Mtazamo wa dunia yetu na matukio yake
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mnamo 2023, idadi ya migogoro iliyohusisha mataifa ilikuwa jumla ya 59, idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea tangu mwanzo wa ukusanyaji wa data mnamo 1946. Vilele vya awali vilionekana mnamo 2020 na 2022, kila moja ikiwa na migogoro 56. Kati ya hiyo migogoro 28 ilikuwa barani Afrika. Kwa njia hiyo katika taarifa hiyo migogoro zaidi ya silaha ilitokea ulimwenguni mwaka huko kuliko mwaka wowote tangu kumalizika kwa Vita vya Kidunia vya pili,kulingana na utafiti uliochapishwa wa Norway. Lakini pamoja na migogoro hiyo bado kuna mabadiliko ya tabianchi, yanayo sababisha vimbunga na mafuriko., Jua kali. Tunaweza kusema Ulimwenguni kwa ujumla hakuna amani. Tutazame hali halisi hizi za migogoro na mengine katika makala hii kwa kuanzia nchi za Mashariki ya Kati.
Mizozo huko Israeli na Ukraine
Israel imesitisha mapatano ya muda ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza ili kuwezesha chanjo ya polio kwa wakazi wa eneo hilo, kwa Mujibu wa ripoti ya Channel 13. Kwa upande wa Ukraine – na Urusi: Kiev bado iko katika vituko vya Moscow. Kwa sababu uchafu kutoka ndege isiyo na rubani(drons) iliyoanguka usiku wa tarehe 28 Agosti kwenye uwanja wa michezo katika eneo la makazi la kitongoji cha Dnipro, Bwana Vitaliy Klychko Meya alisema, akiongeza kuwa uchafu kutoka ndege nyingine isiyo na rubani iliharibu ghorofa kwenye sehemu za kitongoji cha Holosiiv. Wakati wa usiku, msururu wa ndege zisizo na rubani za Urusi ziligonga pia maeneo mengi ya Ukraine, Jeshi la Wanahewa linaripoti. Hata hivyo ukimya wa baridi wa Moscow juu ya mpango wa amani ambao rais wa Ukraine Zelensky ananuia kuwasilisha kwa Marekani na kwamba “Hautatuzuia. Tutaendelea na operesheni maalum na tutafikia malengo, alisema msemaji wa Kremlin Peskov.
Olimpiki ya Walemavu huko Paris,Ufaransa
Kwa upande wa michezo ya Olimpiki sehemu ya Pili huko Paris Ufaransa: Onesho kwenye Champs Elysees lilifungua Olimpiki ya Walemavu. Kuanzia tarehe 30 Agosti wanariadha 4,400 watashiriki mashindano 549 katika taaluma 23. Idadi ya chaneli za runinga zitakazofuatilia mashindano hayo inadaiwa kuwa hazijawahi kutokea kwani ni 165. Na huko Jijini New York Marekani unafanyika. Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuhuisha tena mamlaka ya ujumbe wa kulinda amani nchini Lebanon. Na kwa upande wa Beijing pia unafanyika Mkutano na waandishi wa habari wa kila mwezi wa Wizara ya Ulinzi ya China. Tukitazama huko jijini Baguio (Ufilipino unafanyika Mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari wa Mkuu wa Wafanyakazi wa Ufilipino, Jenerali Romeo Brawner, na mkuu wa Kamandi ya Indo-Pacific ya Merika, Admiral Samuel Paparo. Brussels Ubelgiji unafanyika Mkutano usio rasmi wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya. Na kuanzia tarehe 29-30 Agosti 2024 inafanyika Ziara ya Rais wa Ufaransa Bwana Emmanuel Macron huko Belgrade nchini Serbia.
Hali mbaya ya hewa imekumba Asia, Afrika na Ulaya
Kuna dharura kamili katika nchi kadhaa za Asia na Afrika kutokana na mvua na mafuriko. Kuna hali ya tahadhari nchini Japani kutokana na kuwasili kwa kimbunga Shanshan, ambacho kitaleta dhoruba kali, na uharibifu pia unaripotiwa nchini Sudan kutokana na machafuko ya siku za hivi karibuni ambayo yalisababisha kuporomoka kwa bwawa la Arbat. Tarehe 27 Agosti 2028 mvua kubwa ya radi pia ilisababisha usumbufu na uharibifu katika maeneo mbalimbali nchini Italia kutokana na radi nyingi.
Kimbunga Japan
Kwa njia hiyo nchini Japan inangoja kuwasili kwa kimbunga chenye nguvu sana, ambacho kitapiga kisiwa kikuu cha kusini cha Kyushu na kuleta dhoruba kali zisizo za kawaida. Wakati huo huo, watu watatu hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya ardhi. Mamlaka za eneo hilo zimetoa maonyo ya kuhama kwa watu 810,000 katika wilaya ya kati ya Shizuoka huko Honshu na wengine 56,000 huko Kagoshima huko Kyushu.Tangu tarehe 27 Agosti 2024, maeneo makubwa ya nchi hiyo ya Japan tayari yalikumbwa na mvua kubwa na jioni ukuta wa matope, mawe na vifusi ulisomba nyumba huko Gamagori, jiji lililo katikati mwa mkoa wa Aichi. Watu wawili waliokolewa, lakini wengine watatu hawajulikani walipo.
Hali mbaya ya hewa pia barani Afrika.
Nchini Sudan, machafuko makali yalisababisha kuporomoka kwa bwawa la Arbat, na kusababisha watu wasiopungua 60 kuuawa na 100 kupotea. 50 elfu bila makazi. Nchini Nigeria, kutokana na wiki za mafuriko makubwa, takriban watu 170 wamekufa na zaidi ya 200,000 wamelazimika kuyahama makazi yao. Eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ya Afrika ndilo lililoathirika zaidi. Hata hivyo, maeneo mengine yanasalia katika hatari, huku kukiwa na mvua kubwa na kuongezeka kwa viwango vya maji katika mito yake miwili mikubwa, Niger na Benue. Hali mbaya ya hewa pia iliikumba Yemen, na kusababisha watu 24 kupotea.
Dharura ya wahamiaji katika Visiwa vya Canary,waliofika waliongezeka maradufu kwa mwaka
Njia ya kuelekea Visiwa vya Canary imekuwa yenye shughuli nyingi zaidi barani Ulaya. Kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Hispania, waliofika wameongezeka zaidi ya mara mbili katika mwaka 2024 : kati ya Januari 1 na Agosti 15, wahamiaji 22,304 walifikia visiwa, ongezeko la 126% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mnamo 2023. Ili kukabiliana na hali ya dharura, gavana wa visiwa Fernando Clavijo alikutana Ijumaa 23 Agosti 2024 huko La Palma na Waziri Mkuu Pedro Sanchez, ambaye anazuru Mauritania, Gambia na Senegal tarehe 28 Agosti na siku inayofuata, 29 Agosti nchi za asili na usafirishaji wa wahamiaji.
Tatizo la watoto wadogo
Hali hiyo visiwani inakaribia kuporomoka. Katika visiwa hakuna nafasi au huduma za kusimamia idadi kubwa ya wahamiaji. Tangu mwanzoni mwa msimu wa joto, kamati ya shida imeundwa kusimamia upokeaji wa watu wanaoweza kuwasili na serikali ya mkoa imepanga uwekaji wa mahema kwenye visiwa vya Fuerteventura, El Hierro, Lanzarote na Tenerife lakini kutua kunaonesha hapana. dalili za kupungua. Tatizo linawakilishwa hasa na watoto wadogo wasiosindikizwa. Kulingana na sheria za Hispania, kiukweli, eneo ambalo watoto hufikia linawajibika kwa ulinzi wao, lakini leo hii kuna zaidi ya watoto na vijana 5,000 katika visiwa hivyo wakati maeneo yaliyohakikishwa na utawala wa mkoa ni karibu 2,000.