Shambulizi,Trump,Vatican,maaskofu&Biden:kuumia demokrasia na hakuna vurugu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jinamizi la Amerika, kwa marais ambapo katika kesi hii wa zamani lakini tena katika mbio ambayo inaishia kwenye macho ya wale wanaotaka kuwaondoa. Wakati huu ilikuwa ni zamu ya Donald Trump, ambapo kwake ilikuwa kama mchezo wa kuigiza wa karibu, na kusababisha jeraha kwenye sikio lake la kulia, lakini ambalo linaumiza dhamiri ya nchi inayojiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa rais mnamo Novemba mwaka huu katika hali iliyochafuliwa zaidi.
Vatican: sababu za jeuri lazima zishinde
Hali ambayo pia imetia wasiwasi Vatican ambapo asubuhi ya tarehe 14 Julai 2024, katika kujibu maswali ya waandishi wa habari, kwenye Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Msemaji wake aliripoti kwamba “ tukio la jana jioni la vurugu linaumiza watu na demokrasia, na kusababisha mateso na kifo.” Pamoja na Maaskofu wa Marekani, ujumbe mfupi ulihitimishwa, “Vatican inaombea Marekani, waathiriwa na amani ya nchi, ili sababu za vurugu zisiwe na nguvu.”
Shambulio dhidi ya Trump
Trump alikuwa Butler saa kumi na mbili jioni (12.00) saa za Pennsylvania nchini Marekani kwa ajili ya mkutano, akiwa amezingirwa na umati wa watu. Majira ya saa 12:20 baadhi ya milio mikali ilisikika hewani, picha hizo zikimuonesha rais huyo wa zamani akiweka mkono sikioni na kisha kujitupa chini ya jukwaa huku wanaume wa kikosi cha usalama wakikimbilia kumkinga na huku mayowe ya hofu yakiinuka kutoka katika umati. Kwa bahati mbaya, kulikuwa na kifo kimoja na majeruhi wawili kati ya umma. Trump alisaidiwa kusimama muda mfupi baadaye, upande mmoja wa uso wake umejaa damu na kabla ya kusindikizwa alipata fursa ya kupiga kelele: “ Pambana mara tatu!” akiinua ngumi yake ya kulia. Risasi hizo zilitoka kwenye paa la jengo ambalo si mbali, ambapo, kijana mwenye umri wa miaka 20 aitwaye Thomas Matthew Crooks, alikuwa amejiweka na bunduki, akikwepa udhibiti na ambapo alikumbana na kifo chake mikononi mwa maafisa wa usalama.
Biden:Hakuna nafasi kama hiyo huko MMarekani
Rais Joe Biden wa Marekani, ambaye baadaye alimpigia simu Trump kufahamu hali yake, alilaani shambulizi hilo kwa maandishi kwenye aacount yake X kuwa: “Hakuna mahali pa vurugu za aina hii Amerika. Ni lazima tuungane kama taifa kulaani,” aliandika, wakati wimbi la maoni nchini Marekani na katika jumuiya ya kimataifa linakuwa kundi la watu kutoidhinishwa kila saa.
Kanisa la Marekani: vuguzu hazisaidii katika siasa
Kufuatia na taarifa za kupigwa risasi kwenye mkutano wa kisiasa uliomhusisha Rais wa zamani Donald Trump tarehe 12 Julai 2024 Jioni,, Askofu Mkuu Timothy P. Broglio wa Jimbo Kuu la Huduma za Kijeshi, Marekani na rais wa Baraza la Maaskofu wa Marekani(USCCB) wametoa tamko lifuatalo kuwa: “Pamoja na ndugu zangu maaskofu, tunalaani ghasia za kisiasa, na tunatoa maombi yetu kwa ajili ya Rais Trump, na wale waliouawa au kujeruhiwa. Pia tunaiombea nchi yetu na kukomeshwa kwa ghasia za kisiasa, ambazo kamwe si suluhisho la mizozo ya kisiasa. Rais wa Maaskofu Marekani aidha aliongeza kusema kuwa: “Tunawaomba watu wote wenye mapenzi mema kuungana nasi katika kuiombea nchi yetu amani. Maria, Mama wa Mungu na Mlinzi wa Marekani utuombee.” Hata hivyo mapema katika kiangazi hiki, Baraza la Maaskofu Marekani(USCCB)lilitoa tamko kuhusu ghasia za kisiasa, likiwataka Wakristo wote na watu wenye mapenzi mema kujiepusha na vurugu za kisiasa, na badala yake, ‘wafuate yale yanayoongoza kwenye amani na kujengana’ kwa njia ya mazungumzo, na kutafuta haki.