Tanzania:Watoto wanadanganywa na vitu,tuwapeleke shuleni&tusiwakabidhi boda boda
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Wazazi na walezi nchini Tanzania wanahamasishwa kulinda watoto wao hasa walio wadogo kufuatia na tabia za kihalifu zilizoibuka katika mji hasa jiji la Dar Es Salaa. Hiki ni kipindi ambacho sio cha kufumbia macho na masikio, bali kuwajibika kwa haraka na kuendelea kutoa elimu stahiki kwa watoto na familia zao, kuwa na umakini muhimu katika jamii iliyooendelea kubadilika. Hivi karibuni tarehe 15 Julai 2024, kumekuwa na mkutano wa kuelimisha huko Mbagala, Kata ya Charambe, jijini Dar - Ess- Salaam, ili kujidhatiti juu ya ulinzi na usalama katika jamii kwa ajili ya watoto, baada ya matukio ya kutisha ya kuuawa watoto watatu mfululizo mjini Dar Es Salaam. Na si hiyo tu lakini pia tukio jingine la upatikanaji wa mtu aliyekuwa ameiba mtoto, vitendo ambavyo vimeibua hisia kali kwa wazalendo wa jiji la Dar Es Salaam.
Matukio ya mauaji ya watoto watatu
Katika mkutano uliofanyika katika vitongoji hivyo vya jiji la Dar-Es -Salaam, wahusika wa Vyombo vya usalama Wilayani Mbagala, walitoa onyo na taadhari kubwa hasa kuelezea jinsi ambavyo Watoto kwa hakika wanapitia changamoto, lakini wazazi hawajuhi, kwa sababu wazazi hao “hawatengenezi urafiki ili kuwapa mazingira rahisi ya kuwaelezwa kinachowasibu wanapokuwa katika mazingira ya shule, wenzao au katika michezo. Akizungumza Afisa wa Polisi alisema: “Shida ikiwa mojawapo na hiyo ya kukaa bila huduma, watoto wanakutana na mtu mbaya na anawarubuni kwa vitu vidogo vidogo, wao wanaingia kule na wanapotea. Kwa sasa wilayani Mbagala kuna matukio ya mauaji ya watoto watatu wadogo. Hawa wameuawa katika mazingira ambayo wamebakwa, hadi kufa. Watoto wametupwa, na Jeshi la Polisi linaumiza kichwa dakika hii kumtafuta mtu huyu ni nani? Na wametoa hata taarifa za kutoa fedha kwa yoyote atatoa taarifa.”
Ndani ya jamii zetu tutoe taharifa kwa vyombo vya Usalama
Kwa kusisisitiza zaidi Afisa huyo alisema: “Lakini hiyo ndani ya jamii yetu tunamoishi kikubwa tunachokihitaji ni taarifa ili tuweze kuzifanyia kazi, katika harakati za kuepuka vitendo vya kikatili.” Polisi huyo alidha alithibitisha juu ya “ watoto kudanganywa kwa mfano wa kununuliwa chips na viatu. Kwa hiyo kuna vitu ambavyo wanadanganywa. Katika muktadha huo ndipo kuna haja ya kutoa mafunzo stahiki.” Onyo: “Tujitahidi kwa kuhakikisha tunawapeleka shuleni hasa watoto wa shule ya awali, usimkabidhi boda boda, au kumwacha mtoto mwenyewe aende kwa sababu anaijua njia ya shule.” Hii i kwa sababu uhakikishe mtoto kafika salama na amerudi salama.” Ni kwa sababu watoto wanapopita njiani wanakutana na changamoto nyingi. Na “ukifuatilia matukio yote, yaliyotokea, aliongeza kusema- ni mtu anakuta mtoto/ watoto njiani /yuko peke yake, au anacheza. Kwa hiyo changamoto kubwa ni ukosefu wa usimamizi. Katika kuepuka hili ni muhimu kupeleka watoto shuleni.”
Wazazi wahamasishwa kuzungumza na watoto na kutengeneza urafiki
Kwa upande wa wazazi aidha waliwahamasisha kwamba kamanda wa Polisi alisema: “tuongee na watoto wetu, wasipokee zawadi au kitu chochote kwa mtu yeyote, kwa sababu matokeo haya hatujuhi mhusika ni nani, lakini yawezekana akawa ni ndugu au hata jirani. Kwa hiyo huwezi kujua mbaya wako ni nani. Tunaishi katika jamii ambayo hatujuhi mbaya ni nani. Tujaribu kuongea na watoto wetu wasipokee vitu vyovyote kutoka kwa mtu yeyote”, alikazia kusema Polisi huyo. “Nipende kuwaomba wazazi, tujenge urafiki na watoto kwa sababu gani? Kwa sababu watoto wengi wanapata changamoto, lakini wazazi hatufahamu. Hatujuhi mtoto wako ameshindaje shuleni. Watoto wanapata changamoto lakini wanashindwa kumueleza mzazi, kwa hiyo ni kujitahidi kutengeneza urafiki na watoto.” Kwa ufafanuzi zaidi alisema: “Kwa mfano muulize anapata changamoto gani shuleni, katika michezo na wenzake, hata kwa baba, lakini amepewa vitisho. Lakini unapotengeneza urafiki na mtoto, unatengeneza mazingira ambayo inakuwa rahisi kupata habari.” Vile vile katika tukio la Kibonde maji Mbagala la mtoto aliyefariki, katika mazingira magumu sana ya kutisha shuhuda mwingine aliomba kutumia “sehemu hii ya matukio kama hayo kuwa makini ili yasirudiwe maana ni ya kutisha.”
Mawasiliano na tabia za udanganyifu kwa watoto
Ndugu msomaji hata hivyo inabidi kufanyia kazi nafasi ambayo inajumuisha au inaweza kuhusisha kuwasiliana na watoto, ambayo kiukweli iwe kipaumbele zaidi kwa sababu ya aina ya mazingira yawe shuleni, nyumbani hata michezo na kwingineko. Vile vile kufanyia kazi na watoto hasa kunamaanisha kuhusika katika shughuli na mtoto ambapo mawasiliano yanaweza kutarajiwa kama sehemu ya kawaida ya shughuli na mawasiliano ambayo yanawezesha kugundua hata wahalifu katika muktadha huo. Kwa sababu watoto kweli wanapitia wakati mgumu kuna matumizi ya nguvu dhidi ya mtoto ambayo humsababishia madhara. Tabia ya unyanyasaji wa kimwili ni pamoja na kusukuma, kumpiga kofi, kumtikisa, kumtupa, kumchoma, kumpiga ngumi, kumpiga mateke, kuuma, kunyonga, kumwekea sumu. Kuna unyanyasaji wa kingono ambapo kuna kumtumia mtoto kujitosheleza kingono kunakofanywa na mtu mzima au na mtoto mwenye umri mkubwa zaidi yake au kijana aliyebalehe. Kuna unyanyasaji wa kihisia unamaanisha kitendo kisichostahili kinachofanywa na mzazi au mlezi kwa mtoto, au kushindwa kwa muda kumpa mtoto malezi ya kutosha yasiyokuwa ya mwili. Vitendo kama hivyo vina uwezekano mkubwa wa kuharibu hali ya kujithamini au uwezo wa kijamii kwa mtoto katika makuzi yake.
Tabia mbaya ya kutelekeza watoto
Kutelekeza pia ni tabia ya kushindwa kwa mzazi au mlezi kumpa mtoto mazingira ambayo yanakubaliwa kiutamaduni kuwa muhimu kwa ukuaji wake kimwili, kihisia na ustawi. Na ambayo matokeo yake yanaweza hali ngumu kwa mtoto. Unyanyasaji mwingine wa kumwadhibu au kumrekebisha mtoto kwa njia isiyofaa au kumtaka mtoto kufanya mambo yanayozidi uwezo wake au ya kudharirisha na / au kumtolea mtoto maneno ya kudhalilisha mara kwa mara. Na bado kuna unyonyaji wa mtoto ambapo hufanya au kumlazimisha mtu mwingine kufanya kitendo au vitendo vya unyanyasaji dhidi ya mtoto. Katika suala jingine lililoenea sana kuna vitu vya ponografia vya watoto. Hii nyenzo inayoonesha mtu, au ni uwakilishi wa mtu, ambaye ni, au anaonekana kuwa chini ya miaka 18 na anajihusisha, au anaonekana kuhusika katika tukio la kingono au shughuli za kingono, na hufanya hivyo kwa njia ambayo mtu mwenye busara angechukulia kuwa, katika hali zote kuwa ni mbaya.
Tabia za kurubuni watoto kupitia mitandao ya kijamii
Tabia hizi mara nyingi zinatokea kwa kurubuni, kama ilivyoeleza katika muktadha wa udanganyifu kwa watoto. Kwa sababu hiyo ni tabia ambayo inafanya iwe rahisi kwa mhalifu kumpata mtoto kwa shughuli za ngono kwa urahisi Kwa mfano, mhalifu anaweza kujenga uhusiano wa uaminifu na mtoto, na kisha atafute uhusiano wa kimapenzi (kwa mfano kwa kuhimiza hisia za kimapenzi, au kunfundisha mtoto dhana za ngono kupitia ponografia). Kuna rubuni nyingi za karne hii kupitia mitandao mingi ya kijamii. Ambao kwa watoto wengi walio na simu za mikononi, unakuta wako katika mtengo. Kitendo cha kutuma ujumbe wa kielektroniki(SMS) kwa mtoto, kwa kusudi la kutaka mpokeaji kujiingiza au kujishughulisha na shughuli za ngono na mtu mwingine, pamoja na lakini sio lazima na mtumaji; au ya kutuma ujumbe wa kielektroniki (SMS)wenye maudhui yasiyofaa kwa mpokeaji ambaye mtumaji anaamini kuwa mtoto. Kwa njia hiyo kinachobaki kwa sasa ni uangalifu mkubwa katika usalama kwa ajili ya watoto na ili kuweza kutambua, kupunguza, kudhibiti au kupunguza hatari inayowazingra watoto ambazo kiukweli inawezekana kuthibiti kupiti wazazi, walimu, walezi na wote wenye mapenzi mema.