Kila mwaka tarehe 15 Juni ni Siku ya Kimataifa ya utambuzi wa mateso na kubaguliwa kwa wazee duniani. Kila mwaka tarehe 15 Juni ni Siku ya Kimataifa ya utambuzi wa mateso na kubaguliwa kwa wazee duniani.  (Vatican Media)

15 Juni ni Siku ya Kimataifa ya utambuzi wa unyanyasaji dhidi ya wazee!

Ni mara ngapi wazee wanabaguliwa kwa tabia za kuwaaacha na ambayo ni euthanasia ya halisi na kweli iliyofichwa!Ni ujumbe mfupi wa Papa katika mtandao wa kijamii wa Papa Francisko katika fursa ya Siku ya Kimafaifa ya uhamasishaji wa utambuzi wa unyanyasaji dhidi ya wazee ifanyikayo kila mwaka ifikapo tarehe 15 Juni ya kila mwaka.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tarehe 15 Juni ni siku iliyoteuliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika azimio lake 66/127, kuwa  ya (World Elder Abuse Awareness Day), Siku ya Uhamasishaji kuhusu unyanyasaji dhidi ya Wazee Duniani, ambayo ni siku ya kila mwaka ilyotambuliwa tangu mnamo 20211, ambapo ulimwengu unazidi kuonesha upinzani mkubwa wa unyanyasaji na mateso wanayofanyiwa wazee kila sehemu nyingi za dunia.  

Ujumbe wa Papa Francisko

Ni katika muktadha huo katika Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwenye mtandao wake wa kijamii tarehe 15 Juni 2024 anaandika kuwa: “Ni mara ngapi wazee wanabaguliwa kwa tabia za kuwaaacha na ambayo ni euthanasia  halisi na kweli iliyofichwa! Ni matokeo yake ya utamaduni wa kubagua ambao unafanya vibaya sana katika ulimwengu wetu. Sisi sote tunaitwa kupinga sumu hii ya utamaduni wa kubagua.” Kwa mujibu wa taarifa za waandaaji wa siku huu wanabainisha kuwa maadhimisho haya yanakusudia kuongeza ufahamu wa kimataifa wa jambo lisilokadiriwa na kubwa sana ambalo huathiri vizazi vya zamani. Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO)linafafanua unyanyasaji wa wazee kama “tendo lolote, moja au linalorudiwa, au kunyimwa hatua inayofaa, inayotokea ndani ya uhusiano wowote ambapo kuna matarajio ya kuaminiwa, na kusababisha madhara au dhiki kwa mtu mzee.”

Aina na matokeo ya unyanyasaji

Aina hii ya unyanyasaji, kulingana na WHO, inawakilisha ukiukaji wa haki za binadamu na inaweza kuwa ya kimwili, kingono, kisaikolojia na kihisia, kifedha, na inajumuisha uzembe. Matokeo kwa mwathirika ni mabaya, na kwa kiwango cha kisaikolojia, yanaweza kusababisha wazee kuingiza hisia za kukataliwa na kutengwa. Wanaweza kusababisha kupungua kwa uwezo wa kimwili na kiakili na, katika hali mbaya zaidi za unyanyasaji, hata kusababisha kifo. Dhana ya unyanyasaji wa wazee mara nyingi husababishwa na miktadha tofauti ya kitamaduni na kijamii ya nchi na njia za kukabiliana nayo - na viwango tofauti vya ufahamu na umakini kwa jambo hilo - hutofautiana sana katika kiwango cha kimataifa.

15 June 2024, 16:05