WHO:Zaidi ya watoto milioni moja wako katika hatari ya utapiamlo mkali
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Zaidi ya watoto milioni moja wako katika hatari ya utapiamlo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) kutokana na kuongezeka kwa ghasia mashariki ambayo imesababisha mzozo mkubwa wa watu kuhama makazi yao. Malalamiko hayo yametokana na Shirika la Afya Duniani (WHO). Kwa sababu hiyo athari kwa raia inatokana na mzozo unaoendelea kati ya vikosi vya Kinshasa na wanamgambo wa M23 katika maeneo ya mashariki mwa nchi ambayo tayari imesababisha zaidi ya watu milioni 2.7 kukimbia katika Kivu Kaskazini pekee. Pia hali inayozidi kuwa mbaya zaidi ni mafuriko na maporomoko ya ardhi, pamoja na ukosefu wa usalama unaoathiri maeneo mengine ya nchi, huku karibu wakazi milioni 25 wanahitaji msaada wa kibinadamu kwa sasa, kulingana na maelezo ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO.)
Mwaliko kutoka WHO ili kuingilia kati
Kutokana na hiyo ndiyo mwaliko wa kuingilia kati mara moja ili kukidhi mahitaji ya kimsingi ulitoka kwa Adelheid Marschang, mkuu wa kitengo cha dharura cha WHO, wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Geneva Uswiss ambapo aliripoti jinsi ambavyo kwa mwaka huu tayari wamesajiliwa zaidi ya kesi 20,000 za kipindupindu na 60,000 za surua.
Jumuiya ya kimataifa imeomba iwekee vikwazo Rwanda
Wakati huo huo, kutoka Kinshasa mamlaka ya Congo imeiomba Jumuiya ya kimataifa kuiwekea vikwazo nchi ya Rwanda, inayoshutumiwa - pia kutokana na ripoti kutoka katika kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa-kuwaunga mkono waasi wa kundi la M23. Kigali, hata hivyo, inakanusha mashtaka yote. Huko lakini chini, mapigano yanaendelea licha ya maafikiano ya kibinadamu yanayoendelea: mapigano yameripotiwa katika eneo la Nyange na katika maeneo kadhaa kaskazini-magharibi mwa Goma.