Rais wa Tume ya Ulaya Bi Ursula von der Leyen amechaguliwa tena kwa miaka mitano. Rais wa Tume ya Ulaya Bi Ursula von der Leyen amechaguliwa tena kwa miaka mitano.  (AFP or licensors)

Tume ya Ulaya,imethibitisha Bi Ursula von der Leyen kuwa rais tena!

Bunge la Ulaya lilitoa imani yake kwa Mjerumani kwa kura 401 za ndio,284 zilizopinga na 15 hazikushiriki.Kura saba batili.Kulikuwa na wapiga kura 707 idadi ya chini zaidi iliyohitajika kwa uchaguzi ilikuwa 360.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Makofi ya muda mrefu katika chumba cha Strasbourg yalifuatia kutangazwa kwa matokeo ya kura ya uthibitisho wa Bi Ursula von der Leyen kama mkuu wa Tume ya Umoja wa EU. Ni kura 360 zilihitajika kwa ajili ya ushindi; Bunge la Ulaya lilimzawadia rais kura 401 za upendeleo kutoka kwa Wabunge wa lengo wa Kijani Washoshalisiti,Waliberali na MEPs Maarufu, huku Wazalendo na wale wa mrengo wa kulia wakikaribisha uthibitisho huo kwa ubaridi.

Furaha ya von der Leyen

“Miaka mingine 5. Siwezi kueleza jinsi ninavyo shukuru kwa imani ya MEPs na wote walionipigia kura.” Ndiyo yalikuwa maneo ya Rais Mpya wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Bi Ursula von der Leyen ambapo aliandika kwenye akaunti ya X baada ya kuchaguliwa tena, huku akibainisha kwamba: “kura 401 za ndio zilikuwa ujumbe mzito wa imani. Nadhani ni hatua nzuri ya kuanzia. Wakati wa mkutano wa baada ya matokeo, Rais wa Tume ya Ulaya alisema: Nitafanya kazi kwa bidii na bora iwezekanavyo na wale walioniunga mkono.” Kiukweli, haya yote yanaunga mkono Ulaya, Ukraine na vyama vinavyounga mkono utawala wa sheria. Ninashukuru sana jukwaa la ‘EPP,’ ‘Renew na S&I’, lakini pia ninashukuru sana kundi la Kijani ambao waliniunga mkono, tulikuwa na mabadilishano makali juu ya masuala yote na ni vizuri kwamba mwishowe waliamua kuniunga mkono.”  Bi Ursula aidha alista kuhusu ulinzi wa Ulaya kwamba: “Hebu tufanye kazi pamoja kwa Ulaya yenye nguvu, kulingana na haki ya kijamii, kulinda watu kutoka katika mtazamo wa usalama, lakini juu ya yote kutetea demokrasia yetu, ambayo inashambuliwa kutoka ndani na nje.”

Ujumbe wa kupongeza rais wa Tume ya Ulaya

Hata hivyo ujumbe mwingi wa kumuunga mkono von der Leyen umefika kutoka kwa watetezi mbalimbali wa siasa za kimataifa: “Pongezi zangu kwa rafiki yangu Ursula von der Leyen kwa hawamu yake ya pili katika uongozi wa Tume ya Ulaya. Ushirikiano wa kimkakati wa NATO na Umoja wa Ulaya unachangia kuimarisha usalama barani Ulaya na kwingineko”. Hayo  yalisemwa na Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, Waziri Mkuu wa Poland; vile vile Donald Tusk, ambaye katika siku za nyuma pia aliwahi kushika wadhifa wa Rais wa Baraza la Ulaya kwamba: “Hongera kwa uthibitisho wako, mpendwa Ursula. Nyakati ni ngumu, lakini kwa ujasiri na dhamira yako, nina hakika utafanya kazi nzuri.” Matashi mazuri pia yalikuja kutoka kwa Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ambaye alizungumzia juu ya ishara ya wazi ya uwezo wa kuchukua hatua katika Umoja wa Ulaya, hasa katika nyakati ngumu.

Matashi mengine ni kutoka kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer: “Ninatarajia kufanya kazi kwa karibu na utafafanua upya uhusiano kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya”, alisema. Mwitikio kutoka Moscow pia ulikuwa wa hapo hapo: mwakilishi wa kudumu wa Urusi katika EU, Kirill Logvinov, alisema kwamba: “ushindi wa von der Leyen ni mafanikio ya utaratibu wa Ulaya na mfumo uliopo wa kisiasa ambao, licha ya matokeo maumivu ya uchaguzi wa Bunge la Ulaya,  inaendelea kufuata sera ambazo zimepelekea kuimarishwa kwa nafasi ya haki barani Ulaya.”

Rais wa Tume ya Ulaya amechaguliwa tena kwa miaka 5
19 July 2024, 16:34