Jubilei,barabara ya chini katika Uwanja wa Pia inaanza kuona mwanga!
Alessandro Guarasci na Angella Rwezaula – Vatican.
Kazi ya maandalizi kwa ajili ya Jubilei ya 2025 inaendelea kwa kasi kubwa jijini Roma ambapo Jumatano tarehe 17 Julai 2024 wameonesha matokeo muhimu yaliyopatikana hadi sasa ya matengenezo ya barabara ya chini ya Uwanja wa Pia, mbele ya Makao Makuu ya Radio Vatican mjini Vatican. Kiukweli sehemu ya mwisho iliyokuwa inaunganisha kipande cha chini katika Handaki Mpya na ya zamani imebomolewa katika baraba ya Conciliazione.
Gualtieri:kazi ya kubadilisha eneo karibu na Mtakatifu Pietro
Kazi hiyo inagharimu milioni 85 na itafanya njia yote ya Conciliazione kuwa ya kutembea kwa miguu kabisa, kwa hiyo mahujaji wataweza kutembea kutoka Castel Sant’Angelo hadi Uwanja wa Mtakatifu Pietro. Hii ni hatua ya msingi katika mtazamo wa Mwaka Mtakatifu, kwa usahihi kuruhusu ufikiaji rahisi wa Mlango Mtakatifu na kaburi la mtume Petro. Kwa meya wa Roma, Bwana Roberto Gualtieri, alisisitiza kuwa “hili ni eneo lakutia rekodi ya ujenzi, hata tulibomoa Daraja la Genova. Kazi tuliifungua mwezi Agosti mwaka jana na lengo ni kuifunga mwezi Desemba”, alisema Meya wa Mji. Dhamira yetu ni kubadilisha Roma na tunahitaji tiba ya mshtuko.” Kwa upade Meya wa mji hata hivyo, alisema mji mkuu unahitaji euro bilioni 20 nyingine ili kuboresha miundombinu yake.
Miundombinu ya kisasa na matokeo yanaweza kuwepo pamoja
Kimsingi, inahusisha kupanua njia ya chini ya sasa kando ya Tiber huko Sassia kwa takriban mita 130, kuanzia Njia ya Borgo. Kazi hizo zilihusisha ucheleweshaji kidiogo kutokana na kubadilisha mkondo wa maji taka ya Roma Kaskazini na vile vile wakati wa kuchimba walikutana na magaofu ya kirumi na jengo za wakati wa Caligula. Matokeo hayo ya magofu yamehamishwa na yatapelekwa kwenye bustani za Castel Sant'Angelo,zitakazotengenezwa ambapo maonesho ya wazi kwa umma yataanzishwa.
Rocca:Vyumba vya dharura vya Roma vilikarabatiwa kwa Jubilei
Katika uzinduzi huo alishiriki hata Askofu mkuu Salvatore Rino Fisichella, Mwenyekiti mwenza, wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, ambaye alishuhudia hata tukio la handaki mbili zilizobomolewa na kuunganishwa.
Milioni 155 za euro nyingine zimewekezwa kukarabati vyumba vya dharura jijini Roma, alisema rais wa eneo la Mkoa wa Lazio, Francesco Rocca, ambaye alihakikisha kuwa kazi hiyo itakamilika na Jubilei. Hii pia inatumika kwa eneo la pembeni mwa Tiber, ambapo ni wajibu mwingine wa Mkoa wa Lazio. Kwa ajili ya Jubilei, kama walivyosema Waziri wa Miundombinu, Italia Bwana Salvini na Meya Gualtieri, walisema kuna uthibitisho wa uwajibikaji na ushirikiano mkubwa wa kitaasisi, ambao lengo ni moja na taasisi zote zinafanya kazi bega kwa bega na kwa pamoja.
Salvini:Uwanja wa Pia unaonesha thamani ya uhandisi wetu
Waziri wa Miundombinu, wa Italia, Bwana Matteo Salvini, pia alitaka kusisitiza thamani ya kazi hii kwa ajili ya Jubilee ya 2025 ambayo, alisema, inaonesha uwezo wa uhandisi wa Italia. “Tunakimbia kufidia ucheleweshaji uliokusanywa hapo awali, tutafika kwa wakati kwa ajili ya Jubilei na Olimpiki. Mahali pa ujenzi wa leo ni eneo ambalo wengi walilitazama kwa mashaka mwaka mmoja uliopita na ambalo sasa litakuwa mwenyeji wa Waroma na mahujaji kabla ya Noeli kwa urahisi na uzuri tofauti.” Kuhusu ombi la fedha zaidi kwa ajili ya mji mkuu, lililotolewa na meya Gualtieri, Salvini alijibu kwamba serikali inajaribu kufanya kile 'kinachowezekana'."