akizungumza alitangaza kwamba nchi yake itaanzisha ushirikiano wa madini na baadhi ya mataifa katika bara hilo na kwamba “Jukumu la Afrika limekuwa muhimu zaidi kutokana na kutotabirika kwa mfumo wa ugavi wa kimataifa unaosababishwa na hatari za kijiografia. Natumaini kuanzisha ushirikiano muhimu wa madini na mataifa ya Afrika na kupanua ushirikiano wa kunufaishana katika rasilimali kupitia ushirikiano muhimu wa usalama wa madini na nchi ambazo zina thamani sawa. Shirika la habari la serikali la Yonhap liliripoti kuwa wawakilishi wa Afrika walikubali kuzindua mazungumzo ya ngazi ya mawaziri ya madini ili kuhakikisha kuwa kuna msururu wa ugavi wa rasilimali zinazohitajika kwa teknolojia muhimu. Ufikiaji wa Korea Kusini kwa Afrika ni hatua ya kimkakati. Waziri wa Mambo ya Nje Cho Tae-yul alisema Afrika ni  “mshirika muhimu wa Korea katika kutimiza matarajio yake ya sera ya kigeni".

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol akizungumza wakati wa Mkutano huko Korea tareje 5 Juni
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol akizungumza wakati wa Mkutano huko Korea tareje 5 Juni

Kwa njia hiyo, nchini Korea Kusini inajiunga na safu ya nchi mbali mbali zisizo za Kiafrika kama vile (China, Marekani, Ufaransa, Japan, Italia, Uingereza, Uturuki) au taasisi za bara (kama vile Jumuiya ya Ulaya) zinazoalika wakuu wa nchi na serikali za Kiafrika kwenye mkutano wa pamoja. Nia ya Seoul katika bara la Afrika inazingatia mada tatu: upatikanaji wa malighafi ya kimkakati; kuundwa kwa masoko mapya ya bidhaa zake na msaada wa kisiasa katika mashirika ya Umoja wa Mataifa; hasa kuhusu Pyongyang.

Mbio mpya za frika za mataifa makubwa na ulubwa wa kati

Kwa upande wao, nchi za Kiafrika zinaona katika mbio hizi mpya za Afrika za mataifa makubwa na ya ukubwa wa kati fursa ya kujinasua kutoka katika mantiki ya zamani ya baada ya ukoloni (hii inatumika kwa makoloni ya zamani ya Ufaransa) na kuweza kufanya mazungumzo ya  hali bora badala ya malighafi zao au usaidizi wao wa kisiasa na kimkakati (kwa mfano, kuhusu uhamisho wa kambi za kijeshi kwa mamlaka zisizo za Kiafrika).

Washiriki wa mkutano huo

Mkutano wa Seoul ulihudhuriwa na nchi 48 za Afrika (30 zikiwakilishwa na Wakuu wa Nchi zao), pamoja na wawakilishi wa Umoja wa Afrika (UA) na Kundi la Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Korea Kusini imeahidi kuongeza mara dufu misaada yake ya maendeleo kwa Afrika hadi dola bilioni 10 ifikapo 2030 na kutoa dola bilioni 14 katika ufadhili wa mauzo ya nje ili kusaidia makampuni ya Korea kuongeza biashara na uwekezaji wao katika bara hilo. Seoul pia inaunga mkono mpango wa kuunda soko moja la Afrika, kama inavyotarajiwa katika mikataba ya kuanzisha Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA). Katika muktadha huo, Korea Kusini inakubali kusaidia kuunda taratibu za forodha ili kuwezesha biashara ya ndani ya Afrika.

Rais wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani akizungumza huko Korea Kusini
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani akizungumza huko Korea Kusini

Serikali ya Korea pia inakusudia kuongeza jukumu la makampuni ya ndani katika ujenzi wa miundombinu kutoka ile ya kijadi:(barabara, reli, madaraja, bandari, viwanja vya ndege, mabwawa, mitambo ya kusafisha maji ya bahari, mifumo ya usimamizi wa umeme na maji) kwa  miundombinu ya ubunifu(inayoitwa miji yenye akili), na kuiweka katika ushindani wa moja kwa moja sio tu na China bali pia na nguvu ya ukubwa wa kati kama Uturuki. Kulingana na Seoul, uwekaji kidigitali wa tawala za mataifa ya Afrika unaweza kuchukua fursa ya programu ambazo tayari ziko nchini Korea Kusini. Kwa kuongezea, nchi hiyo ya Asia imejitolea “kuboresha ujuzi wa kidijitali wa vijana barani Afrika” kupitia mafunzo na ufadhili wa masomo kama sehemu ya mpango wa “Tech4Africa Initiative.” Hizi ni hatua laini za nguvu zinazolenga kuanzisha uhusiano na viongozi wa baadaye wa Kiafrika katika siasa na biashara katika muda wa kati hadi mrefu. Korea Kusini aidha inatafuta kuingia katika soko kubwa na linalokua kwa kasi linalojumuisha watu bilioni 1.4, wengi wao wakiwa na umri wa chini ya miaka 25, kwa kusaidia miundombinu ya viwanda na mabadiliko ya kidijitali.

Upatikanaji madini barani Afrika

Hata hivyo, upatikanaji wa rasilimali za madini barani Afrika, ambao unapingwa na mataifa yote yenye nguvu duniani, kwa sasa ni jambo la kipaumbele. Wakati wa mkutano huo, “Mazungumzo muhimu ya Madini kati ya Korea na Afrika” yalizinduliwa, ambayo yatatumika kama msingi muhimu wa kitaasisi katika kuimarisha ushirikiano wa Korea na Afrika. “Tuna maono ya pamoja ya kuimarisha ushirikiano ili kuhakikisha upatikanaji wa kutosha wa madini muhimu na kukuza ushirikiano wa kiteknolojia katika madini muhimu kwa masharti yaliyokubaliwa,” ilisema taarifa hiyo ya pamoja, ikifungua njia ya ushirikiano ambao unapita zaidi ya uchimbaji wa madini ili kuunda madini,  mnyororo wa usindikaji barani Afrika kwa uchumi wa hali ya juu zaidi. Kwa upande wa kisiasa, dhamira ya Seoul ya “kuchangia amani na usalama barani Afrika, ikiwa ni pamoja na uboreshaji na upanuzi wa miradi ya ushirikiano katika nyanja za ulinzi, sekta ya ulinzi na usalama wa umma kati ya Korea na Afrika “haiwezi kupuuzwa.

Rais wa Mauritania na Rais wa Korea katika Mkutano wa kibiashara
Rais wa Mauritania na Rais wa Korea katika Mkutano wa kibiashara

Marejeo ya sekta ya ulinzi yanavutia ikizingatiwa kuwa Korea Kusini inashika nafasi ya kumi kwenye orodha ya mataifa yanayouza silaha kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni iliyochapishwa na SIPRI (Trends in International arms Transfers 2023.)  Hatimaye, Seoul ina nia ya kijiografia katika kudumisha nafasi yake katika miili ya Umoja wa Mataifa katika kambi za nchi 54 ambazo zinashikilia viti vitatu vya kupokezana katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Sio kwa bahati mbaya kwamba aya ya 21 ya taarifa ya pamoja inasema: “Tunasisitiza ahadi yetu ya utekelezaji kamili wa maazimio yote ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusisitiza umuhimu wa juhudi za jumuiya ya kimataifa kufikia uondoaji kamili wa nyuklia wa peninsula ya Korea.

Rais wa Mauritania ambaye pia ni wa Umoja wa Afrika akimkaribisha Rais wa Korea
Rais wa Mauritania ambaye pia ni wa Umoja wa Afrika akimkaribisha Rais wa Korea

Kando ya kikao kikuu, Rais Yoon alifanya mikutano tofauti na viongozi kama vile wa Kenya, Madagascar, Liberia na Ghana.  Kwa njia hiyo Rais  Yoon alikutana na viongozi 13 wa Afrika kutia saini makubaliano kadhaa ili kufungua njia ya kupanua biashara na uwekezaji na ushirikiano katika madini muhimu, ushirikiano wa teknolojia na uchunguzi wa pamoja. Nchi hizo ni pamoja na Sierra Leone, Tanzania, Ethiopia, Lesotho, Ivory Coast, Mauritius, Zimbabwe, Togo, Rwanda, Msumbiji, Sao Tome na Principe, Guinea-Bissau na Cape Verde.

Korea Kusini na Bara la Afrika
17 June 2024, 11:03