Nicaragua yafuta Mashirika 1500 yasiyo ya kiserikali
Vatican News
Serikali ya Nicaragua imefuta hadhi ya kisheria ya mashirika 1,500 yasiyo ya kiserikali yaliyopo nchini, na kuhamisha mali zao kwa serikali. Uamuzi huo, ulioidhinishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Maria Amelia Coronel, na kuchapishwa katika gazeti la serikali la Nicaragua ‘La Gaceta’ inatokana, kama inavyooneshwa, kutokana na kutotekelezwa na NGOs kwa baadhi ya majukumu, kama vile kuwasilisha, kwa muda wa kati ya mwaka mmoja na 35 bajeti zao kulingana na muda wa fedha, pamoja na mchanganuo wa kina wa mapato na matumizi, bajeti ya malipo, maelezo ya michango na bodi zao za wakurugenzi.” Mashirika hayo, kama yalivyoripotiwa na baadhi ya tovuti huru kama vile 100%Noticias na La Prensa, ambazo hazikupokea notisi yoyote, zinashutumiwa na serikali kwa kuzuia udhibiti wa Wizara ya Mambo ya Ndani. Kulingana na makubaliano yaliyopo hadi sasa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu sasa itawajibika kwa uhamisho wa mali zinazohamishika na zisizohamishika kwa jina la Jimbo la Nicaragua.
Nicaragua, mapadre wengine wawili walifukuzwa na kupelekwa Roma
Ufungaji huo mkubwa, kwa vyanzo vya wanahabari vinasisitiza zaidi, kufuatia tangazo la makamu wa rais, Rosario Murillo la mfano mpya wa ushirikiano kati ya NGOs na serikali, ambapo mashirika sasa, ili kutekeleza miradi yao, yanalazimika kuwasilisha programu au miradi na kushirikiana na taasisi za serikali. Misamaha pia imeondolewa. Mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yaliyofungwa ni ya jumuiya za kiinjili, ambapo yale ya Kikatoliki yanajumuisha, miongoni mwa mengine, Caritas ya jimbo la Granada. Misaada, michezo na vyama vya asili pia vinaonekana kwenye orodha. Kwa hatua hiyo ya hivi karibuni, ambayo haijawahi kushuhudiwa kwani kwa mara ya kwanza na sheria moja ya mashirika 1,500 yamepigwa marufuku, zaidi ya NGOs 5,200 zimefutwa tangu 2018, kwa mwanzo wa maandamano maarufu.