Kisima kilichochimbwa ardhini ni kama kitanda cha mchanga na mimea iliyo karibu imekauka. Kisima kilichochimbwa ardhini ni kama kitanda cha mchanga na mimea iliyo karibu imekauka. 

Zimbabwe:ukame unazidi kuwa mbaya na hakuna chakula

Hakuna mavuno na kwa hiyo ukame nchini Zimbabwe unazidi kuwa mbaya na wakati huo huo hifadhi ya maji imekauka na utapiamlo unaongezeka.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kisima kilichochimbwa ardhini ni kama kitanda cha mchanga na mimea iliyo karibu imekauka. Ndicho kimachobaki katika hifadhi ya maji ambapo wakati flani ilikuwa kinamwagilia mazao na  kunywesha mifugo katika wilaya ya Mudzi kaskazini mashariki mwa Zimbabwe. Nchi, kama  ilivyo sehemu kubwa ya kusini mwa Afrika, inakabiliwa na ukame mbaya zaidi katika miaka arobaini, kutokana na mchanganyiko wa hali ya El Niño, wakati ongezeko la joto la kawaida la maji ya mashariki ya Pasifiki huangaza joto ndani ya hewa na kusababisha hali ya hewa ya joto duniani kote. Na ni joto la juu la wastani, linalofuatiliwa na wanasayansi hadi utoaji wa gesi chafuzi na mabadiliko ya hali ya hewa kwa ujumla.

Maji yalitoweka tangu Mei

Georgina Kwengwere mwanamke, mama wa watoto sita anayeishi kwa  kilimo lakini shambani mwake ni mahindi yaliyokauka kwa sababu  ya jua na ambaye aliliambia Shirika la Mpango na Chakula( AFP) kuwa: “Sikuvuna chochote baada ya kutumia akiba yetu kununua mbegu.”  Kwa upande wake alisema kuwa maji yalitoweka tangu mwezi Mei. Wakati huo huo, yeye na wanawake wengine wa kijiji hicho wanajaribu kukusanya kadiri wawezavyo, chini kabisa ya ardhi ambayo sasa ni kavu na isiyo na rutuba. Kisha wanatembea kilomita tano kila siku kufikia mji wa karibu wa  Kotwa, wakitumaini kupata kazi zisizo za kawaida, kuanzia dola tatu tu kwa siku.

Hakuna chakula katika nyumba

Ni wachache mno kulisha familia, ambapo Takesure Chimbu, mkazi mwingine  alithibitisha kuwa: “Hakuna chakula katika nyumba zetu.” Utapiamlo katika wilaya ya Mudzi, ambayo ina watu 164,000, unaenea. “Katika miezi mitatu iliyopita tumerekodi ongezeko la 20% la idadi ya kesi,” alisema Kudzai Madamombe, meneja wa afya wa eneo hilo. Takriban watu milioni 7.6 kwa sasa wanategemea misaada, wakati mamlaka ya Harare imetangaza hali ya maafa ya asili kutokana na upotevu mkubwa wa mazao, ambayo pia ni msingi wa marekebisho ya chini ya makadirio ya ukuaji wa Mfuko wa Fedha kwa nchi ya kimataifa: 2% mwaka 2024, ikilinganishwa na 5.3% mwaka  2023.

 

13 July 2024, 15:50