Watoto milioni 400 duniani kote hukumbana na adhabu kali nyumbani mara kwa mara
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Bi Catherine Russell akizungumza kutoka Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani alisema: “Takriban watoto milioni 400 chini ya umri wa miaka 5 au 6 kati ya watoto 10 (katika kundi hilo la umri duniani kote), hukumbwa na ukatili wa kisaikolojia au adhabu ya kimwili mara kwa mara wakiwa nyumbani. Kati yao, takriban milioni 330 wanaadhibiwa kwa njia za kimwili kulingana makadirio mapya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF.” Takwimu mpya pia zinaonesha kuwa watoto wengi wadogo hunyimwa fursa ya kucheza, ili kuchochea akili na kuwa na uhusiano bora na wazazi na walezi wao. Matokeo haya pia yanasisitiza mchango muhimu wa kucheza katika ukuaji wa watoto na afya ya akili ya watoto, wazazi, na walezi ikilinganishwa na takwimu zinazoonesha hali ya upungufu wa malezi bora, ikiwa ni pamoja na kuchochea akili na mwingiliano nyumbani.
Aidha: “Watoto wanapokumbana na unyanyasaji wa kimwili au wa maneno nyumbani, au wanaponyimwa huduma za kijamii na za kihisia kutoka kwa wapendwa wao, inaweza kudhoofisha hisia zao za kujithamini na ukuzi,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell na kuongeza kuwa: “Malezi yenye upendo na michezo yanaweza kuleta furaha na pia kuwasaidia watoto kujisikia salama, kujifunza, kujenga ujuzi, na kudhibiti maswala tofauti maishani mwao.” Nchi nyingi zaidi zinapiga marufuku adhabu ya kimwili dhidi ya watoto nyumbani. Zaidi ya nusu ya nchi 66 ambazo zimepiga marufuku utaratibu huo zimepitisha sheria ndani ya miaka 15 iliyopita, lakini hii bado inaacha takriban watoto nusu bilioni chini ya umri wa miaka 5 bila ulinzi wa kutosha wa kisheria. Duniani kote, mila potofu zinazounga mkono mbinu za malezi za ukatili bado zipo. Kulingana na utafiti zaidi ya 1 kati ya akina mama na walezi wa msingi 4 wanasema kwamba adhabu ya kimwili ni muhimu kwa kulea na kuelimisha watoto ipasavyo.
Takwimu zilizotolewa kwa mara ya kwanza kwenye Siku ya Kimataifa ya Michezo zinaonesha tofauti katika mbinu za malezi na upatikanaji wa fursa za kucheza. Kwa mfano, makadirio mapya yanaonesha kuwa karibu watoto 4 kati ya 10 wenye umri wa miaka 2-4 hawapati mwingiliano au kuchochewa akili vya kutosha nyumbani. Hii inamaanisha kwamba wanaweza kukumbana na kujihisi kupuuzwa kihisia na hali ya kujitenga, kutojiamini, na changamoto za kitabia ambazo zinaweza kuendelea hadi utu uzima. Wakati huo huo, mmoja kati ya 10 anakosa kushiriki katika shughuli na walezi wao ambazo ni muhimu kwa kukumza kiakili, kijamii, na kihisia, kama kusoma, kusimulia hadithi, kuimba, na kuchora. Takwimu pia zinaonesha kuwa karibu mmoja kati ya watoto 5 wenye umri wa miaka 2-4 hawachezi na walezi wao nyumbani, wakati karibu mmoja kati ya 8 chini ya umri wa miaka 5 hawana vifaa vya kuchezea nyumbani.
Utafiti unaoneesha kwamba mipangilio ya malezi inayotegemea matokeo ya tafiti inaboresha malezi; Halikadhalika, inapunguza ukatili na unyanyasaji kwenye familia, na kuimarisha afya ya akili ya watoto na wazazi. Mipangilio hii inajumuisha mafunzo ya mtazamo chanya, kujenga mahusiano thabiti kati ya mzazi na mtoto, na kuchangia katika michezo, nidhamu isiyo ya kikatili, na mawasiliano. Ili kuhakikisha kila mtoto anakua akijisikia salama na kupendwa, UNICEF imetoa wito kwa serikali kuimarisha juhudi na uwekezaji katika mambo haya:
Ulinzi: Kuimarisha mifumo ya kisheria na sera zinazopiga marufuku na kumaliza aina zote za ukatili dhidi ya watoto nyumbani;
Msaada wa malezi: Kupanua mipangilio ya malezi inayotegemea utafiti, ambayo hukuza mitazamo chanya ya michezo, na kuzuia ukatili katika familia; Kujifunza kupitia michezo ya: Kupanua upatikanaji wa maeneo ya kujifunza na michezo kwa watoto, ikiwa ni pamoja na chekechea, shule, na viwanja vya michezo. “Katika Siku ya Kimataifa ya Michezo kwa mara ya kwanza, lazima tuungane na kujitolea tena kumaliza ukatili dhidi ya watoto na kukuza malezi chanya, yenye upendo, na ya michezo,” alisisitiza Russell.