Tafuta

Josep Borrell, Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU)wa Sera ya Mambo ya Nje. Josep Borrell, Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU)wa Sera ya Mambo ya Nje.  (REUTERS)

Borrell(EU):Jumuiya ya kimataifa,iungane katika vita dhidi ya ubaguzi,chuki ya dini au imani!

Katika kuelekea Siku ya Kimataifa ya Waathirika wa Vitendo vya Ukatili kwa Msingi wa Dini au Imani,iadhimishwayo kila tarehe 22 Agosti,Umoja wa Ulaya (EU)unasema:“Misimamo mikali,ubabe,ugaidi na chuki zinazosababishwa na migogoro bado hazijatokomezwa.Watu wengi sana duniani kote hasa kutokana na wanakabiliwa na mashambulizi dhidi ya jumuiya zao na haki zao za kibinadamu zinakiukwa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika kuelekea hafla ya Siku ya Kimataifa ya Waathirika  wa Vitendo vya Ukatili kwa Msingi wa Dini au Imani,iadhimishwayo kila tarehe 22 Agosti ya k ila mwaka, Bwana Josep Borrell, Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU)wa Sera ya Mambo ya Nje tarehe 21 Agosti 2024 alitoa pongezi kwa waathiriwa wote wa ubaguzi, kutovumilia, mateso, chuki, kudhoofisha utu au vurugu kwa sababu ya dini au imani yao.  Bwana Borell alisema: “Misimamo mikali, ubabe, ugaidi na chuki zinazosababishwa na migogoro bado hazijatokomezwa. Watu wengi sana duniani kote, hasa kutokana  na dini ndogo, wanakabiliwa na mashambulizi dhidi ya jumuiya zao na haki zao za kibinadamu zinakiukwa kwa sababu ya imani yao halisi au inayofikiriwa.” Kwa kususiririza zaidi Bwana Borelli alisema “Tunaamini na kuunga mkono kwa dhati kanuni kwamba watu wote wana haki ya uhuru wa mawazo, dhamiri, dini au imani; na kueleza au kubadilisha dini au imani ya mtu, bila hatari ya ubaguzi, mateso au vurugu.” Kwa njia hiyo alibanisha kwamba “Muungano wa Ulaya unashutumu kuhalalishwa kwa uasi-imani na matumizi mabaya ya sheria za kukufuru zinapokiuka haki ya uhuru wa dini au imani. Sheria hizi ni kichocheo hatari cha chuki za kidini na uchochezi wa ubaguzi, uhasama au vurugu.”

Uwajibu wa kuhakikisha Ulinzi wa haki za binadamu

Kwa kuongeza Bwana  Borrell, alisema “ Tunakumbuka kwamba Mataifa yote yana wajibu wa kuhakikisha ulinzi wa haki za binadamu na kufanya bidii ili kuzuia, kuchunguza na kuadhibu vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watu kwa misingi ya dini au imani yao. Jumuiya ya kimataifa, lazima iungane katika vita dhidi ya ubaguzi, chuki na jeuri inayotokana na dini au imani. Ni lazima tuendeleze utamaduni wa kuvumiliana kidini, kuheshimu tofauti na kuelewana. Kila mtu, bila kujali ana imani au dini, ana haki ya kuheshimiwa kikamilifu kwa haki zake za kibinadamu. EU itaendelea kulinda kanuni hii na kukuza utekelezaji wake kila mahali.”

Ifuatayo ni tamko kamili la EU:Kila mtu awe huru wa mawazo ya imani na dini

Tamko zima la Mwakilishi wa Mkuu kwa niaba ya Umoja wa Ulaya katika  Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Wathriwa wa Vitendo vya Vurugu Kulingana na Dini au Imani ifanyikayo kila tarehe 22 Agosti anabainisha: “Katika hafla ya Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha Wahasiriwa wa Vitendo vya Ukatili Kwa Msingi wa Dini au Imani, Umoja wa Ulaya linatoa pongezi kwa wahasiriwa wote wa ubaguzi, kutovumilia, mateso, chuki, kudhoofisha utu au unyanyasaji kwa sababu ya dini au imani yao wanayoamini. Misimamo mikali, ubabe, ugaidi na chuki zinazochochewa na migogoro bado hazijatokomezwa. Ulimwenguni kote, watu wengi sana, haswa wale wa dini ndogo, wanakabiliwa na mashambulizi dhidi ya jumuiya zao na haki zao za kibinadamu zinakiukwa kwa sababu ya imani yao halisi au inayofikiriwa. Tunaamini kwa uthabiti kanuni, ambayo tunaiunga mkono kwa dhati, ambayo kwayo kila mtu ana haki ya uhuru wa mawazo, dhamiri, dini au imani na pia ana haki ya kudhihirisha au kubadilisha dini au imani yake, bila kuwa na hatari ya kubaguliwa. mateso au vurugu."

Jumuiya ya Kimataifa iunge mkono 

Aidha "Umoja wa Ulaya unalaani kuharamishwa kwa uasi-imani na matumizi mabaya ya sheria za kukufuru wakati zinakiuka haki ya uhuru wa dini au imani.  Sheria hizo ni kichocheo hatari cha chuki za kidini na uchochezi wa ubaguzi, uhasama au vurugu. Tunakumbuka kwamba Mataifa yote yana wajibu wa kuhakikisha ulinzi wa haki za binadamu na kuhakikisha kwamba yanazuia, kuelimisha na kukandamiza vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watu kwa misingi ya dini au imani yao. Jumuiya ya kimataifa lazima iungane katika kupiga vita ubaguzi, chuki na unyanyasaji kwa misingi ya dini au imani. Ni lazima kukuza utamaduni wenye sifa ya uvumilivu wa kidini, heshima kwa utofauti na maelewano. Kila mtu, awe anadhihirisha dini au imani yake, ana haki ya kuheshimu kikamilifu haki zake za kibinadamu. EU utaendelea kutetea kanuni hii na kukuza utekelezaji wake kila mahali.”

Siku ya kimataifa ya waathirika wa chuki dhidi ya dini au imani
22 August 2024, 15:24