Mkutano wa watu Rimini,Mattarella:Mtu awe kitovu cha maisha na jumuiya!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mbele ya fursa nyingi kwa ajili ya ubinadamu , tunagusa kwa mkono wetu makosa ukatili na kuongezeka kwa vita, tamaa ya kutawala, na kurudi kwa kushangaza kwa siku za nyuma. Hisia za hofu, kutoaminiana, wakati mwingine kutojali, si mara chache kuwa na chuki na hasira, ambazo hutokea tena. Kwa sababu hiyo ni muhimu kumrudisha mtu huyo katikati. Tamaa ya maisha na utimilifu, katika uhusiano na jamii. Kwa sababu kilicho muhimu hakiko katika kujitenga, kujitosheleza binafsi, bali katika kukutana na wengine, katika ugunduzi wa ukweli ambapo mtu mwingine ndiye mbebaji na kwa hiyo katika kutembea pamoja, katika ile kesho ya kufikirika na ukaribu na kujengwa.
Mchango wa utamaduni, mazungumzo na ubinadamu
Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella, ameandika katika ujumbe wake aliomtumia Rais wa Mfuko wa Mkutano wa Urafiki na Watu (Fondazione Meeting per l’amicizia fra i popoli), Bwana Bernhard Scholz, katika fursa ya Ufunguzi wa Toleo la 45 la tukio hilo ambalo linafanyika jijini Rimini mkoa wa Emilia Romagna nchini Italia kuanzia tarehe 20 hadi 25 Agosti 2024. Katika ujumbe huo, Mkuu wa Italia anabainisha kuwa “ Mwaka huu pia, Mkutano unatoa mchango wake wa utamaduni, mazungumzo na ubinadamu. Ni historia ambayo imeweza kuhoji sababu za msingi za jamii yetu na ambayo inaendelea kujirekebisha, ikihusisha vijana na wazee, kujaribu kufahamu zaidi ya dharura ni nini kinachosonga zaidi.
Ahadi ya kielimu na kiutamaduni
Bwana Mattarella aidha anasisizitia kuwa “Ninatoa salamu zangu za dhati kwa wale watakaoshiriki, kwa uhakika kwamba siku za Rimini zitakuwa utajiri wa thamani kwa kila mtu, na kwa waandaaji na watu wanaojitolea ninatoa shukrani zangu kwa kujitolea kwao kulingana na mandhari ya toleo hili linaelezea mizizi ya kiutamaduni ya Mkutano kwa kupendekeza mtazamo wazi wa mabadiliko ya ajabu tunayopitia.” Kwa kuhitimisha kiongozi wa Italia anatoa pongezi kuwa “Ahadi ya kielimu na kiutamaduni, ambayo Mkutano unashuhudia, ina thamani kubwa.”
Mkutano wa Rimini juu ya kutafuta muhimu huanza
Upepo wa vita, uharaka wa amani, maswali ambayo yanasumbua moyo wa mwanadamu, kujitolea kwa vijana na kujitolea kwa ujumba ni viungo vingi vya toleo la 45 la tukio la 2024, ambalo linafungua kwa kuingilia kati kwa Patraka wa Kilatini wa Yerusalemu, Kardinali Pizzaballa. Mikutano 140 imepangwa na wasemaji karibu 450 wa Kiitaliano na wa kimataifa
Nchi Takatifu na ukosefu wa usawa
Katika siku ya kwanza ya Mkutano ni matarajio yaushuhuda wa Hussam Abu Sini, mkuu wa Ushirika na Ukombozi katika Nchi Takatifu na onesho la Changamoto ya Yerusalemu na mkurugenzi Otello Cenci, ambamo mwandishi wa tamthilia Eric-Emmanuel Schmitt anatafuta mbegu za amani kati ya mitaa ya mji mtakatifu Mwanauchumi Branko Milanovic na rais wa zamani wa Tume ya Ulaya Jose Manuel Barroso ambao watajadili kuongezeka kwa ukosefu wa usawa unaozalishwa na mifumo ya kiuchumi katika nchi mbalimbali baada ya Uviko. Ratiba hiyo inajumuisha kuakisi magonjwa ya akili kwa kuzingatia uzoefu wa Franco Basaglia na mazungumzo kati ya mashirika ya umma na biashara kuhusu umuhimu wa maji.
Ni ratiba iliyojaa
Ratiba kwa hiyo ya Mkutano inajumuisha jumla ya makongamano 140 yenye wazungumzaji 450 wa Kiitaliano na kimataifa, ambapo 100 wanatoka nje ya nchi. Masaa 200 za utiririshaji wa moja kwa moja yatatangazwa katika lugha 7. Mwaka huu 2024 pia kutakuwa na watu wa kujitolea 3,000, wakati 500 katika mkutano wa awali na 2,500 wakati wa hafla hiyo, asilimia 60 kati yao wakiwa na umri wa chini ya miaka 30. Miongoni mwao pia kuna vijana kutoka Brazil na Armenia, na uwakilishi mkubwa kutoka Uswiss, Hispania na Ureno. Kutakuwa na maonesho 16 yaliyowekwa, ikiwa ni pamoja na maisha na kazi za Alcide de Gasperi; mapatano ya Noeli ya 1914 katika Vita vya Kwanza vya Dunia; ujenzi wa Mabasilika ya Mlima Tabori na Gethsemane. Baadhi ya maonesho ya toleo la 2024 la Mkutano yatafanyika kwa njia ya msafiri na yatawasilishwa katika miji mbalimbali ya Italia kuanzia Septemba.
Scholz: "Hatujiachii kwa kutojali kwa ulimwengu"
Kwa mujibu wa Rais wa Mfuko wa Mkutano wa Urafiki wa Watu Rimini, Bernand Scholz katika mahojiano yaliyofanywa na ofisi ya waandishi wa habari kuhusu Mkutano alisema kuwa unafanyika katika wakati wa kihistoria wa kushangaza, uliojaa mabadiliko makubwa ya kusikitisha, ya teknolojia na kiuchumi, na haijulikani na yasiyoweza kutabirika, na migogoro mingi, ikiwa ni pamoja na ya kimataifa. Katika Mkutano huu tunataka kwa pamoja kugundua tena kile kinachoturuhusu kuwa wahusika wakuu hata katika nyakati hizi ngumu, kutoshindwa, kutokimbilia kutojali na kujiuzulu.” Kwa rais, huyo utoaji mpana wa hafla hiyo ni kugundua ni kiasi gani kizuri kilichopo katika ulimwengu ambao kwa njia nyingi hauonekani kutoa nafasi kubwa ya matumaini, kwa siku zijazo. Mwaliko, ukikumbuka mada ya Mkutano, ni kutoka nje ya juu juu, kusema kwamba kuna jambo muhimu, ambalo kila mtu anaweza kulifikia, hata katika mabadiliko makubwa tunayopata katika uchumi, shuleni, katika viwanda, katika siasa.