Marekani,Biden:mkataba wa mfumo ulioidhinishwa na Israel na Hamas
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Bado kuna kazi ya kufanywa, lakini Israel na Hamas wameidhinisha mpango uliowasilishwa Majuma sita yaliyopita na Joe Biden, Rais wa Marekani wa kusitisha mapigano na kuwarudisha nyumbani mateka wa Israel ambao bado wanazuiliwa huko Gaza.
Mazungumzo ya Cairo
Ni rais wa Marekani mwenyewe ndiye aliyeitangaza kwenye mitandao yake ya kijamii. Baada ya Doha, Cairo kwa sasa ni mwenyeji wa mazungumzo chini ya uangalizi wa Marekani, Misri na Qatar. Mazungumzo hayo yanaripotiwa kujadili mfumo wa uchunguzi wa kielektroniki kati ya Gaza na Misri ambao unaweza kuiruhusu Israel kuondoa wanajeshi wake katika eneo la mpaka. Suala la kudumu kwa vikosi vya Israel kwenye mpaka ni moja ya masuala muhimu ya majadiliano, lakini ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel imefahamisha kuwa Benjamin Netanyahu alisisitiza ombi la kudumisha udhibiti wa eneo hilo, kuepusha kutumwa tena kwa jeshi. ambao kwa hiyo wangebaki kwenye “ukanda wa Philadelphia”.
Kurejesha mateka
Hoja nyingine ya mazungumzo bado ni kurejea kwa wanachama wa Hamas kaskazini mwa Gaza. Netanyahu pia anasemekana kupinga suala hili la mwisho, kwa mujibu wa gazeti la Times of Israel linaripoti, kwa upande wake akinukuu Channel 12. Familia za zaidi ya mateka 100 wa Israel mikononi mwa Hamas kwa mara nyingine tena zilisimama katika suala hili, na kukosoa usimamizi wa mazungumzo na Netanyahu.
Watu 71 kuuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa
Wakati huo huo, taariza za Palestina zinaripoti kuwa, watu 71 wameuawa na zaidi ya 100 wamejeruhiwa katika shambulio kubwa la wanajeshi wa Israel katika eneo la Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza. “Haaretz” inaripoti kwamba hakuna taarifa fulani juu ya hatima ya mkuu wa tawi la kijeshi la Hamas, Mohammed Deif, ambaye angekuwa mlengwa wa uvamizi huo. Kulingana na baadhi ya vyombo vya habari vya Saudia, Deif - aliyeonyeshwa na wengi kama mpangaji mkuu wa shambulio la Oktoba 7 - yuko katika hali mbaya, wakati Rafa Salameh, kamanda wa kikosi cha Khan Yunis cha wanamgambo, ambaye alikuwa pamoja naye, ameuawa.
Wafanyakazi 4 wa kibadamu wa kipatestina walikufa kwenye shambulizi la bomu
Wafanyakazi wanne wa kibinadamu wa Kipalestina badala yake walikufa chini ya shambulio jingine la bomu katika Ukanda huo: wanaongeza wafanyakazi 194 wa UNRWA waliouawa katika mzozo huo, uliokumbukwa tarehe 12 Julai mjini New York na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres, mwishoni mwa mkutano wa wafadhili ambapo nchi 118 zilitia saini ahadi ya kuimarisha msaada wa kifedha na kisiasa kwa shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi wa Kipalestina.