Katibu Mkuu wa UN alitangaza mfumo wa pamoja wa kimataifa wenye uratibu wa pamoja ili kuhakikisha majukwaa ya taarifa au habari yanakuwa salama na ya kibinadamu. Katibu Mkuu wa UN alitangaza mfumo wa pamoja wa kimataifa wenye uratibu wa pamoja ili kuhakikisha majukwaa ya taarifa au habari yanakuwa salama na ya kibinadamu. 

UN yazindua mapendekezo ya kudhibiti madhara ya habari potofu na kauli za chuki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Guterres wakati wa uzinduzi wa Kanuni za Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Uadilifu wa Habari alisema:“Dunia inapaswa kuchukua hatua dhidi ya madhara yatokanayo na kusambaa kwa chuki na uongo mtandaoni huku ikizingatia vema haki za binadamu.”Habari za kughushi zimekuwa nyingi mno.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Akizungumza  jijini New York, Marekani, tarehe 24 Juni 2024  ikiwa ni mwaka mmoja tangu azindue ripoti yake kuhusu uadilifu wa Kanuni za Umoja wa Mataifa za uadilifu wa Habari kwenye majukwaa ya kidijitali, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Gutterres alitangaza mfumo wa pamoja wa kimataifa wenye uratibu wa pamoja ili kuhakikisha majukwaa ya taarifa au habari yanakuwa salama na ya kibinadamu, moja ya jukumu letu la dharura kwa sasa. Bwana Gutterres alisema habari potofu, habari za uongo, na kauli za chuki na hatari nyingine zitokazo kwenye mfumo wa habari vinachochea mizozo, vinatishia demokrasia na haki za binadamu, na vile vile vinagandamiza afya ya umma na hatua kwa tabianchi.

Nafasi ya Akili Mnemba kwenye habari potofu na za uongo

“Kuenea kwao hivi sasa kunachochewa kwa kasi kubwa na ongezeko la teknolojia za Akili Mnemba (AI) na hivyo kuongeza kitisho kwa makundi kwenye majukwaa ya habari, hasa watoto,” alisema Katibu Mkuu. Kwa njia hiyo alisema Kanuni za Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Uadilifu wa Habari zitajengea uwezo watu kudai haki zao,” na kuongeza kuwa: “katika wakati huu ambapo mabilioni ya watu wanakumbwa na taarifa za uongo na potofu, kanuni hizi zinaweka bayana njia iliyozingatia haki za binadamu, ikiwemo haki ya kujieleza na kutoa maoni.”

Hata hivyo kuhusiana na suala la Akili Mnemna, katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Siku ya Upashanaji Habari Ulimwenguni kwa Mwaka 2024 uliongozwa na kauli mbiu: “Akili Mnemba (AI) na Hekima ya Moyo: Kuelekea katika Mawasiliano Imara ya Mwanadamu.” Kauli mbiu hiyo imekuwa  ni mwendelezo wa ujumbe wa Papa  aliutoa katika maadhimisho ya Siku ya Kuombea Amani Ulimwenguni kwa  2024 ambapo alikazia kuhusu maendeleo ya mifumo ya akili Mnemba, yanavyoathiri ulimwengu wa mawasiliano. Na akizungumza na Wakuu wa Mataifa 7 yaliyoendelea duniani kiviwanda(G7), alikazia vile vile juu ya Akili Mnemba.

Kuna maborehso ya kiteknolojia lakini yafuate vigezo

Na zaidi akigusia Teknolojia ya siku zijazo alibanisha wazi juu ya uwepo maboresho makubwa katika maisha ya watu kutokana na kuboreka kwa njia za mawasiliano, huduma kwa umma, elimu pamoja na ongezeko la ulaji; mwingiliano na mafunagamano ya kijamii, mambo yanayojionesha katika uhalisia wa kila siku ya maisha ya watu. Lakini kuna haja ya kufahamu kwa kina maana ya sayansi na teknolojia pamoja na athari zake kwa binadamu. Kutokana na hili teknolojia ya akili Mnemo lazima izingatie kati ya mambo yafuatayo: Iwe ni shirikishi, inayotekelezeka kwa misingi ya ukweli na uwazi; usalama, usawa, pamoja na kulinda siri za watu na kwamba, teknolojia ya akili  mnemba au bandia, iwe inategemewa. Kuwepo na chombo kitakachodhibiti masuala ya maadili, haki msingi za watumiaji na waathirika. 

Je kuna haki ya kuita Akili mnemba kwa kitu ambacho si kweli ?

Hata hivyo pia hivi karibuni akizungumza tena na Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa, ulioandaliwa na Mfuko wa Centesimus Annus Pro Potentefice, Papa  Francisko aliwaachia cahngamoto ya swali la kujiuliza kuhusiana na suala la Akili mnemba kwamba: “Je, tuna uhakika kwamba tunapaswa kuendelea kuita “Yenye akili”, kitu ambacho si kweli?... Hebu tutafakari na tujiulize ikiwa matumizi yasiyofaa ya neno hili kiukweli ni muhimu, ipasavyo kwa “binadamu”, au tayari tunajisalimisha kwa nguvu za kiteknolojia!” (Hotuba kwa washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Centesimus Annus 22 Juni 2024).

Serikali na kampuni ziwajibike kwa kuenea kwa maudhui yenye madhara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aidha amesihi serikali zote, kampuni za teknolojia, watu wa matangazo na tasnia ya uhusiano wa umma kuchukua hatua na kuwajibika kwa kuenea na utozaji wa fedha kwenye maudhui yanayosababisha madhara.Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa UN alisema malengo, operesheni na vipaumbele vya Umoja wa Mataifa vinaharibiwa na mmomonyoko wa uadilifu wa taarifa, ikiwemo juhudi muhimu za ulinzi wa amani na za kiutu. Utafiti uliofanywa kwa watumishi wa Umoja wa Mataifa, asilimia 80 ya walioshiriki walisema taarifa hatarishi zinatishia usalama wao na wa jamii inazowahudumia.

Kanuni zinatokana na nini?

Kanuni hizo ni matokeo ya mashauriano mapana na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, sekta binafsi, viongozi vijana, vyombo vya habari, wanazuoni na mashirika ya kiraia. Mapendekezo yaliyomo yameundwa kuchochea majukwaa ya taarifa yaliyo salama, yanayososngesha haki za binadamu, jamii zenye amani na mustakabali endelevu.

Serikali zihakikishe wananchi wana vyanzo vya uhakika vya taarifa

Mapendekezo hayo ni pamoja na serikali, kampuni za teknolojia, kampuni za matangazo, vyombo vya habar, na wadau wengine wajiepushe na kutumia, kuunga mkono au kupazia sauti taarifa za uongo na kauli za chuki kwa lengo lolote lile. Serikali zihakikishe wananchi wao wanapata taarifa kwa wakati, na raia wawe na uhakika wa kupata vyombo vya habari vya uhakika, huru na wakati huo huo ihakikishe ulinzi thabiti kwa waandishi wa habari, watafiti na mashirika ya kiraia.

Kampuni za teknolojia zilinde wanaolengwa mitandaoni

Kwa upande wao kampuni za teknolojia zihakikishe usalama na faragha kwa kuunda bidhaa zinazozingatia sera za kuwalinda hasa makundi yanayolengwa mtandaoni. Vile vile Kampuni ziongeze hatua zao za kusaidia uadilifu wa taarifa hasa wakati wa uchaguzi. Wadau wote wanaohusika na uendelezaji wa teknolojia za Akili Mnemba wanapaswa kuchukua hatua za dharura, za wazi na jumuishi kuhakikisha teknolojia zote za Akili Mnemba zinazotolewa, zinazobuniwa zinatumika kwa usalama, zinazingatia maadili na haki za binadamu.

25 June 2024, 15:21