Tafuta

24.07.2024:Rais Luiz Inacio Lula da Silva akizungumza wakati wa uzinduzi wa kqmpeni ya kupambana na njaa na umaskini katika G20 huko Rio de Janeiro,Brazil.Kwanza FAO iliwakilisha Ripoti ya  kila mwaka(SOFI.) 24.07.2024:Rais Luiz Inacio Lula da Silva akizungumza wakati wa uzinduzi wa kqmpeni ya kupambana na njaa na umaskini katika G20 huko Rio de Janeiro,Brazil.Kwanza FAO iliwakilisha Ripoti ya kila mwaka(SOFI.)  (AFP or licensors)

Ripoti ya SOFI 2024:Tutakuwa na watu milioni 582 wa utapiamlo au njaa ifikapo 2030!

Takriban watu milioni 733 walikabiliwa na njaa mnamo 2023,sawa na mtu mmoja kati ya kumi na moja.Hayo yemeripotiwa na Wataalamu wa FAO kuhusu ripoti ya Hali ya Usalama wa Chakula na Lishe Duniani(SOFI) ya 2024."Jambo la kusikitisha kwa mwaka 2024 unaonesha idadi haijabadilika tangu miaka iliyopita,ambayo tayari ilikuwa imeonekana kuongezeka njaa ulimwenguni kwa sababu ya UVIK-19.”

Na Agella Rwezaula – Vatican.

Takriban watu milioni 733 walikabiliwa na njaa mwaka 2023, sawa na mtu mmoja kati ya kumi na moja duniani, kulingana na ripoti ya Hali ya Usalama wa Chakula na Lishe Duniani kwa kifupi (SOFI), kwa 2024 ambayo imetolewa na Wataalamu wa FAO. Takwimu hizi ni za juu kwa  miaka mitatu mfululizo. Dunia imerudishwa nyuma kwa miaka 15, huku viwango vya utapiamlo vikilinganishwa na vile vya mwaka 2008-2009, vikiwa vimepungua kwa kiasi kikubwa kufikia Lengo la Maendeleo Endelevu(SDG)  Njiaa Zero, ifikapo 2030, kwa mujibu wa  SOFI. Upatikanaji wa chakula cha kutosha bado ni vigumu kwa mabilioni na ikiwa mwelekeo wa sasa utaendelea, takriban watu milioni 582 watakuwa na utapiamlo wa kudumu mwaka 2030, nusu yao wakiwa barani Afrika kwa mujibu wa onyo ya ripoti ya Umoja wa Mataifa.

1.Ripoti ya Fao(SOFI)

Ripoti ya SOFI ambayo kila mwaka hutoa idadi ya njaa duniani na hali ya viashiria vya usalama wa chakula na lishe duniani inabainisha kuwa, cha kusikitisha, mwaka 2024  “inaonesha  idadi haijabadilika kutoka miaka iliyopita, ambayo kimsingi  tayari ilikuwa miaka  inayoonekana kuongezeka njaa ulimwenguni kwa sababu ya UVIK-19.” Kwa hivyo kinachoripotiwa mwaka huu ni kwamba “watu kati ya milioni 713 na milioni 757 ni ambao wana utapiamlo kwa muda mrefu, watu wanaokabiliwa na njaa. Na hii ni mmoja kati ya watu 11 duniani wanaokabiliwa na njaa. Hali si kama tulivyopenda, lakini kwa tofauti kubwa katika kanda, Afrika ikiwa eneo ambalo limeathiriwa zaidi, na Amerika ya Kusini, hasa Amerika ya Kusini, kuwa eneo ambalo limeimarika zaidi.”

2.Afrika na Fedha

Kwa mujibu wa ripoti hiyo inabainisha kuwa “Tukilinganisha Afrika na Amerika Kusini, tofauti tunazoziona ni kwamba Amerika Kusini hutumia kiasi kikubwa cha pesa zao katika mipango ya hifadhi ya jamii. Amerika Kusini imeanzisha programu za ulinzi wa kijamii ambazo huwaruhusu kulenga sulihisho, ili waweze kuondokana na njaa kwa njia ya haraka sana, kwa sababu ni bora. Kwa upande wa Afrika, hatujaona hilo. Lakini kwa upande mwingine, Afrika ni eneo ambalo limeathiriwa zaidi na migogoro na (mabadiliko ya tabianchi), na bila shaka na mdororo wa kiuchumi. Ni eneo ambalo leo hii linaonesha idadi kubwa zaidi ya nchi katika mgogoro wa chakula kwa sababu ya vichochezi hivi vitatu muhimu, na migogoro ikiwa ya kwanza kwa maana hii, ikifuatiwa na hali ya hewa na kupungua na kushuka. Pia ni eneo ambalo leo hii linakabiliwa na changamoto kubwa za kifedha, ikimaanisha upatikanaji wa fedha, kwa sababu nchi nyingi za ukanda huo zinakabiliwa na hali ya madeni, ambayo hayaruhusu kuwa na rasilimali za kuweza kufanya sera ambazo tunahitaji kuweka ili kuongeza kasi ya kupunguza njaa duniani.”

3.Maendeleo Amerika Kusini

Ripoti ya SOFI aidha inabainisha kuwa “Bila shaka, kuwekeza katika hifadhi ya jamii ni mojawapo ya mambo ambayo tunahitaji kujifunza kutoka Amerika ya Kusini, hasa Amerika Kusini. Brazili ina mfumo mzuri sana wa ulinzi wa kijamii unaotumika… Colombia, Peru, Chile… Hiyo inawaruhusu kuguswa haraka na mabadiliko na kulenga haraka rasilimali za kifedha walizonazo, kwa sababu sisi sote tunakabiliwa na mkazo katika suala la ukata na rasilimali za kifedha. Lakini ikiwa una ufanisi katika njia unayofanya, utalenga idadi ya watu ambayo iko katika hali mbaya zaidi. Pia ni eneo ambalo limekuwa likipata nafuu haraka sana kutoka kwa UVIKO - 19 ikilinganishwa na maeneo mengine ulimwenguni, na hii ndiyo sababu tunaona mabadiliko haya muhimu.  Katika bara la Amerika ya Kusini, tunazungumza juu ya zaidi ya watu milioni 5 ambao wameondolewa na njaa katika miaka mitatu iliyopita.”

4.Lishe, utapiamlo na unene kuzidi kiasi

POFI inatbitisha kuwa “Tunapoangalia uhaba wa chakula, hatuangalii njaa tu, ambayo ni utapiamlo wa kudumu, bali pia tunaangalia uzito uliopitiliza na unene kupita kiasi. Umuhimu wa uwezo wa kumudu mlo wenye afya ni kwamba ni chakula ambacho ni tofauti na huleta mtazamo na lishe yote tunayohitaji, ili tuweze kuepuka matatizo ya utapiamlo wa muda mrefu, lakini pia tunaweza kuepuka matatizo ya kunenepa kuzidi kiasi. Leo hii tuna watu bilioni 2.8 ambao hawawezi kufikia gharama ya chini ya lishe bora. Idadi ni kubwa mno, haijaimarika ikilinganishwa na miaka iliyopita, na hiyo inatuambia kwamba tunahitaji kufanya mengi hapa. Inabidi tubadilishe dhana hii, kwanini nchi zina bei ya juu sana ambayo hairuhusu watu kutumia, na kwanini mapato ni shida, kwa sababu sio suala la upande wa usambazaji tu, bali pia ni suala la mapato. upande.

5.Mkwamo wa lengo kwa 2030 wa kufikia njaa Sufuri 

Ripoti inabanisha kwamba: “Tunachojua ni kwamba, ikiwa tutaonesha idadi ya leo, tutakuwa na hadi watu milioni 582 wenye utapiamlo au njaa ifikapo 2030.  Hii ni zaidi ya kile kilicholengwa, ambacho ni njaa sifuri, kwa hivyo tunahitaji kuharakisha mchakato na tunahitaji kubadilika ikiwa tunataka kuwa karibu iwezekanavyo kwa lengo letu. Tumebakiza miaka sita tu.”

25 July 2024, 15:26