Mkutano wa G7 Italia. Mkutano wa G7 Italia.  (AFP or licensors)

Tamko la viongozi wa G7 kwa Afrika ni kuzindua G7 kwa ajili ya Nishati ya ukuaji wa Afrika

Wakati wa mkutano wa G7 uliofunguliwa tarehe 13 na kufungwa tarehe 15 Juni 2024 Viongozi hao wakianza na mada kuhusu bara la Afrika walitoa tamko:“Ili kufikia malengo na juhudi za kimataifa zilizoamuliwa katika kikao cha 5 cha Mkutano wa Nchi Wanachama zinazotumika kama Mkutano wa Nchi Wanachama katika Mkataba wa Paris(CMA5),tunatazamia kuzinduliwa kwa G7 ya Nishati kwa Ukuaji wa Afrika,mpango na kuchangia mafanikio yake.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika siku ya kwanza ya Mkutano wa Viongozi wakuu wa nchi (G7) wakiwa mgeni wa Nchi ya Italia uliofunguliwa tarehe 13 Juni na ambao umefungwa rasmi tarehe 15 Juni 2024 kati ya mada nyingi walijikita na mada ya majadiliano kuhusu Afrika, Ukraine na Mashariki ya Kati, lakini pia utata kuhusu utoaji wa  mimba ambao pia ulikuwa na nafasi kubwa ambapo kwa hakika  Waziri Mkuu Giorgia Meloni aliwakaribisha wakuu wa nchi na serikali za Canada, Ujerumani, Ufaransa, Japan, Uingereza na Marekani huko  Borgo Egnazia , Puglia katika jimbo la Brindisi. Na zaidi, Baba Mtakatifu aliwasili na kuhutubia na kukutana na viongozi kadhaa kwa mkutano mfupi. Baada ya mkutano kuhusu Afrika viongozi hawa wa G7 walitoa kauli moja    kuhusu Nishati kwa Ukuaji wa Afrika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alikuwa ni mgeni wa G7 na Rais wa Benko ya Maendeleo Afrika Akinwumi Adesina
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alikuwa ni mgeni wa G7 na Rais wa Benko ya Maendeleo Afrika Akinwumi Adesina

 

Ifuatayo ni tamko la viongozi hao: Sisi, wawakilishi wa Canada, Jamhuri ya Congo, Ivory Coast, Ethiopia, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Kenya, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, Uingereza, Marekani na Umoja wa Ulaya tunatambua kwamba upatikanaji kwa wote wa nishati safi ya bei nafuu ni jambo muhimu kwa ukuaji endelevu, uthabiti na shirikishi wa uchumi na maendeleo ya kijamii, kama ilivyotangazwa na Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika(UA). Pia unachangia kufikia malengo ya tabianchi ya Mkataba wa Paris na kuweka kikomo cha kufikia ndani ya halijoto 1.5C. Uwezo mkubwa wa nishati safi barani Afrika lakini ambao haujatumika unahitaji uwekezaji mkubwa. Tutafanya kazi ili kuharakisha uwekezaji katika vyanzo vya nishati safi ili kuhakikisha mabadiliko jumuishi ambayo yanaunga mkono usalama wa nishati, kwa kutambua kwamba idadi kubwa ya watu barani Afrika bado hawana upatikanaji wa umeme na upishi safi.

Rai wa Uturuki na Marekani wakisikiliza kwa makini hotuba ya Papa
Rai wa Uturuki na Marekani wakisikiliza kwa makini hotuba ya Papa

Ili kufikia malengo haya na juhudi za kimataifa zilizoamuliwa katika kikao cha 5 cha Mkutano wa Nchi Wanachama zinazotumika kama Mkutano wa Nchi Wanachama katika Mkataba wa Paris (CMA5), tunatazamia kuzinduliwa kwa G7 ya Nishati kwa Ukuaji wa Afrika,  mpango na kuchangia mafanikio yake. Mpango huo utasaidia kuendeleza miradi ya nishati safi inayoweza kulipwa, kuvutia mtaji wa kibinafsi kupitia matumizi ya kichocheo ya fedha za umma na usaidizi wa kiufundi, kuhimiza mtiririko wa fedha za masharti nafuu, na kuondokana na vikwazo kwa uwekezaji katika nishati safi Afrika yote.

Picha ya pamoja ya Papa na viongozi wa G7
Picha ya pamoja ya Papa na viongozi wa G7

Mpango huo utashirikiana na serikali, sekta ya kibinafsi, taasisi za fedha, benki za maendeleo za kimataifa na vikundi vya jamii. Itashirikiana na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati. Pia itaratibu na programu zilizopo, ili kuhakikisha ulinganifu na kuepuka kurudiwa, na itafanya kazi kwa uratibu wa karibu na Ushirikiano wa G7 wa Miundombinu na Uwekezaji wa Kimataifa.

15 June 2024, 15:03