Tafuta

Magazeti yote duniani yanaeleza juu ya Rais Biden. Magazeti yote duniani yanaeleza juu ya Rais Biden.  (CAITLIN OCHS)

Marekani:Joe Biden anaondoka kwenye kinyang'anyiro cha urais

Kuarasa za kwanza za habari kimataifa zimeelezea kujiondoa kwa rais katika kampeni za uchaguzi wa Ikulu ya Marekani,baada ya juma za shinikizo kutoka kwa Chama cha Kidemokrasia.Sasa uchaguzi wa mgombea mpya wa Kidemokrasia unafunguliwa na atalazimika kusimama na Trump katika uchaguzi wa Novemba 5:Kama Harris,makamu rais,yuko mbioni,lakini yote hayo yataonekana.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Uamuzi uliotarajiwa lakini ambao bado umekuwa wa kustaajabisha wa Joe Biden,Rais wa Marekani ambao umekuja baada ya ushauri wa chama chake kujiondoa kufuatia na kura zinazozidi kuwa mbaya kufuatia mkutano wake wa ana kwa ana na Donald Trump kwenye televisheni. Biden mwenyewe alitangaza hilo katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, huku akisema kwamba atasalia katika Ikulu hadi mwisho wa muhula wake. Lakini hata uwezekano huo unapingwa na mikondo ya Chama cha Kidemokrasia, kinachoelekeza hatua ya kurudi nyuma mara moja na rais. Hii ingetoa jukumu na mwonekano, katika miezi hii ya mwisho ya ofisi, kwa Makamu wa Rais Bi Kamala Harris, ambaye tayari ameelekezwa na Biden kama mgombea anayewezekana kukabiliana na Trump.

Mgombea mpya

Kwa hivyo, Chama cha Demokrasia sasa kiko na harakati sasa za kuchagua mgombea mpya ambacho kwa uhakika kitazingatia zaidi. Na ni kwa uhakika huo kwamba watu wa Kidemokrasia wataamua wakati wa mchujo ambao utalazimika kufanywa kwa wakati wa rekodi. Wakati huo huo, kujiondoa kwa  Rais Biden kumetoa msukumo mpya wa kampeni ya uchaguzi wa Kidemokrasia. Katika saa massa chache tu, michango ya karibu dola milioni 50 ilifika kwa haraka wa mwisho wa mwisho usio na kifani: ushahidi zaidi wa uthabiti wa wapiga kura wa Marekani.

Majibu

Rais Joe Biden hata hivyo anaendelea kupokea shukrani za chama chake kwa kuitawala nchi katika hali ngumu ya ndani na kimataifa ya miaka ya hivi karibuni. Wakati huo huo na kutoka nje ya nchi, miongoni mwa wengine, viongozi wa Urusi wanasema wanaendelea kufuatilia maendeleo katika mchakato wa uchaguzi wa Marekani, lakini bila kuingiliwa. Kutoka kwa rais wa Ukraine, Volodomyr Zelensky, ameshukuru kutambuliwa kwa  Biden kwa kile alichokifanya kwa niaba ya Kyiv wakati wa vita na Urusi na hitaji lililotangazwa la msaada wa Amerika kuendelea. Nchi zingine nyingi zinatambua jukumu la msingi alilokabiliana nalo Biden na kuelewa chaguo ngumu alilofanya kujiuzulu. Na Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia, Waziri Antonio Tajani, alisisitiza kuwa: “Roma itaendelea kufanya kazi vizuri pia na rais ajaye wa Marekani. Hata hivyo wakati majibu kutoka ulimwengu wa kifedha umekuwa ni ya kutatanisha,wakati dhahabu ikipanda sana, lakini masoko ya hisa yanashuka.

22 July 2024, 16:51