Hadi sasa watu 2000 wamekamatwa nchini Venezuela
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya katika Sera ya Mambo ya Nje, Bwana Josep Borrell, akiungana na serikali saba za Ulaya: Italia, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Uhispania, Poland na Ureno ambao Dominika tarehe 4 Agosti walitoa tamko la pamoja huku wakitaka mhurasari wa ushindi wa Nicolás Maduro katika uchaguzi wa tarehe 28 Julai. Katika tamko hilo viongozi wa Ulaya walibainisha kuwa: “Kukomesha kukamata, ukandamizaji na maneno ya vurugu dhidi ya wanachama wa upinzani Venezuela yote, na wakati ambapo matokeo ya uchaguzi wa rais hayajathibitishwa na hayawezi kuchukuliwa mwakilishi wa mapenzi ya watu.” Hata hivyo viongozi wa Ulaya walipokea shukrani kutoka kwa kiongozi wa upinzani wa Venezuela, María Corina Machado, baada ya maelfu ya watu kuitikia wito wake wa maandamano mapya siku ya Jumamosi tarehe 4 Agosti 2024, wakimiminika katika mitaa ya nchi hiyo ya Amerika Kusini ili kupinga matokeo ya mashauriano na kumuunga mkono mgombea wa chama cha Edmundo González Urrutia(Plataforma Unitaria Democrática).
ULAYA YAKOSOA RAIS MADURO
Ukosoaji wa Umoja wa Ulaya (EU) na Borrell ulitoka kwa Rais Maduro, ambaye pia alishutumu upinzani kwa kutaka kunyakua urais na akatangaza kwamba Ulinzi wa kijeshi na polisi utaendelea. “Vikosi vya usalama, tayari vimewakamata watu 2,000, na kutishia kwamba wengine - wanaotuhumiwa kusababisha machafuko na ghasia wataishia kwenye magereza yenye usalama wa juu zaidi huko Tocorón na Tocuyito katika siku zijazo. Pia siku ya Jumamosi, tareeh 4 Agosti 2024 Chama cha Umoja wa Kisoshalisti cha Venezuela, kilicho madarakani kwa sasa, kilifanya maandamano ya kitaifa kuunga mkono uwekezaji wa Maduro kwa muhula wa tatu wa miaka 6.