shughuli za kutoa miili mingi inaendelea kutoka kwenye vifusi vya shule iliyoporomoka katikati mwa Nigeria. shughuli za kutoa miili mingi inaendelea kutoka kwenye vifusi vya shule iliyoporomoka katikati mwa Nigeria. 

Nigeria:hadi sasa ni watoto 22 waliokufa katika shule iliyoanguka

Takwimu hadi sasa ni watoto ishirini na mbili waliokufa kutokana na kuanguka kwa shule moja nchini Nigeria Sababu zilizosababisha kuanguka kwa jengo hilo bado hazijajulikana lakini ni katika eneo ambalo lilikuwa limeathiriwa na mvua kubwa katika siku za hivi karibuni.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Idadi ya vifo iliyosababishwa na kuporomoka kwa shule ya orofa mbili kaskazini-kati mwa Nigeria siku ya Ijumaa tarehe 12 Julai 2024 asubuhi kwa sasa imefikia watu 22. Kituo kinachozungumziwa ni chuo cha Watakatifu wa Elimu katika Jumuiya ya Busa Buji katika Serikali ya  Plateau, ambacho kiliripotiwa kuanguka muda mfupi baada ya kuingia kwa wanafunzi hao darasani, ambao wengi wao walikuwa na umri wa miaka 15 au chini yake. Mbali na waathiriwa pia kuna karibu  watoto 70 waliojeruhiwa. Idadi  hata hivyo, bado ni wa muda na kuna hofu kwamba inaweza kuongezeka zaidi kwani bado shughuli ya kutafuta katika vifusi zinaendelea.

Shughuli za kuchimbua kweny vifusi zinaendelea
Shughuli za kuchimbua kweny vifusi zinaendelea

Uokoaji bado unaendelea kutoka katika vifusi

Jumla ya wanafunzi 154 awali walinaswa chini ya vifusi, na hivyo kusababisha msako mkali wa kuwatafuta manusura. Msemaji wa polisi wa Plateau Alfred Alabo, baadaye alisema kuwa 132 kati yao waliokolewa na kusafirishwa hadi hospitali mbalimbali za mitaa, huku 22 wakiwa wamekufa.

Shule zenye majengo kama hayo lazima zifungwe

Sababu zilizosababisha kuanguka kwa jengo hilo bado hazijajulikana, lakini eneo ni ambalo lilikuwa limeathiriwa na mvua kubwa katika siku za hivi karibuni. Serikali ya eneo hilo pia ilihusisha tukio hilo kama “muundo dhaifu wa shule na eneo karibu na ukingo wa mto, ikitaka majengo mengine ya shule yenye matatizo sawa na hizo zifungwe.”

Watoto 22 wamekufa katika shule iliyoanguka nchini Nigeria
Watoto 22 wamekufa katika shule iliyoanguka nchini Nigeria
13 July 2024, 15:37