Kila tarehe 29 Agosti ni Siku ya Kimataifa dhini ya majaribio ya Nyuklia. Kila tarehe 29 Agosti ni Siku ya Kimataifa dhini ya majaribio ya Nyuklia. 

Siku ya Kimataifa Dhidi ya Majaribio ya Nyuklia,chi zote zitie sahini ya Mkataba

Mkataba wa kimataifa wa kupinga majaribio ya silaha za nyuklia(CTBT)haujaweza kuanza kutumika kwa sababu idadi ya nchi zinazopaswa kuridhia ili uweze kuanza kutumika bado haijatimia.Katibu Mkuu wa UN Bwana Guterres ametuma ujumbe kwa kutaka nchi hizo zifanye haraka na bila masharti.Nchi hizo ni 9:China,Misri,India,Iran,Israeli,Korea Kaskazini,Pakistani,Urusi na Marekani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Bomu la nyuklia ni silaha inayosababisha mlipuko mkubwa sana. Kati ya silaha zote, hilo ni lenye nguvu na pia lenye hatari zaidi. Katika dunia hii bado kuna  mataifa yenye uwezo mkubwa wa silaha hatari za nyuklia ulimwenguni na kuwa tishio kubwa. Na kila taifa linalomiliki silaha za kinyuklia lina mpango wa kuboresha zana zake za kivita. Marekani na Urusi ndizo zinazomiliki idadi kubwa ya silaha za kinyuklia duniani. Kwa njia hiyo kila tarehe 29 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa Dhidi ya Majaribio ya Nyuklia. Katika taarifa  inabainisha kuwa Mkataba wa kimataifa wa kupinga majaribio ya silaha za nyuklia, CTBT, haujaweza kuanza kutumika kwa sababu idadi ya nchi zinazopaswa kuridhia ili uweze kuanza kutumika bado haijatimia. Mkataba huo ulipitishwa na Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa tarehe 10 mwezi Septemba mwaka 1996, na kutiwa saini tarehe 24 mwezi huo huo wa Septemba mwaka 1996. Ingawa hivyo hadi sasa haujaanza kutumika ukisubiri nchi 9 ambazo ni China, Misri, India, Iran, Israeli, Korea Kaskazini, Pakistani, Urusi na Marekani.

Katibu wa Un, Dunia iung mkono kauli moja ya kumaliza mazoezi haya

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Antonio Guterres ametumia ujumbe wake wa siku hii  ambayo ni ya kimataifa ya kupinga majaribio ya silaha za nyuklia, kwa kutaka nchi hizo zifanye hivyo haraka bila kuchelewa na bila masharti. Msingi wa wito huo ni kwamba majaribio ya nyuklia yameleta uharibifu mkubwa, na kufanya iwe vigumu kuishi kwenye ardhi na kuleta matatizo ya kudumu ya kiafya. Katibu Mkuu ameonya kuwa wito wa hivi karibuni wa kurudi kwenye majaribio la nyuklia unaonesha kwamba masomo ya matukio mabaya ya zamani yamesahaulika au kupuuziliwa mbali.  Katibu Mkuu alisema, “katika siku ya kimataifa ya kupinga majaribio ya silaha za nyuklia, dunia lazima iunge mkono kwa kauli moja  kumaliza mazoezi haya mara moja. Mkataba wa Kukomesha majaribio la Nyuklia ndiyo marufuku pekee ya majaribio yote ya nyuklia, na chombo muhimu na kinachoweza kuthibitishwa cha usalama.” Hadi sasa, mionzi ya nyuklia bado inaenea ndani ya mazingira  kote duniani  kiasi kwamba inaweza kupimwa na kupatikana  kwenye pembe za tembo,  kwenye mwamba mkubwa wa matumbawe na kwenye mashimo yenye kina kirefu zaidi duniani.

Milipuko mibaya 1945

Hali hii hatari imemhamasisha na Balozi Dennis Francis, Rais wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na Dkt. Robert Floyd, Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Mkataba wa Kimataifa wa Kukomesha Jaribio la Nyuklia (CTBTO), kutoa wito wa hatua za pamoja kwa ajili ya kumaliza jaribio lolote la nyuklia kwa ulimwengu mzima na kwa kudumu kupitia makala ya maoni. Kupitia tahariri yao ya pamoja kwa siku hii ya kimataifa dhidi ya majaribio ya silaha za nyuklia, wawili hawa wanazihimiza nchi kuwa wazi kwa hatua zinazohitaijka ili kufikia makubaliano ya mwisho duniani chini ya Mkataba wa Kukomesha Jaribio la Nyuklia ili kumaliza jaribio la nyuklia. Balozi Francis na Dk. Floyd wanabaini kuwa jaribio la silaha za nyuklia kati ya mwaka 1954 na 1984 limekuwa na milipuko mibaya zaidi angani, baharini, juu ya ardhi na chini ya ardhi ikilinganishwa na mabomu yaliyotumika Hiroshima nchini Japani mwaka 1945. Viongozi hawa wanaonya pia kuwa akiba ya silaha za nyuklia inaongezeka kwa kasi mwaka hadi mwaka, nyingi zao zikiwa na nguvu zaidi kuliko mabomu yaliyotumika Hiroshima na Nagasaki nchini Japani. Wanaeleza kwamba ingawa kulikuwa na makubaliano ya kumaliza jaribio la nyuklia la milipuko katika miaka ya sitini, kukuza na kupunguza usambazaji wa nyuklia na silaha, ilichukua takribani miaka 30 zaidi na kulitokea milipuko zaidi ya jaribio la nyuklia kabla ya Mkataba wa Kukomesha Jaribio la Nyuklia (CTBT) kupitishwa mwaka 1996.

Kuhalalisha majaribio ya nyuklia ni kuvunja amani na mshikamano wa kimataifa

Wanaamini kuwa CTBT ni moja ya mikataba muhimu zaidi duniani yenye mafanikio makubwa, wakitaja kwamba katika karne hii, ni majaribio sita pekee yamefanyika, yote yakifanywa na Korea Kaskazini. Mkataba huu unategemea mtandao wa vituo zaidi ya 300 vya kisayansi duniani kote vinavyoweza kugundua haraka jaribio la nyuklia, hasa likiwa dogo zaidi kuliko mlipuko wa Hiroshima na kubaini mahali pake, hivyo hakuna nchi popote duniani inayoweza kufanya jaribio la silaha za nyuklia kwa siri. Licha ya maendeleo haya, Balozi Francis na Dkt. Floyd wanabainisha kwamba kuhalalisha upya majaribio la nyuklia, au hata matumizi ya silaha za nyuklia katika mgogoro, kutavunja imani na mshikamano wa kimataifa. Wanasisitiza pia kwamba kurudi kwenye siku za majaribio ya nyuklia bila kizuizi kutaacha nchi au jamii bila usalama. Wakihamasisha   mkataba huo zaid, wanasema , “nchi zinapaswa kujifunza kutokana na mafanikio ya mkataba huu. CTBT inajumuisha ubora wa diplomasia na teknolojia kwa faida ya pamoja ya kimataifa. Inajenga uwazi na imani, hasa wakati uwazi na imani vinaonekana kupungua.” Jaribio la kwanza kabisa la nyuklia duniani lilifanywa na Marekani  asubuhi ya Julai 16 mwaka 1945 kwenye jangwa la Alamogordo huko New Mexico.

IAEA kupata taarifa za ndege zisizo na rubani katika Kiwanda cha Nguvu za Nyuklia cha Kursk,Mkurugenzi Mkuu Grossi kutathmini eneo

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) lilifahamishwa na Shirikisho la Urusi leo kwamba mabaki ya ndege isiyo na rubani yalipatikana ndani ya eneo la Kiwanda cha Nguvu za Nyuklia cha Kursk. Vipande vya ndege zisizo na rubani ziliripotiwa kuwa ziko takriban mita 100 kutoka katika kituo cha kuhifadhi mafuta ya nyuklia kilichotumika. IAEA iliarifiwa kuwa ndege hiyo isiyo na rubani ilizimwa mapema asubuhi ya tarehe 22 Agosti 2024. Katika muktadha huu, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Bwana Rafael Mariano Grossi alithibitisha nia yake ya kutathmini kibinafsi hali katika tovuti wakati wa ziara yake wiki ijayo. Wakati wa ziara yake, Mkurugenzi Mkuu Grossi atatathmini hali kwenye tovuti na kujadili mbinu kwa ajili ya shughuli zaidi kama inaweza kuhitajika ili kutathmini usalama wa nyuklia na hali ya usalama wa Kursk Nuclear Power Plant. “Shughuli za kijeshi katika eneo la kinu cha nyuklia ni hatari kubwa kwa usalama na usalama wa nyuklia. Ziara yangu ya KNPP wiki ijayo itatupatia ufikiaji wa wakati wa kutathmini hali kwa uhuru,” Mkurugenzi Mkuu Grossi alisema.

29 August 2024, 10:29