Maandamano ya Bangladesh Maandamano ya Bangladesh  (AFP or licensors)

Makazi ya Sheikh Hasina yashambuliwa na Jeshi kuelekea serikali ya mpito

Baada ya majuma kadhaa za maandamano ya ghasia,waziri mkuu wa Bangladesh amejiuzulu na Mkuu wa majeshi,Jenerali Waker-Uz-Zaman,alitangaza kuundwa kwa serikali ya mpito.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Waziri Mkuu Sheikh Hasina amejiuzulu na tayari kuondoka Bangladesh, chini ya shinikizo la wanafunzi na maandamano dhidi ya serikali ambayo yameendelea kwa juma katika nchi hiyo ya Asia. Hayo yameripotiwa na vyanzo vya jeshi huko Dhaka, vilivyonukuliwa na shirika la Reuters, baada ya maelfu ya waandamanaji kushambulia makazi yake rasmi katika mji mkuu asubuhi tarehe 5 Julai 2024. Wakati jengo hilo likilengwa na waandamanaji, waziri mkuu - aliye madarakani tangu 2009 - tayari alikuwa ameondoka kwenye jengo hilo pamoja na dada yake, vyombo vya habari vya ndani, vilieleza ambavyo vilizungumza juu ya kuhamishwa kwake kwa helikopta hadi “mahali salama.”

Kuundwa kwa serikali ya mpito

Mkuu wa majeshi, Jenerali Waker-Uz-Zaman, alitangaza kuundwa kwa serikali ya mpito. Wakati huo huo, katika saa chache zilizopita idadi ya waliofariki kutokana na mapigano kati ya vikosi vya polisi na waandamanaji katika mwezi uliopita iliongezeka hadi 300, ambapo 94 kati yao walikufa tarehe 4 Agosti 2024, kulingana na takwimu za shirika la ‘Presse’ la Habari  Ufaransa, na ripoti za polisi na taarifa za madaktari na hospitali, wakati jeshi lilikuwa limeweka amri ya kutotoka nje kwa muda usiojulikana na miunganisho ya mtandao ilikuwa imekatwa katika jaribio la kukomesha machafuko.

Maandamano ya wanafunzi

Maandamano hayo yalianza katika Juma za hivi karibuni wakati maandamano ya wanafunzi dhidi ya mfumo wa nafasi zilizohifadhiwa katika kazi za umma: mapigano yalizuka na polisi na wanaharakati wanaoiunga mkono serikali, na kusababisha vurugu ambazo zilitikisa nchi nzima. “Vurugu za kushtua nchini Bangladesh lazima ziishe, Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, tarehe 4 Agosti 2024 alisema huku, akizitaka mamlaka kutowalenga waandamanaji kwa amani.Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa alitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa ghasia nchini Bangladesh, ambazo zimegharimu maisha ya watu wengi, wakiwemo maafisa wa polisi, mwishoni mwa wiki. Katika ukurasa wa habari za Umoja wa mataifa zinabainisha kuwa “Zaidi ya watu 80, wakiwemo polisi 13, wanasemekana kuuawa katika mapigano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji, kulingana na ripoti za vyombo vya habari. Mamlaka ya nchi hiyo imeweka amri ya kutotoka nje na imezuia upatikanaji wa mtandao wa intaneti. Kituo cha polisi katika wilaya ya Sirajganj, takriban kilomita 100 sawa na maili 62.5 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka, pia kilishambuliwa.

05 August 2024, 16:42