Rais wa Ukraine Zelensky akikaribishwa na Waziri Mkuu wa Italia wakati wa G7. Rais wa Ukraine Zelensky akikaribishwa na Waziri Mkuu wa Italia wakati wa G7.  (ANSA)

Makubaliano yalifikiwa katika G7 juu ya msaada kwa Ukraine

Mkutano wa G7, umehitimishwa uliowaleta pamoja wakuu wa dunia,uliofanyika katika eneo la kifahari la Borgo Egnazia,Kusini mwa Italia.Mara tu makubaliano ya msaada kwa Ukraine yalipofikiwa kwenye meza ya majadiliano na euro bilioni 50 za Kirusi zilitolewa kusaidia Kyiv.

Na  Angella Rwezaula – Vatican.

Kuanzia tarehe 13 hadi 15 umefanyika mkutano wa Wakuu wa mataafa mbali mbali ya dunia (G7) ambapo  Alhamisi 13 Juni 2024, mkopo wa kipekee kwa Ukraine ulitangazwa kuwa ni  bilioni 50 ambazo zitakopeshwa kutoka  Marekani(5) na Canada(2)  na Japan, wakati takwimu za Umoja wa Ulaya zitafafanuliwa katika Baraza lijalo la Ulaya. Mkopo huo utafadhiliwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa kutumia mali zilizohifadhiwa kwa Urusi kama matokeo ya vikwazo vya kimataifa.

Rais wa Ukraine alikutana pia na rais wa India
Rais wa Ukraine alikutana pia na rais wa India

Matumizi ya fedha 

Pesa hizo zitatumika kugharamia gharama za kijeshi za jeshi la Ukraine na ujenzi wa miundombinu ya nishati ya nchi hiyo, ambayo imekuwa ikipigana dhidi ya uvamizi huo kwa zaidi ya miaka miwili. Pia katika siku ya ufunguzi, rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, na mkuu wa nchi ya Marekani, Joe Biden, pia walitia saini makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya usalama. Makubaliano hayo ambayo yatadumu kwa miaka 10, yanaeleza kuwa iwapo kutatokea shambulio pande husika zitalazimika kushauriana ndani ya saa 24 ili kukubaliana kuhusu hatua za kujihami zitakazochukuliwa.

Giorgia Meloni, Waziri Mkuu wa Italia
Giorgia Meloni, Waziri Mkuu wa Italia

Viongozi wa G7 waungana kwa ajili ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza

Ukanda wa Gaza bado umekuwa katika matazamoa wa viongozi hawa na hasa kuhusu suala la kuachiliwa kwa mateka, kusitishwa mapigano mara moja na kuwepo kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina tangu siku moja baada ya kumalizika kwa mapigano hayo, ndivyo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliomba, kuhusiana na suala la vita vya Palestina, mwishoni mwa  siku ya kwanza ya mkutano huko Borgo Egnazia. Watu wengine wenye nguvu wa Dunia waliongeza kukubaliana na hatua hiyo. Rais wa Marekani Bwana Joe Biden, licha ya kuwa ameonesha mashaka juu ya uwezekano wa kupata usitishaji mapigano mara moja, hata hivyo aliwataka Hamas kukubali pendekezo la usitishaji vita, ambalo bado liko kwenye meza ya mazungumzo. Rais wa Tume ya Ulaya Bi Ursula von der Leyen, akiwa kando ya mkutano huo, alikabidhi tamko lake juu ya vita katika Ukanda wa X: “Tuko tayari kufanya jukumu letu kwa hatua za haraka na zenye ufanisi, ambazo zinaweza kupelekea suluhisho la Nchi mbili.

Wahusika wakuu wa G7
Wahusika wakuu wa G7
15 June 2024, 15:24