2024.08.27 : Picha ya pamoja ya wachezaji na Washindi wa Toleo la Pili la Shindano la KUSI 2024 huko Zanzibar. 2024.08.27 : Picha ya pamoja ya wachezaji na Washindi wa Toleo la Pili la Shindano la KUSI 2024 huko Zanzibar. 

Kombe la Zanzibar 2024:kuelekea amani inawezekana

Wataalamu 33 kutoka mataifa 8 tofauti walishiriki Toleo la II la mashindano ya kimataifa ya kitesurfing,yaliyofanyika siku za hivi karibuni katika maji ya Fukwe za Kiwengwa,mjini Zanzibar.Kwa mujibu wa Dk.Stefano Conte,kati ya waandaaji wa tukio hilo alisema:“Mkutano kati ya watu mbalimbali ni mfano sahihi kwa ulimwengu unaohitaji kubadilisha mkondo.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hatimaye mchezo unaonaendeshwa na upepo katika kubembeleza kwa muda mrefu katika bahari,na ili kuweza kutuma hata ujumbe unaopingana na wa usasa uliopo umeweza kuwaona Wachezaji 33 wa kitaalamu ambao mnamo tarehe 24 Agosti 2024 walishiriki mashindano kwenye fukwe za Kiwengwa, kaskazini mwa Zanzibar nchini Tanzania. Hili llikuwa ni toleo la II  liitwalo: “Zanzibar CUP KUSI 2024,”kwa maana ya upepo wa Kusi ambapo walikusanyika kusherehekea mkutano kati ya watu mbalimbali. Kwa bahati nzuri pepo za msimu zinazovuma kwa nguvu katika ukanda huo wa visiwa vya Tanzania, mashariki mwa pwani ya Afrika Mashariki, ulivuma na  kuifanya iwezekane kufanya mazoezi ya mchezo huo unaojumuishwa hata hivyo katika nidhamu  kati ya taaluma za Olimpiki.

Washindi wa Zanzibar Cup 2024
Washindi wa Zanzibar Cup 2024

Dk. Stefano Conte, ambaye ni daktari wa watoto kutoka Italia na anayeishi Zanzibar, ambaye amejitolea sana kwa miaka mingi barani Afrika na mmoja wa waandaaji wa mbio hizo, alieleza kwa vyombo vya habari vya Vatican baada ya shindano hilo kwamba: “ Upepo ndiyo chanzo cha kuteleza kwa kite kwa sababu bila angalau fundo 10, huwezi kufanya  mbio hizo. Huu ni mchezo kwa hakika unaoendeshwa na upepo katika kubembeleza kwa muda mrefu kwenye bahari, na kutaka kutuma ujumbe unaopingana na usasa uliopo.” Alisema Dk huyo.

Mashindano ya Zanzibar 2024
Mashindano ya Zanzibar 2024

Akidadavua juu ya tukio hilo Dk Conte alisema :“Kwa bahati Jumamosi kulikuwa na karibu mafundo 20, hata ikiwa ilikuwa juu ya upepo wote wa udugu ambao ulivuma sana kwa washiriki wa mataifa 8 tofauti waliounganishwa na mapenzi yao ya mchezo mmoja.” Dk. Stefano aliongeza kuwa “Mbali na kujiburudisha, vijana walipata hali ya urafiki na amani- na  huku akieleza kwamba- kwa njia yao ndogo, ni kielelezo sahihi kwa ulimwengu ambao mara nyingi unapitia njia tofauti, zile za vita na nchi zenye migogoro kutokana na maslahi na uchoyo. Taratibu zote ambazo hazielekei popote na ni ndugu zetu wa Kiafrika wanaotufundisha hilo kwamba: hakika unaweza kujisikia vizuri hata kwa  kiganja cha mchele, samaki kidogo, jua na bahari. Hakuna haja ya ujuu juu hasa katika ulimwengu wa Magharibi na katika baadhi ya simulizi za vyombo vya habari, kuchukuliwa kuwa ni za lazima ili hali kiuhalisia zichangie udanganyifu mkubwa tu."

Furaha ya ushindi wa Kombe la Zanzibar Cup 2024
Furaha ya ushindi wa Kombe la Zanzibar Cup 2024

Kwa Mshindi wa shindano la kimataifa alikuwa kutoka Italia mwenye asili ya Follonica, Jacopo Cantini, ambaye alifungua shule ya kitesurfing huko Watamu, nchini Kenya. Kwa kuzingatia toleo lijalo la mchezo wa kitesurfing, unaotarajiwa kufanyika mnamo  Februari 2025, Dk. Conte alitunga hata  wimbo wa: “Zanzibar Cup song”, ambao anaota unaweza kufasiriwa na mwimbaji maarufu: wakati wa kusubiri, kutoka Zanzibar, kati ya “badiliko la ukuta” mmoja na mwingine, uthibitisho ulienea kama wimbi kwamba mchezo unaweza kuunganisha wahusika wake wakuu, hata kama wanatoka ulimwengu wa mbali, katika kukumbatia ubinadamu, kwa matumaini ya kuelekea kwenye amani.

28 August 2024, 18:05