Papa kwa Maandamano ya kitaifa ya maisha: kilicho hatarini ni hadhi ya mwanadamu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumamosi tarehe 22 Juni 2024, katika mitaa ya jiji la Roma itawaona katika matembezi, maelfu ya akina mama, baba na watoto wakiwa katika sherehe ambayo watahuisha maandamano ya kitaifa yenye kauli mbiu: “Chagua Maisha.” Hili ni tukio muhimu zaidi la umma nchini Italia la kutetea na kukuza heshima ya maisha ya mwanadamu tangu kutungwa kwa mimba hadi kifo chake cha asili ambapo ni ukweli wa vyama 130 vitakavyoshiriki na vinavyofuatilia.
Katika ujumbe wake Baba Mtakatifu Francisko wa tukio hili, "anawashukuru wale waliojiandaa na wale watakaoshiriki katika maandamano hayo kwa kutoa “ushuhuda wa hadharani katika kutetea maisha ya binadamu tangu kutungwa kwa mimba hadi kifo cha kawaida na ahihimiza kusonga mbele kwa ujasiri licha ya shida zote kwa sababu, zaidi, kuna vigingi, ambavyo vinaweka changamoto ya hadhi kamili ya maisha ya mwanadamu, ambayo ni zawadi ya Mungu Muumba, na ni ya juu sana kuwa fundisho la maelewano au upatanishio."
Shuhuda za wale waliochagua maisha
Waandaaji wa maandamamo hayo waliliripoti kuwa msafara huo utahudhuriwa na familia nyingi zinazotarajiwa kutoka Italia nzima na hivyo (mabasi mengi tayari yameandaliwa). Maandamano yataanzia katika Uwanja wa Jamhuri, majira ya saa 8.00 mchana hadi kuwasili kupitia Njia ya Cavour kwenye Fori Imperiali, na kuelekea Altare della Patria (Altare ya Nchi.(Uwanja wa Venezia).
Kutoka vituo viwili vilivyowekwa mwanzoni na mwisho wa maandamano, kuwakuwa na ushikishwaji wa ushuhuda wa familia, ya mama na baba ambao wamechagua na kukaribisha maisha hata katikati ya matatizo ya kijamii na kiuchumi pamoja na wasemaji wengine wa hafla hiyo ni Massimo Gandolfini na Maria Rachele Ruiu.
Matukio ya maandamano
Miongoni mwa maombi yaliyopendekezwa na Maandamano ya Kitaifa ya Uhai ni HAPANA kwa utamaduni wa kubagua na kwa kila vitendo vyovyote vinavyokiuka utu wa asili wa maisha ya mwanadamu, kuanzia na utoaji mimba, euthanasia, kusaidiwa kujiua na ghiliba au uharibifu wa viinitete kwa madhumuni ya uzalishaji.
Gandolfini: kila maisha yana hadhi ya ndani
Kwa mujibu wa daktari bingwa wa upasuaji wa neva kutoka Brescia na msemaji wa tukio hilo Massimo Gandolfini akizungumza na mwandishi Marco Guerra katika maikrofoni ya Radio Vatican - Vatican News, alisema: “Maandamano haya yanataka kuwa tofauti kabisa na utamaduni wa kifo kama Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili alivyoyaita na utamaduni wa kutupa kama Papa Francisko anavyoita, na wakati huo huo yanataka kukuza uzuri wa kufungua maisha, ndiyo maana itakuwa maandamano ya sherehe.” Rais wa Siku ya Familia kisha alizungumza juu ya msukumo uliopokelewa kutoka katika Hati ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, Dignitas Infinita, ambayo inafafanua kuwa yenye kuelimisha: “Hadhi ya maisha haina kikomo na haihitaji sifa zingine, kwa sababu kila kiumbe hai, tangu kutungwa mimba hadi kifo cha asili, ndiyo inabeba utu wa mwanadamu na hivyo lazima itambuliwe na kuheshimiwa.”
Kusaidia maisha ni kuamini katika siku zijazo
Gandolfini alikumbuka kwamba tamaduni za kutisha za nyakati hizi “zinatia sumu katika jamii zetu”, kwa mujibu wa msemaji wa tukio hilo moja ya matunda ya utamaduni huu ni kupungua kwa kiwango cha kuzaliwa ambacho kinaathiri Italia, kisha alizingatia kutupilia mbali wazee na wagonjwa na aliomba kwamba kusindikizwa kwa heshima hadi kifo na huduma shufaa ihakikishwe. Zaidi ya hayo, Dk. Gandolfini alisisitiza hitaji la kulinda uzazi na maisha kabla ya kuzaliwa kwa kutofautisha pia desturi zinazokiuka na kubadilisha maisha ya akina mama na watoto, kama vile uzazi wa kokodi. Hatimaye, Dk. Gandolfini alihimiza jamii na ulimwengu wa siasa kusaidia familia, kwa sababu “familia ni utoto unaokaribisha maisha na nafasi ya elimu ya kila mtu hadi mtu mzima licha ya matatizo yote ya kijamii yaliyopo". “Kutegemeza maisha na familia kunamaanisha kutegemeza manufaa ya wote na kuwa na tumaini changamfu la wakati ujao,” alihitimisha Dk. Gandolfini.